Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Sjapotoshwa niko makini sana!!
Sema tatizo langu mimi siyo muumini wa mawazo ya ghafla hasa ya kiongozi mkubwa kama raisi wa nchi.

Hakuna anae unga mkono ama kutetea wanafunzi kupata ujauzito wakiwa shuleni.Ama kutetea utovu wa nidhamu kwa wanafunzi.

Lakini Ni mhimu kutafakari kwa kina njia sahihi ya kunusuru hatima ya mabinti Na Dada zetu kabla ya kuwahukumu wakati sababu za wao kupata mimba wkiwa shuleni Ni nyingi mno.

Aidha,Kuhusisha NGO's kwenye hili na kubeza mchango wa NGO's Ni utovu wafikra chanya Na Ni uvivu wa kufikiri.

Mfano Leo hii utabeza mchango wa tafiti za haki elimu kwenye hili @kwasababu raisi kasema!!!?

Lengo la mwanafunzi aliyepata ujauzito kurudi shule bada ya kujifungua lilikuwa Ni kutaka kutoa nafasi ya pili kwa wanafunzi hasa wenye uwezo Na nia ya kurudi darasani kurekebisha makosa yao ama wale ambao walikuwa Ni wahanga wa matukio ya ubakaji ama kurubuniwa Na wanaume watu wazima au vinginevyo kupata hatima njema kielimu.

Hili lilikuwa Ni wazo zuri sawasawa Na kutoa frusa kwa waliofeli kidato cha pili kukariri darasa ama waliofeli kidato cha nne kurudia mitihani.

Wenye ufahamu wanajua fika Mazingira ya shule za serikali hasa za kata Ni hatarishi sana Na ndio chanzo kikubwa kikifuatiwa Na umasikini wa kipato katika familia pamoja na ukosefu wa maadili katika jamii.

Kuchukulia kigezo kimoja tuu cha utovu wa nidhamu Na kukosa maadili,kuwahukumu wanafunzi wa kike Na kuwanyima frusa ya pili kupata haki ya elimu Ni uvivu wa kufikiri narudia tena Ni uvivu wa kiwango cha juu sana!!!

Kwanza shule nyingi za serikali zinahamasisha sana mihemko na fikra za ngono kwa vijana wetu hatimae mimba kwa wasichana.

Mfano...
Shule nyingi hazina mabweni
Hazina maabara
Hazina makitaba
Zipo mbali Na makazi ya wanafunzi(hasa vijijini)mwanafunzi anatembea umbali mrefu Na njaa kali

Upande wa pili
Walimu hawatoshelezi hasa masomo ya sayansi
Hakuna nyumba za walimu
Mishahara duni n.k

Nyumbani kipato duni Na umaskini wa kipato n fikra hasa kwa wazazi waliowengi nayo Ni mimba nyingine.

Katika mazingira ya namana hii huwezi kuzalisha kizazi chenye fikra chanya hata kidogo mana wanafunzi na walimu woote wanawaza nje Na taaluma.

Wakati mtoto wa private yuko maabara akifanya mfunzo kwa vitendo ama makitaba akiwekeza ufahamu kwenye ubongo....

Mwanafunzi wa shule ya kata atakuwa anapiga kelele darasani ama akiwa Na msongo wa mawazo atarudije nyumbani Na akifika atakula Nini!!n.k

Alafu out of the blues mtoto anapata mimba unakrupka kaa ulee mtoto hapa hakuna shule bila kujiuliza sababu ama nini hatima ya binti yako Na mjukuu.!!

Namkubli JPM kwa mengi lkn pia sikubaliani nae kwa mengi hasa Hili la kuwanyiwa second chance wanafunzi Wangu ambao kimsingi Ni wahanga wa mfumo mbovu wa elimu nchini.

"I have the freedom to disagree with you just as you have the right to defend your mediocrity and ignorance"





Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
Ni hoja dhaifu sana ambazo zina nia ya kuzidi kuingiza jamii yetu kwenye dimbwi la immorality.Hii haikubaliki na hatutakubali.Ni wazi kwa mtu yeyote anayelitakia taifa letu mema kwamba maamuzi ya kuwaruhusu wanafunzi waliopata mimba na kujifungua warudi shuleni yanahamasisha umalaya.You do not need a PhD to know this.Hili hatuko tayari kulivumilia.
 
tujifunze na sisi kuwa na mambo yetu, na viwango vyetu vya maadili ambavyo tunavisimamia.
NGO na wafadhili wake ambao wengi ni wazungu wasilazimishe kuleta mambo ambayo sisi hatujaona maana yake.
Mkuu usibwabwaje sana hii si utamaduni au kesi ya maadili ni suali la haki ya mtoto awe qa kike au wa kiume !utovu wake wa adabu ipo adhavu yake ataondolewa shule kwa wakati ule laki i sio kumpa total ban asisome!babu yetu nyerere hakufundisha watoto waliozaa tu hadi babu na bibi zetu walifundishwa ngumbaru at least waweze kuandika ndio au hapana siku ya uchaguzi wa enzi ya chama kimoja!
 
Nawaonea huruma sana Watanzania. Ushabiki umeleta msiba kwa taifa.
 
