Sjapotoshwa niko makini sana!!
Sema tatizo langu mimi siyo muumini wa mawazo ya ghafla hasa ya kiongozi mkubwa kama raisi wa nchi.
Hakuna anae unga mkono ama kutetea wanafunzi kupata ujauzito wakiwa shuleni.Ama kutetea utovu wa nidhamu kwa wanafunzi.
Lakini Ni mhimu kutafakari kwa kina njia sahihi ya kunusuru hatima ya mabinti Na Dada zetu kabla ya kuwahukumu wakati sababu za wao kupata mimba wkiwa shuleni Ni nyingi mno.
Aidha,Kuhusisha NGO's kwenye hili na kubeza mchango wa NGO's Ni utovu wafikra chanya Na Ni uvivu wa kufikiri.
Mfano Leo hii utabeza mchango wa tafiti za haki elimu kwenye hili @kwasababu raisi kasema!!!?
Lengo la mwanafunzi aliyepata ujauzito kurudi shule bada ya kujifungua lilikuwa Ni kutaka kutoa nafasi ya pili kwa wanafunzi hasa wenye uwezo Na nia ya kurudi darasani kurekebisha makosa yao ama wale ambao walikuwa Ni wahanga wa matukio ya ubakaji ama kurubuniwa Na wanaume watu wazima au vinginevyo kupata hatima njema kielimu.
Hili lilikuwa Ni wazo zuri sawasawa Na kutoa frusa kwa waliofeli kidato cha pili kukariri darasa ama waliofeli kidato cha nne kurudia mitihani.
Wenye ufahamu wanajua fika Mazingira ya shule za serikali hasa za kata Ni hatarishi sana Na ndio chanzo kikubwa kikifuatiwa Na umasikini wa kipato katika familia pamoja na ukosefu wa maadili katika jamii.
Kuchukulia kigezo kimoja tuu cha utovu wa nidhamu Na kukosa maadili,kuwahukumu wanafunzi wa kike Na kuwanyima frusa ya pili kupata haki ya elimu Ni uvivu wa kufikiri narudia tena Ni uvivu wa kiwango cha juu sana!!!
Kwanza shule nyingi za serikali zinahamasisha sana mihemko na fikra za ngono kwa vijana wetu hatimae mimba kwa wasichana.
Mfano...
Shule nyingi hazina mabweni
Hazina maabara
Hazina makitaba
Zipo mbali Na makazi ya wanafunzi(hasa vijijini)mwanafunzi anatembea umbali mrefu Na njaa kali
Upande wa pili
Walimu hawatoshelezi hasa masomo ya sayansi
Hakuna nyumba za walimu
Mishahara duni n.k
Nyumbani kipato duni Na umaskini wa kipato n fikra hasa kwa wazazi waliowengi nayo Ni mimba nyingine.
Katika mazingira ya namana hii huwezi kuzalisha kizazi chenye fikra chanya hata kidogo mana wanafunzi na walimu woote wanawaza nje Na taaluma.
Wakati mtoto wa private yuko maabara akifanya mfunzo kwa vitendo ama makitaba akiwekeza ufahamu kwenye ubongo....
Mwanafunzi wa shule ya kata atakuwa anapiga kelele darasani ama akiwa Na msongo wa mawazo atarudije nyumbani Na akifika atakula Nini!!n.k
Alafu out of the blues mtoto anapata mimba unakrupka kaa ulee mtoto hapa hakuna shule bila kujiuliza sababu ama nini hatima ya binti yako Na mjukuu.!!
Namkubli JPM kwa mengi lkn pia sikubaliani nae kwa mengi hasa Hili la kuwanyiwa second chance wanafunzi Wangu ambao kimsingi Ni wahanga wa mfumo mbovu wa elimu nchini.
"I have the freedom to disagree with you just as you have the right to defend your mediocrity and ignorance"
Sent from my TECNO-J8 using
JamiiForums mobile app