Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Busara inasema kati ya maovu makubwa mawili, chagua ovu lililo jepesi. Hivyo mwanafunzi aliyekatisha masomo kwa sababu ya ujauzito na akarudi kusoma ni kuchagua ovu jepesi. Na Magu akumbuke kuwa ukimwelimisha mwanamke, umeelisha familia nzima! Hivyo ni busara wanafunzi wazazi wakarudi kusoma provided wana nia bado ya kupata elimu.
 
Hiyo mimba kainunua dukani?
1: Kavua pichu kalalia mgongo akaruhusu aingiliwe kupata uroda.
2: Binti kubakwa kuna mazingira aliyatengeneza( kukaa ghetto za wavulana peke yako)
3: Kushinda kwenye masoko, magulio hadi usiku
4: Kudanganywa na vitu vidogo ( simu, chips mitumba(Nguo)
5: Kutokuwasikiliza vizuri wazazi walezi waalimu.
UBAKAJI HAUJI HIVI HIVI TU.
Tema mate chini wewe.... na wale watoto wa miaka miwili wanabakwaga gulioni??? Wanaobakwa na baba zao ni gulioni huko... fikiria kabla hujaropoka
 
Baada ya kumsikiliza Mh Rais kwa umakini na kwa tafakari kubwa nimeona kuna kasoro kubwa ambayo ipo katika sera na sheria zetu kama nchi hasa kuhusu masuala haya.

Napenda niende moja kwa moja alichosema Rais leo ni sawa kabisa hata mimi siwezi kusomesha mtu aliyezaa akiwa shule kwa kujitakia tatizo linakuja sio wote walio pata mimba shuleni walipenda, wengine walibakwa na wengine ni kutokana na changamoto za kiuchumi na kijamii ikiwepo ukosefu wa mabweni shuleni, umbali kutoka nyumbani, ugumu wa maisha na hata ushawishi wa aliyempa mimba mfano mwalimu au kiongozi.

Sasa basi katika hili sera na sheria zetu ikatoa adhabu sio tu kwa aliyebeba mimba na aliyempa mwenzie mimba bali kwa wote hata na wasio husika

Ntaelezea wasio husika ni kina nani

1. Mzazi, huyu anaweza kuhusika au asihusike lakini sheria inamudhibu

2. Mtoto atakaye zaliwa, katika hali ya kawaida huyu ahusiki hata kidogo juu ya makosa ya baba au mama yake lakini sheria inamudhibu vikali tena pengine kuliko wote. Kwanini nitaeleza

Hebu fikiria wanafunzi wawili wa kike na wakiume wana mahusiano ya kimapenzi Mwanafunzi wa kike akipata mimba atafukuzwa shule na yule wakiume atafungwa miaka 30. Maana yake mtoto atakaye zaliwa atakuwa na mama kilaza maana hakumaliza shule lakini pia atakuwa hana baba wa kumlea kwa kuwa baba yuko jela. Hivyo basi mtoto atakua kwa shida na wengi huishia mtaani kama adhabu ya kosa la wazazi wake.

NINI KIFANYIKE

1. Nashauri sheria na sera zetu ziwe na exceptional option yaani kwa mfano Endapo itatokea mazingira kama hayo yametokea mama yaani aliyepata mimba ndio awe final say katika decision ya nini kifanyike kwa baba yaani aliyempa mimba kama atachagua kumfunga basi afungwe la ataki basi aachwe walee mtoto wao.

2. Mtoto wa kike aliyebakwa au kupata mimba kwa makosa ambayo ni ya sisi Jamii mfano ukosefu wa mabweni kama atutaki arudi shule basi tumpeleke vyuo vya ufundi stadi kama VETA ili apate ujuzi wa kumuwezesha kumlea mtoto angalau tuepuke laana ya kumuadhibu mtoto asiye na hatia kama taifa.
 
Kauli ya Rais ina mapungufu makubwa sana. Kama serikali kuna njia na mikakati ya kudiscourage upatikanaji wa mimba kabla ya wakati au zisizo hitajika sio kutosomesha na ma kuwafunga wale wa kiume walio wapa wa kike mimba. Kwanza they are minor, hata wanaweza wasifungwe kisheria.
 
Too brutal from the president. Anasahau kabisa kwamba nchi yetu kuna mfumo dume. Tena yeye amekuwa kielelezo cha huo mfumo dume.
 
Hapa tupo sawa mkuu hawa watoto wanakimbilia vitu vizuri wache wapate kupanga ni kuchagua kama anataka mimba basi akae akuze mwana
 
Labda tujiulize elimu inatolewa kwa ubaguzi?
Ni haki kwa watu kupata elimu?
Kupata mimba kunazuia mtu kuelimika?

Serikali iweke shule maalumu kwa wote watakao kumbwa na hilo jambo. Hiyo tu itawafanya waone pia ni kosa.
Kuruhusu pia haina maana ndio itaruhusu mimba kwa watoto,maadili yetu bado yapo vilev ile.
 
Tatizo lake yeye, Ndalichako, Salma Kikwete na wengineo wanaotetea huo upuuzi ni kuwa misinformed.

Sera za dunia zinaandaliwa kisayansi sio moral view points labda kwenye nchi zilizo na misimamo mikali ya kidini.

Ni hivi kigezo cha afya bora kwa tafsiri ya WHO sio kukosekana kwa maradhi tu bali usalama wa mtu kwa ujumla wake ikimaanisha mazingira bora ya kila siku, kuwa na elimu ya kutosha kumwezesha kufanya maamuzi sahihi (saa zingine mtu anapata magonjwa ya maambukizi au anabeba kisa elimu tu ya kujua umuhimu kutumia kinga), ushirikiano wa mtu na familia na jamii (inawezekana kuna watoto wanapata hizo mimba kwa sababu wazazi awawezi kuwapa ata basic needs zao) etc.

