Rais Magufuli: RC Dar, Abubakar Kunenge usiwe Sheikh au Padri, badilika uwe mkali

Rais Magufuli: RC Dar, Abubakar Kunenge usiwe Sheikh au Padri, badilika uwe mkali

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Posts
8,270
Reaction score
9,116
Kama kawaida yake Rais Magufuli huwa hafichi hisia zake hasa mambo yanapokwenda ndivyo sivyo katika utendaji kazi, na hii ndio hulka yake.

Maneno haya kayasema leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi stand ya mabasi Mbezi.

Hii ni baada ya ujenzi kusuasua kwa visingizio hafifu.

Nahisi anaweza kuwa mkuu wa mkoa atakayekaa ofisni ndani hili jiji kwa muda mfupi sana asipobadilika, kadhalika pengo la Paul Makonda limeanza kuonekana.

Ni kazi kwako Abubakar, kuamua kufanya kazi kishikaji ili uonekane mwema kwa wale ambao ulitakiwa kuwasimamia barabara, au usicheke na nyani kama ambavyo rais Magufuli hufanya, kulinda kibarua chako.

Sina mengi, kwa mbali namuona mkuu wa wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe akipasha (akila jalamba) kwa nafasi hiyo.
 
Nahisi anaweza kuwa mkuu wa mkoa atakae kaa ofisni ndani hili jiji kwa muda mfupi sana asipobadilika,kadhalika pengo la Paul Makonda limeanza kuonekana.

Makonda naye alinangwa waziwazi kwenye machinjio
 
Godwin Gondwe yupo Ilala? Mamluki banaa. Ninavyojua mimi Godwin Gondwe ni boss wangu Temeke.
 
Pengo la Makonda?
Unakumbuka machinjio ya vingunguti kipindi Cha Makonda mpaka Kuna hela ziI ipigwa ?
 
Sasa mkuu anataka kunenge ashinde na media azurure kwenye mikasino ndio aonekane mchapa kazi.

Kunenge ni mtaratibu na mfata protocol tangu yuko tra pale ata mzee wake ilikua hivyo
 
Yes, maanake huyo hawezi hata kuteka watu hataki kufanya vitendo vitakavyomuudhi Allah.

Kakabidhiwa ofisi na wasioamini katika ukuu wa Mungu, wanaojiona kuwa wenyewe ndio miungu. Ndio hayo hayo yaliyomponza Dr. Assad kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na weledi kitu ambacho miungu hawapendi kabisa.
 
"We suppose to focus according our direction according our environment that's only way we can help our peoples no body should come and say that his there to save the problems of our peoples we are the one we are leader we suppose to change the direction" kiingereza cha jiwe Leo Mbezi
 
Kwa wiki hizi mbili zilizo baki kila msaidizi ataonekana hajiwezi na ndio anaekwamisha maendeleo
 
"We suppose to focus according our direction according our environment that's only way we can help our peoples no body should come and say that his there to save the problems of our peoples we are the one we are leader we suppose to change the direction" kiingereza cha jiwe Leo Mbezi
Alitaka kumlipa Lissu Jana alipoongea na balozi wa USA
 
Mkuu wa Mkoa... ongoza mkoa wako kwa kufuata sheria na kanuni, usipelekeshwe km yule ***** bashite.
 
"We suppose to focus according our direction according our environment that's only way we can help our peoples no body should come and say that his there to save the problems of our peoples we are the one we are leader we suppose to change the direction" kiingereza cha jiwe Leo Mbezi
Your excellency i am just trying to preach but .... but I cant reach you
 
..Mheshimiwa RC ameshatengenezewa mazingira ya kutenguliwa.[emoji1787]
Tulimwambia mwanzoni kabisa ,hili jiji akitaka kuliweza awe kaksi,sasa kajifanya eti yeye poa sana.
 
Back
Top Bottom