One In a million huyo ukweli usemwe tu Nchi itoe Tangazo kuwa atakaepata mimba arudi shule wanafunzi watasoma kweli? ukijua saikolojia ya watu walio katika mobb maamuzi kama hayo ya kuwaruhusu ni sawa kumfunga mfugo katika shamba la mazao!! Naomba nikuulize ile ishu ya mbeya day iliishaje baada ya wale wanafunzi kutetewa sana na ukweli ulipojulikana ni hatua zipi zilichukuliwa??
Tanzania lazima ibaki katika misingi yake kulinda maadili yanayoporomoka kila siku leo mnapiga kelele kwa huyu inaonekana mmesahau kauli ya "viherehere vyao" ya mtangulizi wake yote ni katika kusaidia kizazi cha watanzania na si kuendekeza mambo yasiyo na maadili kama hayo.
Kesi za kubakwa naamini zinaripotiwa katika maeneo husika na mwanafunzi kama huyo sidhani kama kuna kosa la kuendelea na shule kama kweli atathibitika alibakwa. Lakini si kuruhusu watu wa do na wapate mimba then warudi shule Hilo HAPANA.
Kulinda maadili yapi? Unajua unajifanya utasema Tanzania tuliwahi kua na kitu cha kujidai huko nyuma, hakuna hata kimoja, huko nyuma wazee walikua wanabaka tu wanawake bila consequences, hata leo hii vijijini ni hivyohivyo, angalau tena imepungua miaka ya hivi karibuni.
Tunang'ang'ania misingi ipi wakati hatuna lolote tumefata tunachojua miaka mingi toka tupate uhuru na bado nchi masikini ya kutupa. Watu eliku hawana, viongozi hata kusoma wengine hawajui. Hivi we unavyoona unaona tuna cha kujidai kweli? Toka nje uone.
Hizo nchi mnazosema watu wanatembea uchi nimeishi miaka zaidi ya 8 sasa, wadada kutembea na vikaptula vidogo sana vinabana hamna anayewasumbua, hamna ubakaji uliokithiri ka bongo, na watoto wana heshima, uvaaji wanaona kitu cha kawaida tu sio kukaa wanakodoa mimacho ka wabongo. Ila juzijuzi tu huko wametaka kumvua dada wa watu nguo mbele ya watu kisa kavaa miniskirt, kuna joto avae vipi sasa?
Yaani watanzania mmekaa kwenye bubble ya ujinga mko comfortable mnahisi the whole fckn world revolves around you, hamna cha kujidai Tanzania HATA KIMOJA, ni muda tubadilike tuige sasa mazuri wanayofanya wengine.
We unadhani kila aliyepata mimba alipenda? Dont be stupid, angekua mtoto wako ungejua uchungu wake ulivyo, sometimes shit happens, mlee mtoto vizuri na mpe elimu ajue jinsi ya kujikinga sio mnakaa kutoa adhabu za kipumbavu, sasa mdada aache shule, mkaka jela 30years, huyo mtoto anayeletwa duniani hivi ataishia wapi kama sio kuzoa takataka? Mama kazi hawezi pata, baba jela. Umeongeza watu watatu kwenye umasikini bila sababu ya msingi.
Akili ndogo. Mnaboa aisee