Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

"Jesca John - Mwanafunzi wa kidato cha Sita chang'ombe.

Tutathini ni nini kifanyike ili rais ajaye asiharibu kile kilichofanywa na Magufuli, tunahitajij wakina Magufuli katika Miongo mitatu. Asante "

Sijui kama hoja ya mwanafunzi huyu kuna aliyeizingatia. Ana hoja nzito. Sawa kwa wale tunaoamini kuwa tumepata 'malaika', je huyu 'malaika' akimaliza muda wake au Muumba akampenda zaidi ya sisi tunavyompenda, haya mambo yake ya kimailaka nani atayaendeleza? Je tutapata 'malaika' mwingine? Je, tunafanya maandalizi yo yote ya kuendelea kupata 'wamalaika' tuseme katika miaka 50 ijayo? Kwa maoni yangu huyu binti alikuwa anasisitiza suala la uwepo wa Katiba mpya iliyobora itakayohakikisha kila zuri lililotendwa na 'malaika' litadumishwa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Vinginevyo vitukuu vyetu kuna siku vitapiga bakora makaburi yetu! nachema tu
Hata Magufuli mwenyewe anajua Watanzania wanataka katiba mpya, lakini maneno yake yanaonesha woga wa mabadiliko kwa sababu anafaidika na ubovu wa katiba uliopo. Ndo maana kasema hata akipewa hiyo fedha na mtu ataitumia kujenga reli. Ninachoungana naye ni kutokubali watu kulundikana Dodoma kupiga soga huku wakidanganya kila mmoja yuko busy kutunga katiba wakati wengi hakuna wanachofanya zaidi ya kutumika kishabiki. Ukiangalia bunge la Katiba lililopita utashangaa baadhi wa wajumbe walikwenda kufanya nini Dodoma na kwa nini walilipwa? Mtu kama Aeshi Hilary, Ally Kessy, Kibajaji, Sugu, Makonda....!!
 
Tulipo fikia kama taifa hatuwezi kuwakwepa hawa wazungu tunadanganyana tu kila kitu tunacho tumia wametengeneza wao. Taifa kama ujeruman mkuu wao wa nchi alikuwa anarecodiwa. Sasa huku kwetu sindiyo balaa kabisa! mkuu wetu pengine wanamwona kila anacho fanya. [emoji3][emoji3]
Wazungu hawakwepeki kabisa hata tufanyeje Hali ikizidi Kuwa mbaya lazima magoti yapigwe Nyerere alibana wee akaona anaumiza wananchi akajiuzulu. Tunahtaji kushirikiana nao in positive way
 
Nampenda sana Rais Magufuli. Natamani sana iwekwe misingi thabiti ili ajaye baada ya Rais Magufuli aifuate na si kuibomoa kwa maslahi yao binafsi na makundi yao. Long live JPM
 
UDSM mnatakiwa mtuambie inakuwaje wahitimu wenu hawana viashiria vya Kisomi?
 
Kuna watu katiba zao zimeandikwa mwaka 1800 na wanapiga hatua za kimaendeleo kila kukicha.

Jenga reli uimalize megawatts ziongezeke. Jenga SGR mpaka Kigoma usafiri uwe rahisi Tangaza Tanzania watalii waje pato liongezeke.

Halafu ukishakuwa na nchi ambayo imefunguka kiuwekezaji ndipo mkae chini na kuongelea hayo mambo ya katiba.

Badala ya kufikiria namna gani dreamliner inaweza kwenda Toronto na kurudi kama Kenya walivyofanya safari ya Nairobi to New York watu wapoteze muda kwenye mjadala wa serikali mbili au tatu.

Labda viwango vya kuutambua umaskini wetu na fursa zilizopo, unatofautiana kwa kila mtanzania.
 
Hakuna hata mmoja ambaye kasemea utekwaji unaofanyw serikali. Hakuna aliyezungumzia maisha magumu.
Hakuna aliyezungumzia kuwa hakuna ajira kwa vijana

Hakuna aliuluza umuhimu wa ppp

Hakuna aliyesema kwamba serikali maana yake nini na jpm anapaswa aongoze kulingana nd definition ya serikali.

Hakuna hata mmoja aliyesema kwa nini makonda anaendelea kutawala dar wakati hana vyeti
Labda kidogo aliyejitahidi ni pd kitima aliyewasemea wanyonge kwamba purchasing powwer parity (ppp) imepungua sana japo tunadanganywa sana kuwa uchumi umekuwa.

