Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli huo NI UJINGA, kwa kiingereza, IGNORANCE. hata hao unaowahutubia wanashindwa kupiga makofi. Elimu ni HAKI YA MTU. Vile vile Rais siyo wa kuamua na kuelekeza mambo kama hayo. kuna vyombo vinavyohusika katika maamuzi, baada ya michakato. hatukumchagua Rais kutuamulia kila kitu. Rais hana mamlaka ya kuamua nani asome na nani asisome. Mengine inabidi tu tumwambie Rais ukweli wake, kwa sababu yeye ni Msema Kweli na ni mpenzi wa Mungu
 
Tatizo siyo NGOs. Tatizo letu katika suala la mimba ni primitive thinking.
 
Bado naendelea kufanya utafiti , lakini mpaka dakika hii dalili zinaonyesha kwamba DR JOHN MAGUFULI anaweza kuwa ndiye raia wa Tanzania mwenye ROHO MBAYA ZAIDI KUWAHI KUWEPO TANGU KUUMBWA KWA MBINGU NA ARDHI .

He is too aggressive !
usukumani na unyamwezini hatunaga lugha ya kubembeleza,kiazi ni kiazi sio mzizi mnene wenye sukarisukari
 
Kila karne ina watu na mawazo yake. Ni kosa kubwa sana kuwa na mtu mwenye mawazo ya karne ya 10 katika karne ya 20. Very dangerous...
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.



" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.

Mhs Rais kakosea labda haelewi hata watumishi wengi wa kike walipta mimba.
Wengi walitoa wengine wakazaa wakarudi shule ni watu wakubwa.
Peleka hoja bungeni MaCCM wakatae kama kawaida yao.
 
Hao NGO wakajenge shule za Wazazi....kama vipi!
Huo mchezo ni mzuri (tukiwaacha watanogewa na kuzoea)
Itafika wakati kila mwanafunzi (mzazi) anatoka nje kwenda kunyonyesha!
😀😀😀😀😀😀😀😀

Huyu jamaa ana maneno sana...
 
kazi gani kubwa kusomesha wazazi wenzio?labda mkileta changamoto zenu tutawaelewa
hivi inakuaje msomi wa sekondari anshindwa kukwepa mimba au kulaghaiwa?!..usiniletee habari za kubakwa,utakuta anatiwa mimba na mtu asiyejua definition ya physics!
 
Dereva punguza mwendo, Lori letu lina pancha.
 
Mkuu BRUCE LEE tofautisha kuupigia debe ushoga na uwepo wa ushoga!
Anachofanya mzungu ni kuupigia debe na hivyo ni kuukuza. Sasa unapopigia debe ushoga ni wazi umekusudia kuukuza na sio kuutatua!

Nimekuelewa mkuu, ila tatizo linabaki palepale kuukemea ushoga na usagaji bila kuwa na suluhisho na bila kutatua chanzo cha tatizo hilo bado tunakua tunatwanga maji kwenye kinu, swali la msingi ni kwamba je ushoga upo? then tukishakubali upo sasa tujiulize je chanzo chake ni kipi? napia ni kwanini unakua kwa kasi? hapo sasa ndio mbinu na njia za kuzuia au kutibu tatizo hilo zitumike...nadhani tumeelewana.
 
Jamani hotuba za Magu haziunganiki, huwezi ukakusanya mtiririko wake ukatengeneza kitabu.
 
Ndo wawataje wabakaji. Mara nyingi wabakaji wamekuwa wakiachwa tuu wawabebeshe mimba wanafunzi wwngine.

Kwa hili nipo upande wa Rais.
Ukibakwa nenda mahakamani. Mbakaji afungwe wewe uzae na usomeshwe.

Usipopeleka mbakaji jela zaa na hamna kusoma.

Maana kuna wengine wanajitakia kabisa. Ni kiherehere chao.

NB: ukifanya mapenzi na binti umri chini ya 18 Umebaka. Subirini maembe yaive. Kuna Team Wasaka Bikra ndo wanaharibh watoto.

Kwa wanafunzi wasikaribie mazingira hatarishi, watahatarisha Elimu zao.
Umejenga hoja yako vizuri sana mkuu na binafsi umezidi kuongeza uelewa wangu kaitika hili at first hand.

Hofu yangu inakuja pale ambapo anko Magu kasema kAMWE hatamsomesha mwanafunzi aliyezaa (mzazi). To my level of understanding capacity na kama sijamnukuu rais vibaya ni kwamba je kwa mfano binti (mwanafunzi) kabakwa na kupata mimba hata akimtaja mbakaji bado haitaondoa ukweli kwamba kapata mimba.

Na hapo ndio swali langu na hofu inapoanzia kabakwa kapata mimba, kaenda polisi kushtaki na kafanikiwa kumtia mbaroni mbakaji wake. Rais kasema hatamsomesha mzazi (mwanafunzi aliyekwisha jifungua).

Kwa mantiki hiyo hata kwa mfano kama mwanafunzi kabakwa na akafanikiwa kumshitaki na kumtia mbaroni mtuhumiwa wake atasaidiwaje? Mind you anko kasema katu hatosomesha wazazi.
 
Vijana wasome waache starehe,kubebana bebana inasababisha wasisome wanajua hata kesho ntasoma....ni kuchagua tu starehe au kusoma,Wanaopata mimba kwa kesi kama za kubakwa ni chache sana wengi wao hujiachia sana matokeo yake Mimba huwaumbua kisha hujifariji wataenda shule wakijifungua...
Mimba, Nyumbani.
Ni mtazamo tu.
 
Back
Top Bottom