Ndio maana kwenye afya kuna arguments za health inequality wenye mapato mazuri kawaida wanaweza ishi zaidi kwa sababu wanapesa za kupata access ya huduma bora ukienda muhimbili utakuta wazazi na watoto wanaokufa kwa uzazi ni wale wa chini kuliko matajiri, wanaelimu ya kuzuia magonjwa ambayo chanzo chake ni lifestyle, etc.

Kwa hivyo kwa jicho la NGO kupambana na elimu ya watoto wanaopata mimba sio kuleta agenda zao la hasha wao wanachoongalia ni 'social factors' zinazoleta health inequality ata makwao hilo ni tatizo sugu utakuta sehemu zinazopishana kilomita mbili tu kuna gap ya life expectancy ya zaidi ya miaka kumi uwezi kuzi ignore hizo kama causes.

Tatizo serikari yetu aifikirii kupambana na hizo changamoto wanachojua wao ni kwamba dawa ya kikoozi kata kimeo kama tiba kwenye kila kitu.

Ni hivi hii nchi kuendelea tunahitaji proper succession serikari imejaza watu wengi sana wasio na uwezo na wanaopanda madaraka kwa namna za kujipendeza lakini ubunifu ni zero na Ndalichako Phd yake inatakiwa ichunguzwe mama kwa kauli tu she is not technical mimi nakataa Ndalichako kama Phd yake ni halali.

Mi baba yangu aliniambia kuna watu na maeneo waliotoka hata asome vipi watabaki wapumbavu elimu haiondoi upumbavu at least ujinga inaondoa
 
kazi ipo, kwa hiyo na vijana wa kiume waliozaa nao wasiendelee na shule kwa sababu ni wazazi??
mtoto wa kike kupata mimba ni suala la jamii nzima,
asiporudi shule atamlea vipi mwanae??
 
Only Tanzania huu upuuzi ndio upo, halafu mnataka nchi iendelee ikiwa mnawanyima watoto wa kike Elimu kwa kisingizio cha kipuuzi, eti mimba.
Wanaowatia watoto wa kike mimba utawajua tu! Halafu wanakuja hapa kulia lia utadhani wanawaonea huruma kumbe ni unafiki mkubwa! Hongera JPM umetumbua hili jipu! Lazima tuambizane ukweli! Ukibeba mimba ushakuwa mzazi! Shuleni siyo mahali pako tena, anza kujiandaa kulea MTOTO wako! Watoto wa kike na wazazi wanataka kusikia kauli thabiti kama hizi ili wachague kusuka au kunyoa!
 
Rais Magufuli hapo umekosea sana. Hawa watoto wanapata ujauzito wengine wanapewa na mawaziri wako, na wengine waalimu wao wanaowafundisha, wengine wanabakwa na wengine kwa umasikini. hatua zako unarudisha taifa hili kwenye umasikini mkubwa

Hapo Rais Magufuli kakosea sana tena Sana. Watoto watakoadhirika ni watoto masikini, watoto matajiri wataendekea na masomo. Sasa naamini Rais Magufuli ana mawazo ya kizamani sana, Pamoja na kazi nzuri unayoifanya, kwa hili unauwa wanyonge na huwasadii. Elimu yetu iko nyuma, kwasababu wazazi wengi hawajasoma, kuzuwia watoto wasiendelee na masomo Rais Magufuli atalifanya taifa hili lisiendelee, kwani tutakuwa na wazazi wengi wadiyosoma. Hapa Rais Magufuli amenisikitisha sana. Mzazi asiyesoma mala nyingi hasomeshi watoto wake. Wazazi wa Tanzania wengi wetu hatutali elimu ya watoto wetu, Hii ndiyo maana tuko nyumba kwenye education, na kwa maamuzi ya `Rais taifa hili halitaendelea hata alivute na Kamba bila ya elimu kwa wote. So far kuna record kubwa ya wanafunzi wamepata ujauzito, hawa ni wazazi wasiokuwa na elimu na kama hawataruhusiwa kuendelea na elimu, basi taifa hili litakuwa la wajinga Wakati jirani zetu wanaendelea kusomesha watoto wao.. Mawazo haya ni ya kizamani, aliyemshahuri Rais Magufuli kufuata njia hii amemchonganisha na watu wengi wenye kupenda haki kwa wote.
 
Lakini sasa katiba inasemaje kuhusu marufuku hii??

mana haya maneno ni matam sana kuyatamka watu wakakupigia makofi.

Angetupa na kumbukumbu ya katiba kwanza kuhusu haki ya elimu kwa kila mtz kama katiba haikuweka wazi alete katiba mpya ili sasa hii iwe ni sheria kwa mujibu wa katiba otherwise hizi porojo tukienda kwa Mahakamani zitakuwa hazina mashiko.
 
Je kama mwanafunzi alibakwa? Je mwanafunzi akipewa ujauzito na mwalimu? Matineja wengi hawajapevuka kiakili kiasi cha kujua madhara wanayofanya. Si haki kuwanyima fursa adhimu kama ya elimu.

Sio tu na Mwalim hata mawaziri wake, kwa hiyo Waziri atabaki kazini, mtoto wa kike ndiye atapewa adhabu. Kodi za Watanzania zitumiwe kunufaisha maisha ya Watanzania wote.
 
Back
Top Bottom