Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Sema wewe hujaona maana yake siyo sisi! Wewe unaona ni haki mtoto akipata ujauzito asirudi shule? Kwanini anyimwe haki yake ya kikatiba ya kupata elimu, kwanini apewe adhabu mara mbili. Halafu hujui tu hii ni kwa ajili ya watoto wa masikini wanaotegemea shule za serikali
Nyie ndio mnalazimisha hata wasiotaka shule na walio feli waendelee na shule ili NGOS ziendelee kupata misaada ya wazungu bila kujari muda anaopoteza huyo mwanafunzi
 
Taifa lazima Liwe na sheria tena zile ambazo kama Taifa litajuvunia. Mimba za utotoni sio maadili yetu .huku wazungu sio wanapata mimba hizo utotoni unadhani ni Serikali. Familia. Long lived traditions. Nk wee kazana kutetea ujinga
Hawa wanaompinga JPM siwaelewi kabisa,eti wanamtetea mwanafunzi lakini hawamtetei haki za kichanga kitakachokuwa kimezaliwa. Mama akiwa shule haki ya huyo mtoto itapatikanaje?
Viva JPM wazazi walee,kuna fani nyingi watajifunza hukohuko nyumbani
 
Hata private kama uongozi uko makini haitakiwi kuwapokea,unafundisha mzazi pamoja na innocent children?
 
Lakini adhabu kwa mtuhumiwa haimpatii msichana fursa ya kusoma. Watu naona mna-underestimate uzito wa kauli ya kiongozi mkubwa kama rais. Kama rais anawakomesha watoto kwa kuwanyima fursa ya kusoma, wazazi wa huko kijijini ambako mfumo dume umetawala watashawishika vip kuendelea kusomesha mtoto aliyepata ujauzito shuleni?

Kwa kifupi, rais kawapa kisingizio wale wote ambao wanasomesha mabinti kishingo upande na kwa kusuasua. Lazima tukiri, japo moyoni kuwa familia nyingi (tena baba na mama) wanaona fahari sana wakizaa watoto wa kiume tu, kuliko kuzaa wa kike tu. Kwa kauli ya rais, kasumba hii ya kishamba imepata mpiga debe mkuu.
Hizi NGOS badala yakuhangaika na matangazo redioni,TV na semina hizo pesa wawafadhili hao wanafunzi wenye mimba kupata elimu katika tasisi nyingine inje ya mfumo wa shule za serikali. Watakuwa wamewasaidia zaidi kuliko wanavyo piga pesa za wafadhili
 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Wait.... Anamaanisha hata akijifungua ni no kusoma? Sijamwelewa

ametumia maneno harsh ila nachoelewa mimi ni mwanafunzi akipata ujauzito aondolewe shuleni na akishajifungua na akataka kusoma, asinyimwe nafasi.
 
Nimeona kuna watu wanajitoa uelewa, lakini ukweli wanaufahamu.

Sio vizuri kuwa na darasa lililochanganyika na wazazi. Pia ikiwa hivyo unawafundisha nini hawa wengine? Mimba ni mimba bila kujali ni kwa kudanganyana wanafunzi kwa wanafunzi, au kubakwa, kudanganywa n.k. ndio maana hata mtu mzima akifanya mapenzi na mtoto anapewa adhabu kali bila kujali amempa mimba au la.

Tutafakari, je mtoto aliyepata mimba akiwa shuleni anasaidiwaje na serikali/jamii kujiendeleza kielimu? Serikali ilianzisha Taasisi ya Elimu ya watu wazima ili kama hawa wajiendeleze na pia wanahudumiwa ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na sekondari za serikali sambamba na shule binafsi. Hali kadhalika anaruhusiwa kufanya mitihani yake kama private candidate (sekondari). Je huu ni ufumbuzi tosha?

Maoni yangu serikali ianzishe mitihani ya darasa la saba (private candidate) kwa watoto ambao hawako shuleni na hakuna shule binafsi karibu au wazazi hawana uwezo.

Hizi NGO zifanye kazi ya kuwaendeleza hawa vijana waliopata ujauzito badala ya kupambana na serikali. Ziko baadhi ya NGO na taasisi zina program hizo na zimekuwa na msaada mkubwa na inawezekana watoto wanafaidika zaidi kuliko pengine angeendelea na masomo kwani mafanikio hayapatikani kwa elimu kubwa tu.
 
