Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Hivi raisi anajua the term "second chance"? Unataka kuniambia katika maisha yake hajawahi kupewa second chance? Hii mimi nadhani busara itumike. Ujauzito sio kwamba ni mwisho wa ndoto za wasichana walio wengi wanaotaka kujiendeleza ki maisha. Wengi unakuta wanapewa mimba na walimu na watu wengine ambao wao hawapewi adhabu. Hii kwa kweli sio sawa. Kama sote tusingepewa second chance no one will be here.
Anachokataa Magu ni fungulia mbwa watu wazae at any age...uzazi nao una umri wake
 
Wazungu wenyewe wanazaa wakiwa wakubwaa na hawapatagi mimba wakiwa wadogo sn...hv kuna nchi abortion ni legal?.
 
SIO YEYE ANAYESOMESHA BALI WATANZANIA KUPITIA KODI ZAO. NILINI HAWAWATU WATAELEWA NA KUTOFAUTISHA FAMILIA NA TAIFA. YEYE ASISOMESHE WATOTO WAKE LAKINI SISI TUNATAKA WAKWETU WASOME HATAKAMA WAMEZAA...HATUTAKI UBAGUZI NA UJINGA NCHINI TUTAWAADHIBU KIVINGINE! TUMEMPATA .... WAAJABU KAMA LISSU ALIVYOSEMA DAH!!
 
Anachokataa Magu ni fungulia mbwa watu wazae at any age...uzazi nao una umri wake
Takwimu hazitofautuani kabla ya utawala wake na sasa, sasa sijui hiyo fungulia mbwa inatoka wapi? Au anahisi ile kauli yake ya "zaeni watoto wengi elimu ni bure" inamsuta.
 
Amesema hata binti yake akipata mimba kwaheri. Sasa ninin tunataka
 
Binafsi nafikiri kumpinga JPM kwenye hili ni kumwonea. Hili analosema liko kwenye Sheria ya Elimu ya 1978 na marekebisho yake mbalimbali 1995 na 2002.
Tatizo ni namna alivyolisemea lakini kisheria yuko sawa.
Kwa kawaida mtoto wa kike kupata mimba ni ushahidi kuwa amefanya ngono ambayo ni utovu mkubwa wa nidhamu katika kanuni za shule.
Kitu kinachopaswa kwa wanaharakati na wabunge ni kushinikiza sheria ibadilishwe badala ya kumlaumu JPM..
Ninakushauri ukasome sera ya elimu na mafunzo 2014, uone jinsi mkullu alivyotofautiana nayo. Sera hii iliandaliwa na wataalamu baada ya tafiti za kutosha chini usimamizi wa Wizara ya Elimu. Ilizinduliwa na Rais Kikwete mwanzoni mwa 2015.
 
[Inavo onesha we umewapa wtoto mimba shauri yako lakini miaka 30 hiyooo na huyo mtoto anaenda kulea.
Walimu hakuna kufundisha wazazi.
Siungi mtoto kupata mimba akiwa sio shuleni tu bali hata kabla ya ndoa, kuna vitu vingine vinaweza mtokea kutokana na mazingira akajipata katika hali asiyotarajia acha ulimbukeni, We huna mtoto, ungekua na mtoto usingeongea upuuzi wa namna hii, kuzaa hakumuondolei msichana akili darasani.
 
Yes. Nchi zote za magharibi.
Iangaliwe kama option walau watu wafanye safe abortion procedures mahospitalini... ni ukweli usipingika mimba zinatolewa saaanaa tena kwa njia hatarishi sana na vidispensary uchwara,usalama wa vizazi ukoje???...na tamko hili la Mkulu ndo abortions zitazidi
 
Takwimu hazitofautuani kabla ya utawala wake na sasa, sasa sijui hiyo fungulia mbwa inatoka wapi? Au anahisi ile kauli yake ya "zaeni watoto wengi elimu ni bure" inamsuta.
Sina takwimu sahihi I can't speak on that but namsupport kuwa watoto wasome kwanza mapenzi badae..
 
