Akizindua stand mpya ya mabasi korongwe mkoani Tanga, Rais Magufuli ameweka wazi kikwazo kinachomzuia kutawala zaidi ya "miaka kumi"
Yeye, kwa kutumia "mafumbo katika kuongea ameweka wazi na na kufikisha ujumbe na kutueleza Watanzania kuwa;
"Anaheshimu sana katiba ya nchi" iliyowekwa na wananchi, na kwa maana hiyo Katiba ndiyo "kikwazo" kikubwa kinachomzuia kuwepo madarakani kwa mda mrefu, licha ya kuwa watanzania wanampenda ila katiba ikibadilishwa yupo tayari kuwepo madarakani.
Ni dhahiri kuwa Rais Magufuli, kwa mda mchache aliokaa madarakani(miaka miwili), ameonesha kuwa anaouwezo mkubwa wa kuifikisha Tanzania mahali salama kimaendeleo na katika uchumi na hali nzuri waitakayo watanzania.
Hii inatokana na juhudi zake kubwa katika kulinda na kutetea rasilimali za nchi
kutokana na "mtukufu huyu kukubalika na kupendwa na watu, imepelekea hadi baadhi ya viongozi wakubwa nchini, Rais mstaafu, Mzee Mwinyi na wabunge mbalimbali na pia wananchi kutoka kila kona ya Tanzania kudai/kuomba Rais Magufuli tumwongezee muda.
Kwa hili ningelipenda watanzania tuanzishe mchakato wa kubadili katiba ili Rais Magufuli aweze kukaa madarakani kwa muda mrefu(zaidi ya miaka 10)
Rais ametuambia kuwa katiba ndiyo inamzuia kuwepo kwa kipindi kirefu licha ya yeye kuwa na ndoto za kuivusha Tanzania.
Sasa ni jukumu letu wananchi kuondoa hiki kikwazo ili rais wetu mpendwa aweze kuendelea kuwepo madarakani.
Watanzania wengi tumemwelewa na tumempenda ni Rais jasiri, mkweli na muwazi, anayetekeleza na kutenda watakavyo wananchi pia sio fisadi wala mwenye tamaa na pesa kama wafanyavyo wengine kujilimbikizia mali wawapo madarakani.
###Magufuli baki madarakani##
Sent using
Jamii Forums mobile app