Rais Magufuli: Sisi watanzania ni Wamoja tusibaguane kwa makabila, dini na siasa awapongeza CCM na kusema Wapinzani wanaisoma namba

Rais Magufuli: Sisi watanzania ni Wamoja tusibaguane kwa makabila, dini na siasa awapongeza CCM na kusema Wapinzani wanaisoma namba

Huyu anatu
Rais Magufuli amewataka watanzania wapendane na kuacha kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini au itikadi za kisiasa.

Dr Magufuli ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi jimboni Misungwi mkoani Mwanza.

Kadhalika Rais Magufuli amewapongeza wanaccm wa Misungwi kwa ushindi mkubwa walioupata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwaambia Wapinzani wataendelea kuisoma namba.

Source ITV

Maendeleo hayana vyama
Huyu anadhani watanganyika ni mazuzu km yy, ngoja itafika zamu naye ataisoma namba vilevile
 
Cshangai kushuhudia mamilion ya watalii wakija kuangalia viumbe vya ajabu huku Afrika
 
Sawa.
tapatalk_1573980728131.jpeg
 
Juzi kanda ya kaskazini (manyara) mwana lumumba kavunja "UMOJA WA WATU WA KILIMANJARO" (Umoja wa watu wa kaskazini), na amesema hataki kusikia maswala ya umoja huo.

Songwe mwezi uliopita "ADMINI MEKU" aliombwa serikali iwavutie maji kijiji na mwanamke mtu mzima, jibu aliopewa aende akamuombe "MUME WAKE, DIWANI WAKE au MBUNGE WAKE", akiashiria akaombe viongozi wa upinzani waliowachagua eneo hilo (bila ya kujua kama mama huyo ni mwana CCM au MPINZANI).

Kanda ya ziwa leo "MEKU" anasifia maswala ya umoja wao, sambamba akisifia na kutoa pongezi kwa ushindi mkubwa wa CCM.

* Kanda ya Kaskazini marufuku umoja, Kanda ya Ziwa ruhusa na pongezi kwa umoja, Kanda ya Kusini-Magharibi kaombeni misaada wapinzani mliowachagua na umoja wenu.

* Umoja wetu tanzania ndio huo kwenye "SPEECH" ni umoja madhubuti, ila kwenye uhalisia (practical) viongozi hawaoneshi umoja na wanaonesha matabaka wazi wazi.

Unapovunja Umoja wa raia una "ASISI" kitu gani kama sio "DIVISION OF UNION" hata raia wasiwe na umoja wa kusaidiana, kushauriana na kuelimishana pindi mmoja wao anapopatwa na tatizo/shida. Raia wawe na matabaka ya mimi CCM nitasaidiwa, wewe MPINZANI hautasaidiwa.

#Watanzania sijui viongozi wetu wanatuona ni wapumbavu kiasi gani. Sijui mpaka lini wataacha kuchezea akili za raia wanyonge.
Anayemwamini Meko ni wa kuchunguza akili.
 
Sisi wananchi mbona hatubaguani hata kidogo...

Ubaguzi unaletwa na viongozi, kwa kusema maendeleo hayana chama huku wakibagua kupeleka miradi ya maendeleo kwenye maneno yanayoshikiliwa na wapinzaini...



Cc: mahondaw
 
Sisi wananchi mbona hatubaguani hata kidogo...

Ubaguzi unaletwa na viongozi, kwa kusema maendeleo hayana chama huku wakibagua kupeleka miradi ya maendeleo kwenye maneno yanayoshikiliwa na wapinzaini...



Cc: mahondaw
Mbona kawe mbunge ni Halima Mdee wa Chadema lakini CCM inaleta maendeleo kwa kwenda mbele!
 
Hapo nampinga Raisi wetu, kutaka kumiliki Mji wako uliovamiwa na watu ambao siyo asili ya hapo siyo Ubaguzi bali ni lazima. Binafsi nisingependa wenyeji watawaliwe na wageni kama ilivyo Arusha City, hivyo kuutaka Mji wako siyo Ubaguzi bali ndivyo inavyopaswa kuwa.
Mpuuzi na Zezeta
 
Sote ni Watanzania na tupendane kama Watanzania. Ila sote hatuwezi kuwa wasukuma na hatuwezi sote kuishi kama wasukuma.
 
Kabisa ,siasa za ulaghai, kuonewa huruma na majitaka ziwe mwisho na wasiishie kusoma namba za kawaida tu wasome mpaka namba hasi

Yeye ndio kapandikiza siasa za kishenzi nchi hii, hapo alipo anajichekesha lakini anajua fika hawezi siasa za ushindani, na hatakaa aziweze.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Back
Top Bottom