Una heshima gani? Heshima ni nini? Unaweza kukuta wewe ni Waziri na bonge la fisadi. Hapa unajaifanya una heshima. Kwani hao wanaoibia nchi ni kina nani kama sio nyinyi mnaofurahia victims (msichana kupata mimba akiwa shuleni ni victim)? Haki ya msichana wa nchi hii kupata elimu ni haki ya kuzaliwa - haipaswi kutegemea utashi wa Rais. JF imeshuka viwango sana jamani. Eti kuruhusu wasichana wanaopata mimba kuendelea na masomo ni kuhamasisha wasichana wapate mimba. Seriously? Na watu wenye mawazo ya hovyo kiasi hiki ndio wanazungumza mambo ya viwanda etc. Kweli tuna bahati mbaya nchi hii.
Mwambie binti yako basi azae akiwa na 12 years ehh...Utamkuza binti vipi ukihalalisha uzinzi at a very young age??hivi maadili yenu yako wapi na hata makanisani ama miskitini mnajifunza kweli mnayoambiwa???
 
Una heshima gani? Heshima ni nini? Unaweza kukuta wewe ni Waziri na bonge la fisadi. Hapa unajaifanya una heshima. Kwani hao wanaoibia nchi ni kina nani kama sio nyinyi mnaofurahia victims (msichana kupata mimba akiwa shuleni ni victim)? Haki ya msichana wa nchi hii kupata elimu ni haki ya kuzaliwa - haipaswi kutegemea utashi wa Rais. JF imeshuka viwango sana jamani. Eti kuruhusu wasichana wanaopata mimba kuendelea na masomo ni kuhamasisha wasichana wapate mimba. Seriously? Na watu wenye mawazo ya hovyo kiasi hiki ndio wanazungumza mambo ya viwanda etc. Kweli tuna bahati mbaya nchi hii.
Kaka pole sana naona mapovu matupu badala ya hoja za msingi. Wameambiwa wakipata mimba waende VETA wajifunze kushona, waende shule za private.

Nyinyi ndio wanafiki wenyewe, watu wanafukuzwa shule kwa utoro, kwa kupiga waalimu, na kwa makosa mengi tu mbona hao hawatetewi?, ina maana hawana faida kwa taifa lao?.

Hatuwezi kukubaliana na mawazo ya kuzigeuza korido za shule zikawa sawa na zile za zahanati, lazima tulinde maadili ya kitanzania. Wewe unaweza usiwe na uwezo wa kuelewa maana ya maadili lakini wapo wengi wanaonielewa.
 
Sina takwimu sahihi I can't speak on that but namsupport kuwa watoto wasome kwanza mapenzi badae..
Hakuna mtoto anaetoka nyumbani na nia ya kwenda kufanya mapenzi, wengi wanalazimishwa na watu wazima, walimu n.k. sasa mtoto innocent kama huyo unamnyimaje fursa ya kusoma.
 
Mwambie binti yako basi azae akiwa na 12 years ehh...Utamkuza binti vipi ukihalalisha uzinzi at a very young age??hivi maadili yenu yako wapi na hata makanisani ama miskitini mnajifunza kweli mnayoambiwa???
Wewe sijui unaishi dunia gani? Nani kasema wahalalishe uzinzi? Inaonekana wewe hujazaa. Subiri uzae halafu ndo uongee
 
Namuunga mkono Mheshimiwa Rais JPM katika suala hili.

Vyovyote vile mtu anaeweza kuitafsiri kauli ya Mh Rais JPM ya kupinga watoto wa kike wanao beba mimba wakiwa shuleni kuendelea na masomo kwa jinsi yoyote ile anayoiona katika kafakuri yake. Yupo anaweza kuona kwamba ni kitendo cha kuwanyima haki mabinti hao yakuendelea na masomo na kuzima matumaini yao ya badae. Mtizamo kama huo katika dunia inayotoa uhuru wa mtu kuwa na mawazo huru hauwezi kubezwa kama tuna tumia mantiki katika kufikiria mambo na maamuzi muhimu yanayofanyika katika nchi yetu.