Kwa kweli kitima ameongea kifalsafa sana. Kwanza alisema anawaongelea wasio na sauti which means hakupaswa kuongea na wale maprof mana wameshiba na wana mishahara ispokuwa alipaswa aongee na watu wa chini huku ndo wanahangaika hao maprof wataishia kumsifu tu na kutompa facts na kumjaza kichwa kuwa anapendwa wakati siyo kweli. Pili alizungumza kuwa wakuu wa mikoa hawafati sheri wakati maprof walikuwa wameshamsifu kuwa anafata sheria na haki za binadamu zinazingatiwa.

Kwa ambao tulimwelewa kitima aliwazungumzia mpaka waandishi wa habari kuwa hawana uhuru ndo maana alisema anawaongelea wasio na sauti.

Asante fr kitima we ndo kwa kweli hukuwa mnafiki na umelitendea haki jina la bwana.
 
mengi ya yaliyosemwa yalipangwa yawe vile
 
maporofesa Wa bongo ni watu wanaolilia vyeo muda wote .amenisikitisha yule prof.Wa kichaga eti anaomba kwenda ikulu kupata kikombe cha chai. mweh aibu
 
*YALIYOSEMWA NA RAIS MAGUFULI UDSM 01/11/2018*

"Nchi yetu ina akiba ya Dola Bilioni 5.4, fedha hizo zinaweza kununua bidhaa kwa kipindi cha miezi 6, hatujawahi kuwa na kiasi hicho cha fedha tangu tupate uhuru." - Rais Magufuli

"Mfumuko wa bei umeendelea kuwa imara kwa asilimia 3.4 hadi 3.6 na kutokana na hilo nchi yetu ni miongoni mwa nchi tano za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi." - Rais Magufuli

"Katika kipindi cha miaka mitatu zaidi ya viwanda vipya 3066 vimejengwa, na tukishatengeneza viwanda tayari tumeshakuza ajira." - Rais Magufuli

"Nchi yetu ni ya pili kwa kuwa na mifugo mingi Afrika lazima tujiulize na tuweze kuchukua hatua ya kutumia malighafi hizo kujitengenezea bidhaa zetu wenyewe." - Rais Magufuli

"Si vyema kwa nchi yetu ambayo ina utajiri wa kila kitu tukaendelea kuwa watengenezaji wa malighafi pekee hivyo ni lazima viwanda viwepo ili tutengeneze bidhaa wenyewe na kukuza ajira." - Rais Magufuli

"Kazi ya urais ina changamoto nyingi sana. Nimekuwa Waziri kwa miaka 20, ila hizi changamoto ni zaidi. Ukienda chumbani kwangu kuna mafaili hadi kitandani. Huwa najiuliza, wenzangu waliwezaje kuyamaliza yote? Huwa natamani niwaoneshe hayo mafaili." - Rais Magufuli

"Watoto wangu wamefunga harusi, tena wengine wamefunga nikiwa Rais, lakini hamkuwahi kusikia sherehe zao." - Rais Magufuli

"Siku mimi nimefunga ndoa, sikuvaa koti, wala mke wangu hakuvaa shela. Tulienda kanisani Chuo Kikuu (UDSM), Padri alitununulia pete, ilikuwa ya shaba, kisha akatununulia soda, nikanywa pepsi, mke wangu akanywa mirinda, mambo yakaishia hapo." - Rais Magufuli

“Dk. Bashiru alipigwa vita CCM wakasema huyu ni CUF na mimi nikasema nataka CUF wa namna hii CCM, CCM wenyewe ni kwasababu hawakutaka mabadiliko namshukuru huyu CUF wa CCM aliyetoka chuo kikuu kwa kunisaidia"-Rais Magufuli

"Demokrasia nayo ina mipaka yake sio fujo na mkishamaliza uchaguzi mahali pa mabishano ni Bungeni"-Rais Magufuli

"Hii sheria ya madini wapo walioipinga bungeni, leo nimewaambia tumekusanya Bilioni 301 hizi fedha haziendi CCM zinaenda kwenye miradi ya wananchi"-Rais Magufuli

*Shilatu E.J*
Anaogopa katiba mpya. Iliyopo ndio inampa umungumtu.
 
Wakati mchakato wa Katiba Mpya ukiwa umesimama na haijulikani utaendelea lini, Rais John Magufuli amesema hawezi kutenga fedha kuendelea na mchakato huo, ni vyema fedha hizo zikatumika katika ujenzi wa reli ya kisasa.>>>Magufuli asema hawezi kutenga fedha za mchakato wa Katiba Mpya

Kwa maana hiyo kuwa na katiba ya kuwabana wanaoitwa watawala ni upotevu wa hela ila wao kila siku kutunga sheria kuwabana raia ni sahihi kabisa. Na kurudia chaguzi za maigizo ni sahihi kabisa
Utawala bila katiba ni vurugu tupu.
 
kutegemea katiba mpya kupewa na watawala ni ndoto.katiba ya sasa hawaifuati sembuse katiba mpya?
 
Back
Top Bottom