*YALIYOSEMWA NA RAIS MAGUFULI UDSM 01/11/2018*
"Nchi yetu ina akiba ya Dola Bilioni 5.4, fedha hizo zinaweza kununua bidhaa kwa kipindi cha miezi 6, hatujawahi kuwa na kiasi hicho cha fedha tangu tupate uhuru." - Rais Magufuli
"Mfumuko wa bei umeendelea kuwa imara kwa asilimia 3.4 hadi 3.6 na kutokana na hilo nchi yetu ni miongoni mwa nchi tano za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi." - Rais Magufuli
"Katika kipindi cha miaka mitatu zaidi ya viwanda vipya 3066 vimejengwa, na tukishatengeneza viwanda tayari tumeshakuza ajira." - Rais Magufuli
"Nchi yetu ni ya pili kwa kuwa na mifugo mingi Afrika lazima tujiulize na tuweze kuchukua hatua ya kutumia malighafi hizo kujitengenezea bidhaa zetu wenyewe." - Rais Magufuli
"Si vyema kwa nchi yetu ambayo ina utajiri wa kila kitu tukaendelea kuwa watengenezaji wa malighafi pekee hivyo ni lazima viwanda viwepo ili tutengeneze bidhaa wenyewe na kukuza ajira." - Rais Magufuli
"Kazi ya urais ina changamoto nyingi sana. Nimekuwa Waziri kwa miaka 20, ila hizi changamoto ni zaidi. Ukienda chumbani kwangu kuna mafaili hadi kitandani. Huwa najiuliza, wenzangu waliwezaje kuyamaliza yote? Huwa natamani niwaoneshe hayo mafaili." - Rais Magufuli
"Watoto wangu wamefunga harusi, tena wengine wamefunga nikiwa Rais, lakini hamkuwahi kusikia sherehe zao." - Rais Magufuli
"Siku mimi nimefunga ndoa, sikuvaa koti, wala mke wangu hakuvaa shela. Tulienda kanisani Chuo Kikuu (UDSM), Padri alitununulia pete, ilikuwa ya shaba, kisha akatununulia soda, nikanywa pepsi, mke wangu akanywa mirinda, mambo yakaishia hapo." - Rais Magufuli
“Dk. Bashiru alipigwa vita CCM wakasema huyu ni CUF na mimi nikasema nataka CUF wa namna hii CCM, CCM wenyewe ni kwasababu hawakutaka mabadiliko namshukuru huyu CUF wa CCM aliyetoka chuo kikuu kwa kunisaidia"-Rais Magufuli
"Demokrasia nayo ina mipaka yake sio fujo na mkishamaliza uchaguzi mahali pa mabishano ni Bungeni"-Rais Magufuli
"Hii sheria ya madini wapo walioipinga bungeni, leo nimewaambia tumekusanya Bilioni 301 hizi fedha haziendi CCM zinaenda kwenye miradi ya wananchi"-Rais Magufuli
*Shilatu E.J*