Rais Magufuli njoo vyuo vikuu ujionee. Manunuzi ya magari ni suala pana kuliko linavyotajwa mbele yako

Ni hela za CSR ?
 
hii nchi ni vituko aisee,

yani matatizo ya hii nchi hayawezi kutatulika bila rais mwenyewe kwenda kukagua mahesabu ya manunuzi???
Kuubadili mfumo wa upigaji ni kazi sana maana wanufaika ni wengi na inapofika huko ushirikiano ni mkubwa na hawaangalii uchama, udini, utaifa, wala ukabila
 
Kuubadili mfumo wa upigaji ni kazi sana maana wanufaika ni wengi na inapofika huko ushirikiano ni mkubwa na hawaangalii uchama, udini, utaifa, wala ukabila
Kweli mkuu kama pale Muhas ndio balaa yan kuna miradi watu wanapiga hata kodi ya serikali haendi na serikali imesahau kutupia jicho katika vyuo vikuu
 
Siamini kama kila kitu ni suala la CCM-CHADEMA. Mambo mengine ni ubovu wa uelewa na kama ilivyoletwa, vyeti vikubwa vya mashuleni bila uelewa. Inakuwaje wewe una digrii 1,2,3 au 4 kama Mwakyembe unapewa taasisi, unasoma utaratibu unakuruhusu kununua V8 nawe unafanya hivyo wakati taasisi hiyo haina hata choo. Haya siyo CCM! Hata CHADEMA wakitawala ni hayo hayo au huenda ni zaidi ya hayo.

Muhimu tujiulize ni tabia inayoanzia wapi? Nami nasema inaanzia shuleni tunakopeleka watoto, tangu wakiwa na miaka 7 wanafundishwa kunyenyekea waalimu na kuanza kuwalimia mashamba. Inafika chuo kikuu profesa anaona ni halali kununua gari la aina hiyo wakati chuo chake hakiwezi hata kujenga hostel. Anapelekewa pesa ananunua V8! Foooolish!
 
Huo mfumo atauendesha nani kama wafanyakazi wote wa kila taasisi ni wazembe?
 
ni sawa kwa upande mwingine,ili ujue kabisa usimeze yai ambalo likigoma kupasuka utashindwa kulitapika.

kila mtu atakufa na msalaba,msala wake.
 
Ikoje policy yao?

Policy Yao gari wanannunua Toyota
Halafu sehemu ya mkataba toyota watafanya
Maintenance na service Hadi likifikisha kilometres 150,000/-

Halafu likifikisha kilometres hizo wanaliuza
Linapigwa mnada ...
Hawakai na gari zilizo zidi kilometres 150,000/..

Kwahiyo hawana kabisa gharama za mabilioni
Za kutengeneza magari kama ambazo
Ziko mashirika mengine ..
 
Bajeti ya utengenezaji magari Serikalini. Unanunua gari mpya tano

Only NHIF ndo Wana policy nzuri
Hawa NHIF wanaoshirikiana na dispensaries kulipa malipo ya tiba isiyokuwepo? Kwa ujumla hapa tuzungumze udhaifu wa taasisi bila kujali ni kununua magari au la. Wengine hadi leo wanafanya sherehe za mamilioni kuaga viongozi. Hiyo niliisikia kule SUA! Hicho ni chuo kikuu, lakini kinatumia mamilioni kuaga viongozi!
 
Ulipoanza na swali eti, 'sheria inasemaje?' nimekumbuka mila yetu ya mkubwa kula firigisi! Yaani wewe uone mtoto pembeni yako hana mboga bado useme mila yetu ni mkubwa kula firigisi! That will be rubbish!
Kwa ufupi ulichokumbushia ni kwamba watu ambao akili ni mbovu, ni hatari kwa maendeleo ya taasisi zetu. KIla wakati watasema Ofisi ya waziri mkuu ilitoa kibali!
 

Hapo Raisi Magufuli hawezi gusa, unafikiri hajui? Alikuwa Mbunge, Waziri na sasa Raisi anajua vizuri sana na ni mnufaika pia wa mashangingi, hivyo sahau hilo swala isitoshe unafikiri hela ya misaada ktk Japani ni ya nini? Hiyo ndiyo sababu Serikali ni wateja wakubwa na wa uhakika wa Toyota kwa maana hununua gari mpya kabisa na full option, hivyo pagumu hapo, ...
 
Issue siyo kwamba magari ya bei hizo, maofisa wa Serikali hawaruhusiwi kuyanunua, hapana isipokuwa ni kwamba yanaruhusiwa kununuliwa na pia kutumika kulingana na hadhi ya ofisa mhusika, ambaye anaruhusiwa kisheria kutumia gari la hadhi hiyo.

Hao unaowalalamikia usikute wamekuwa wakitumia magari ya aina hiyo miaka yote kihalali kwa sababu kama isingekuwa hivyo, tayari wangekuwa wameshachukuliwa hatua au kuzuiwa kabla.

Na kama itatokea kwamba kweli hata hawa nao pia hawaruhusiwi kuwa na magari ya aina hiyo, basi zoezi zima linaweza hata likawa litahitaji "auditing" ya magari ya aina hii kwa nchi nzima kwenye taasisi zote za umma, mithili ya vile lilivyokuwa zoezi la vyeti feki.

Zaidi ni kuwa kama vilevile situation itakuwa kweli iko hivyo kama nilivyoidhania hapo juu, basi kuna uwezekano hata yule aliyepewa adhabu kwa kununua gari la iana hiyo, pengine akasamehewa kwa sababu mazingira ya sehemu zingine kwenye taasisi nyingine nyingi tu yatakuwa yamem-favour kupata msamaha, assuming magari haya yametapakaa sehemu nyingi yakiwa yanatumika na maofisa ambao hadhi zao haziruhusu watumie magari ya aina hiyo.
 
Kama serikali ina nia kweli ya kubana matumizi kwanini hii miaka 5 iliyopita imeshindwa kupiga marufuku manunuzi ya magari ya kifahari?

Kuna ulazima wowote ule wa DAS/RAS/DED/DC/RC kutumia haya magari ya gharama waliyo nayo sasa hivi?
 
Yeye anajua mfumo uko sawa, isipokuwa bado anakiri kuna matatizo ya hapa na pale, mithili ya hili tunalolijadili hapa muda huu.
 
Dhambi kubwa ya mkurugenzi sio kununua gari.... ni kununua gari ambalo ni juu sana ya cheo chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…