safi kabisa mh Rais wakishindwa kujitunza watafute QT,shule sio za wazazi,wazazi watumie utaratibu wao uliowekwa,hizo NGO zinapiga hela hazina lolote.
Utaratibu wao upi!?
NGO hapa zinahusikaje,mkuu!!?
Mana wengi wa wanaharakati wa NGO's utetezi wao Ni kupunguza Na kudhibiti mimba shuleni.
Na ikitokea mschana akapata mimba wanashauri asitengwe ama kunyanyasika katika jamii apewe nafasi alee mimba yake, ajifungue Na akishakisha jifungua apewe nafasi ya kumalizia masomo pale alipoishia.
Na serikali zilizopita kabla ya awamu ya tano ziliridhia hili Na ziliunga mkono juhudi za NGO's katika hili.Hata baadhi ya mawaziri wa awamu ya tano wanaohusika Na masuala ya Elimu,afya,jinsia,wanawake, watoto Na tamisemi waliliskika Mara kadhaa wakitetea future za Waschana waliopata mimba kupewa frusa ya kuendelea Na masomo!!
Kabla ya kauli ya raisi hata wewe ulikaa kimya wala hukuwahi kujitokeza hadharani kupinga lkn kwa kuwa maamuzi ya watanzania waliowengi hufuata mitazamo ya wanasiasa wanao waamini ama ushabiki Na siyo weledi wa kitaalamu ndio mana Leo hii sishangai kuona mnashambulia NGO's kana kwamba hakuna kilichofanyika Na hakuna kinachofanyika.
Ushauri wangu serikali itamke Na iweke wazi kwa vitendo Ni utaratibu upi rasmi utatumika kuwapa nafasi wanafunzi wenye mimba badaa ya kujifungua kupata elimu.
Na si hao tuu hata wanaofeli darasa la saba, kidato cha nne Na cha sita.
Nasema hivi kwa sababu tukiwaachia wanasiasa waamue kila Jambo kwa hekima zao tuu,bila kuhoji hatima ya maamuzi yao siku mambo yakiharibika sisi wengi ndo tunaumia.
Ipo mifano mingi!! Mfano mzuri Ni madudu yaliyofanyika Sekita ya madini Na uwekezaji.
Elimu yetu iko ICU...watoto wanafaulu darasa la Saba kwa 80% hadi 90%
Wanafika sekondari wanafaulu 15% hadi 20% wengine woote wanafeli wanarudi mtaani bila vyeti wala weledi serikali Na wanasiasa wanakaa kimya,wazazi wanakata tamaa
Vijana wanakata tamaa tunabaki Na kizazi cha kulalamikia ugumu wa maisha Na kushabikia wanasiasa ama kuumizana.
Tunataka serikali ije Na majibu ya maisha ya watoto Na vizazi vijavyo.
Mana hawa watoto ndo wazazi wa kesho woote wakiwa mafundi Nani atakuwa daktari,mwanasheria ama mwalimu!!?