Huwezi kusomesha wajawazito,, dunia nzima hakuna, hata ULAYA hawafanyi hivyo, Ukizaa unasoma kama mtu mzima, ukichanganywa na watoto wataiga mwenzao,,kale kamchezo lazma kawekewe sheria
asa mazingira ya elimu ulaya unaweza kulinganisha na uku kwetu??? ushawahi jiuliza sababu za mimba za utotoni ni nini??? mana wengi ni watoto.
 
Inasiktisha sana...

Adhabu ya kutorudi shule ni ndogo sana... Hapo aliyempa na aliyepewa wote wawajibishwe... Adabu lazima iwepo...


Cc: mahondaw
 
Huwezi kusomesha wajawazito,, dunia nzima hakuna, hata ULAYA hawafanyi hivyo, Ukizaa unasoma kama mtu mzima, ukichanganywa na watoto wataiga mwenzao,,kale kamchezo lazma kawekewe sheria
Ulaya kiwanda ni vyerehani vinne?
 
asa mazingira ya elimu ulaya unaweza kulinganisha na uku kwetu??? ushawahi jiuliza sababu za mimba za utotoni ni nini??? mana wengi ni watoto.

muulize ulaya ipi?,wakati watoto wengine walikua wanapewa hela kidogo ili wakae kwenye education(zamani lakini)
 
Tatizo siyo NGOs. Tatizo letu katika suala la mimba ni primitive thinking.
Mkuu NGOs zimefanya kazi kubwa ya indoctrination, na hatimaye kubadili mitizamo ya watu.Usi down play their contribution,it's huge.
 
Hapana,ukiliangalia suala hili kwa jicho la tatu ni sahihi kabisa alichosema Rais, hii ilikuwa inakatisha tamaa sana waalimu, pia maadili ya kijamii sio sahihi.Inawezekana vipi binti azae akiwa shuleni halafu tena arudi shuleni,hivi si atawadharau walimu kuwa hakuna kigeni asichokifahamu kuhusu mambo ya mapenzi? Si atawafanya wenzake waone ni sawa kujihusisha na ngono?Wakipata watoto si ruhusa kusoma tu? Kutakuwa na nidhamu kweli shuleni? Tunaimbishwa nyimbo za kijinga na wazungu nasi tunaimba na kuzifuata. Tumeletewa haya mafikirio ya wanaume kuoana wenyewe kwa wenyewe bado tunaona wapo sawa. Hivi kweli ambayo wanayapigia kelele tuyafuate na kuyafanya ambayo ni kinyume na utu anapotokea kiongozi kuyakemea bado tunalaamu tu na kuangalia kura? Viongozi wasifanye kazi eti kwa sababu kuogopa kutokosa kura? Za nani, zako au na za wengine wanaoona katazo hili ni sahihi kabisa? Tuwe na mishipa ya aibu kutotetea upuuzi tunaojazwa na hawa ngozi nyeupe. Yaliyo mazuri tuwakubalie, lakini ya udhalilishaji tuyakatae katu. Hizi NGO,s zinasapoti kwa sababu wanataka fedha, ila kwenye familia zao kimoyomoyo hawataki kusikia hicho kitu, waswahili walisema, pesa sabuni roho.Hivi huko majuu watoto waliozaa shuleni wanarudi tena shuleni kuendelea kusoma wakinyonyesha?Katazo hili litafanya watia mimba washughulikiwe hivyo kuleta woga wa mimba kwa watoto wa shule. Rais yupo sahihi kwa katazo hili.
Mimi naona tunahangaika bure wanaopata mimba ni wale ambao siyo wajanja. Watoto wa siku hizi wanajua kila kitu kukupita mtu mzima maana wanatumia kinga vidonge nk ndiyo maana siku hizi unaona binti mdogo ndiyo kwanza kaolewa uzazi umegoma wewe unafikiri matatizo mengi ya uzazi yanaletwa na haya madawa mtoto ameanza kumtumia tangu ana miaka 15
 
nyoosha nchi mkuu watanzania bado hawajaluelewa ila watakuelewa tuu kila kukicha
 
Bora angemtuma msemaj wake ayaseme hayo maneno,ni mazito kwa cheo chake kuyasema,yaan bas tu, kwel hapa kaz tu na kwel ni kaz tu,hakuna kuremba.
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

Kasema waende VETA au wakajifunze cherehani..... all other dreams will be shut down.... sad
 
Sawa sawa....
.
.nakupingaga sana mzee ila katika hili tupo pamoja ,
.
.wazaz watengeneze mazngra mazur kwa watoto kusoma...
.
.ufatiliaj uongezeke ,
.
.sio kuwaachia walimu tu...
.
.hv ni ushawah kujiulza ni kwann wanaopata mimba wakiwa shulen wengu huwa ni wa shule za serikari?? Kwann sio private ????
 
Wanafunzi wanaopata mimba wengi wao hawana akili, wabaki nyumbani na kulea.

Mzazi kama huna pesa ya kusomesha private mkanye mwanao.

Hii ni sababu kubwa ya umasikini Tanzania, tunawaza ngono, tunapenda ngono na tunatetea ngono.
 
Back
Top Bottom