Hizi NGOS badala yakuhangaika na matangazo redioni,TV na semina hizo pesa wawafadhili hao wanafunzi wenye mimba kupata elimu katika tasisi nyingine inje ya mfumo wa shule za serikali. Watakuwa wamewasaidia zaidi kuliko wanavyo piga pesa za wafadhili

Nakubaliana na wewe na hawa wanataka kiki tu.mbona ziko taasisi nyingine zinafanya hivyo kwa mafanikio.?
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.
Nina uhakika wewe huna PhD. Na ulifoji cheti. Ukiona watu wana ongea PhD za watu hivyo ujue wao hawana.
 
Yupo sahihi kbs namuunga mkono kama unajiona umezaa maana yake umechagua kuwa mama yani umeukataa uanafunzi sasa kwann upewe nafasi nyingine?

Ila private wanaruhusu kwahiyo kama umezaa fanya uende private...
 
Tangu nchi hii ipate Uhuru hatukuwahi kuruhusu watoto wa kike wenye ujauzito kurudi mashuleni kuendelea na masomo kisheria. Hivyo kama wewe una NGO yako na ulichukua hela kwa Wazungu zirudishe hazina kazi au badiri proposal ili ujenge shule ya Wazazi, kama ni kurogwa umerogwa wewe. Wanawake wako wengi wamesoma kwa mfumo huo huo na hawakuharirika. Toka hapa usije kutuharibia Taifa.
Wapuuzi hawakosekani sehemu zote.. Na sifa ya kubwa ya mpuuzi, ni kuibishia hata sheria simply kwa sababu anaemshikia akili zake ameamua hivyo..

Ni mpuuzi unaefaa kupuuzwa..
 
Nina uhakika wewe huna PhD. Na ulifoji cheti. Ukiona watu wana ongea PhD za watu hivyo ujue wao hawana.

Hehehe ni kweli sina PhD, nina Masters na inanitosha sana, sioni haja ya PhD kwenye kazi ninayofanya.
Na sijawahi foji cheti, matokeo yangu ni mazuri toka nazaliwa, sijui hata C inafananaje najua A na B tu, sio kila mtu ni kama wewe aisee.
 
Mheshimiwa ameathirika na mfume dume. Ingawa ni kweli kwamba hakuna mzazi au jamii inayopenda mtoto apate mimba shuleni, 'kumkomoa binti' kwa kumuondolea haki yake ya kusoma si sahihi-kwa maoni yangu. Kama ni adhabu basi itolewe kwa wote wawili (me & ke). Wito kwa wazazi, iwapo binti anakumbwa na tatizo hili basi wajitahidi kumpeleka shule za binafsi kuendelea na masomo. Hata jamii isaidie kama tunavyochangia harusi. Ni matumaini yangu kuwa mfumo wa elimu utaruhusu mabinti hawa kuendelea na hizo shule za binafsi, na sio kuleta shida katika kupata uhamisho nk...
 
Mzeee wa kufyatua amefyatuka

Kwani kakosea nini? Mimi naona kaelezea uhalisia. Tatizo mnadhani kutoongea/au kuwa na aibu ndio ustraabu. "Abstract is a reflection of reality".
 
Ninazungumzia wanafunzi. Baba kumbaka mwanaye ni USHETANI.
MTU Mzima kumbaka mtoto wa miaka miwili ni ufirauni. Adhabu zao zinajulikana.
Mjadala hapa ni wanafunzi wanaojitambua.
Hujasikia hao hao wanafunzi wa darasa la sita mpk form one wako waliobakwa na baba zao.... so elewa zipo mimba zilizotungwa kutokana na huo USHETANI.... hlf warudishe kodi basi za wale walisoma baada ya kujifungua... unajua kuna many powerful women ambao walipata mimba bahati mbaya na leo wako serikalini .. umnyime elimu huyu halafu unatarajia mtoto wake ndo aje asome... au aje kua mzalendo kwa taifa hili... think again
 
Rais kanena haki na kweli kwa mujibu Wa sheria na sio kwa hisia zake...big up Mr President keep it up...we pray for you
 
Back
Top Bottom