Haijawahi kutokea katika familia mzazi ama wazazi wakafurahia kitendo cha binti yao kubeba mimba akiwa nyumbani acha hilo la kubeba mimba akiwa shuleni. Familia nyingi zimekuwa zikitisika kwa kitendo cha binti yao kubeba mimba akiwa shuleni na hata nyingine kufikia hatua ya kuvunjika kabisa. Mtoto kubeba mimba akiwa shule ni mgogoro mkubwa na waaina yake katika familia hata kama wanaharakati wa haki za binadamu wakiendelea kusimama katika upande wa utetezi.

Shule kama taasisi wajibu wake mkubwa nikuwajenga vijana ili badae waweze kuwa na mchango katika jitihada za jamii zinazo lenga kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazo dumaza ustawi wa jamii husika. Ili kuwapata vijana wakuweza kutekeleza majumu yao ipasavyo katika jamii baada ya kumaliza masomo yao nidhamu ni jambo la kwanza. Katika jamii yoyote hapa duniani kama vijana wanaandaliwa bila kuzingatia nidhamu ni wazi kwamba jamii hiyo itazilisha vijana ambao watakuwa hawana tija katika utendaji wao hapo badae.

Ni vigumu sana mwanafunzi ambae hana nidhamu shuleni kufanya vizuri katika masomo yake, ni vigumu sana kwa mwananfunzi ambae tayari anajihusisha na matendo ya mapenzi kuwa na nidhamu mbele ya walimu wake wanao mfundish. Kwa uzoefu wa kada ya ualimu na kuwa mwanafunzi kwa muda mrefu naiona nidhamu kama sifa ya kwanza nay a muhimu sana katika kufikia malengo ya elimu katika ngazi yoyote ya masomo. Ukifuatilia vizuri katika shule zetu wanao fanya vibaya ni wale ambao wana nidhamu ya shule. Ni wale ambao muda mwingi wanautumia katika kufanya mambo ambayo hayana msingi kwa manufaa yao ya badae na taifa kwa ujumla.

Jamii zetu za kiafrika kwa wakati wote zimekuwa zikitufundisha vijana masuala ya mahusiano na katika eneo hili mafundisho mengi iwe ya kijamii ama ya kidini yameweka mkazo wa vijana kuanza mahusiano ya kimapenzi baada ya kuoa ama kuolewa, hata kama mahusiano ya aina hii yanafanyika kabla ya muda huo lakini hayawezi kuwa na Baraka za jamii. Huo ndio utamaduni wetu ambao hatuwezi kuacha upotee kwasababu ya sera na mambo tunayo fundishwa na wazungu. Mila na desturi zetu ni muhimu sana zikaheshimika katika kila familia kama tunataka kuijenga nchi yetu katika misingi madhubuti na imara.

Tukisema mabinti zetu waachwe wa bebe mimba badae warudi shule waendelee na masomo ni kama tutakuwa tumewatoa kafala katika ulimwengu wa sasa ambao umegubikwa na matatizo mengi. Kama binti anafanya ngono zembe kiasi cha kubeba mimba akiwa shuleni maana yake ni kwamba katika tendo hilo ukiachilia mbali hiyo mimba upo uwezekano mkubwa wakupata maambukizi ya magonjwa hatarishi kama vile ukimwi n.k. kuwaruhusu wafanye ngono wabebe mimba na badae warudi shule kuendelea na masomo ni sawa na kutoa ruksa ya kufanya vitendo hivyo na kuhalarisha matendo hayo katika vizazi vyetu vya sasa na badae.

Namuunga mkono Mheshimiwa Rais JPM katika suala hili.
 
Back
Top Bottom