Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

eti mimi nimetoa hela!!!! weee faza wewe? inatoka kwenye mshahara wako?duh
 
huna watoto ndio maana unasema hivyo......subiri uwe na watoto au ufurahie kisa mtoto wa jirani yako kapata mimba na masomo hataendelea tena.
Asikufuru....ukishazaa ni mtihani awe wa kike au wa kiume. tulishawahi kuona watu walisema mwanae akipata mimba atamchinja ila wamepata hawajamchinja na bado wajukuu anacheza nao tena kwa furaha
 
Kwa maadili yetu, haturuhusu ngono hadi ndoa, na hili lidumu milele na milele. Unajijua ni mwanafunzi kwa nini ushiriki ngono... hakuna sababu ya kuhalalisha ngono kwa watoto na hili linawezekana. Maana watoto wa siku hizi wanajiona wao ndio zaidi ya watoto wa zamani... nooo acheni hizo .... bibi na mama zenu walisoma na kujitunza; nyie nani msioweza kukaa bila kungonoka? watoto wadogooo wamekomaa kwa ngono then leo mnataka msome na kunyonyesha!

Huwezi kuwatumikia mabwana 2, masomo na kulea, maliza kimoja kingine kianze. Najua mko humu na mtapovuka to the maximum ... ukweli unabaki pale pale. Hakuna kusoma na kunyonyesha. Na huo ndio msimamo wa wazazi, nitashangaa mzazi atakayekuwa kinyume na hili. Mwanao amebeba mimba, muendeleze kwa namna nyingine sio lazima arudi shule alikochezea bahati yake, mbona wengi tu waliharibu na wakawekewa misingi mingine na wako vizuri kimaisha.

Issue za kubakwa ziko wazi, lazima taarifa itatolewa kabla hata ya mimba kujulikana hii itaangaliwa inasaidiwaje. Na wanaobakwa ni wachache wengi wanajipeleka wenyewe! (Kumbuka utakaporuhusu wabeba mimba utotoni wasome matukio ya kubakwa yatazidi).
 
Well said our President. Jamii ya sasa imepotoka kila Ovu wanataka kuhalalalisha/kutetea. Naona unaanza kurudisha watoto wetu kwenye maadili. Hata baadhi ya Makanisa wamekataa kufunga Ndoa za wenye Mimba ndani ya Shela. Wanataka wanaruhusiwa kurudi kundini na kubariki Ndoa siyo Harusi
 
What happened to the mantra that " if you educate a girl you educate a family (nation)."
 
Kwani kuzaa ukiwa shuleni kunapunguza akili au unapunguza umri? kwa akili kama hizi hatuwezi kufuta ujinga hapa nchini. Kusoma kwa wananchi siyo lazima ufanye kazi ya kuajiriwa bali upate maarifa na namna ya kukabiliana na mazingira.

Akiwafuta shule aangalie pia na upande wa pili wa madhara/matokeo yake make baadae atatoa Pesa nyingi kuzuia maradhi..kuzuia wezi...uchafu...na mengine mengi make waliofukuzwa/kukosa elimu kwa kuzaa watakosa elimu jinsi ya kupambana na mazingira.
 
Je kama mwanafunzi alibakwa? Je mwanafunzi akipewa ujauzito na mwalimu? Matineja wengi hawajapevuka kiakili kiasi cha kujua madhara wanayofanya. Si haki kuwanyima fursa adhimu kama ya elimu.
Hawajanyimwa fursa ya kusoma,ila wamejinyima Fursa ya kusoma shule za Serikali.
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Fungua while Ako wakasome
 
Nilianza nikiwa chuo kikuu. Na ndiyo ikawa salama yangu. Mtoto wako akijifanya mjuaji na kuanza mchezo huo akiwa msingi na upili, na ashike ujauzito, hatasomeshwa shule na serikali, labda umuombee msaada kutoka NGO.
Mkuu hongera sana. Huenda ulibahatika kupata malezi mazuri. Hata hivyo sio watoto wote wanabahatika kupata guidance ktk maisha. Fikiria single mothers, fathers, wazazi wenye conflicts, etc.
 
Namuunga mkono, Ila ingekua vyema haya mambo yakatungiwa sheria ambayo itatoa muongozo kwa wote yaani aliyepata na aliyeweka mimba.

Shule binafsi zipo hazina masharti haya ya aliyezaa au asiyezaa. Bila kufanya hivi watoto wote watapata mimba kigezo akijifungua atarudi tu shule.

Mambo mengi yanazungumzwa tu utawala huu ukimaliza mda wake ujao unakuja na yake. Hapo mimi ndio nnaopenda kinyume na serikali.
 
wana jamvi hili swala la ushoga na usagaji lipo na lilikuepo miaka mingi saana ila kwavile tunaishi katika unafiki uliokubuhu tunajifanya kua tatizo hili linaletwa na wazungu, hayo mambo ya biological disorder yapo na hayaja anza leo wala jana, ukitaka kuutibu ugonjwa kwanza kabisa lazima uukubali kua upo then kitakachofuata ni kuutafutia tiba......

mimi kuna kipindi nilikua naishi nchi fulani na nikagundua kua mashoga na wasagaji wapo na pia kiakili ukimchukulia msagaji kama mwanamke wa kawaida unakosea kwakua hisia zao hazipo uko.....

tutaendelea kujifanya tunakemea na kupinga machoni pa wengi ila sirini hao mashoga wanafuatwa na baadhi ya wanaume rijali kamili ambao wanajulikana kama mabasha au ma top gays na kufanya nao kisirisiri tena tunasikia na wengine ni viongozi wakubwa katika taasisi za kidini na serikali....nachoona hapa kinachostahili kufanyika ni kufanya tafiti za kina ili kujua chanzo cha tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi tena kwa njia za busara....

kijana mmoja baada ya baba yake kugundua kua ni shoga alimtisha tisha sana na kusema atamuua, yule kijana alimwambia kua anajuta kuzaliwa na jinsia ya kiume wakati akiwa na hisia za kike na mwisho wa siku alijiua...

tuacheni unafiki wa kulikataa tatizo ambalo lipo miaka mingi hapa duniani.
Mkuu BRUCE LEE tofautisha kuupigia debe ushoga na uwepo wa ushoga!
Anachofanya mzungu ni kuupigia debe na hivyo ni kuukuza. Sasa unapopigia debe ushoga ni wazi umekusudia kuukuza na sio kuutatua!
 
Mkuu hongera sana. Huenda ulibahatika kupata malezi mazuri. Hata hivyo sio watoto wote wanabahatika kupata guidance ktk maisha. Fikiria single mothers, fathers, wazazi wenye conflicts, etc.
Asante kwa hilo. Mimi nimejilea mwenyewe mkuu.
 
Hivi prison break season ya 5 inatoka lini baada ya ile episode ya 09 jamani??
Nimechoka sana na kufuatilia mambo ya nchi yangu.
 
Naona katika ubora wake wa kuchomekea neno
 
Back
Top Bottom