Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Mimi nafikiri kinachotakiwa ni kubadili vipengele vichache tu, tume huru ya uchaguzi, kuingozea nguvu mihimili ya mahakama na bunge, kuruhusu mgombea binafsi na uraia pacha. Hayo mambo mengine kwenye hiyo katiba ata yakibaki constant hakuna kitakacho haribika
 
Katiba mpya ni kitanzi,wakisha kuwa nje ya system ndo huwa na akili.Ujua umuhimu wake baada ya kutoka
 
Ehhh Mh kashasema anafahamu kama watu wanaitaji Katiba Mpya ila Kwasasa Ngoja ajenge SGR, Umeme kule Rufiji..!
Kwasasa tuchape kazi kwanza..!
Watu wanazungumza utafikili hiyo Katiba ndio suruhisho la kila kitu!!!
 
Kutembea, kuandika uko chuoni au kuongoza vikao kwa kusoma nyaraka zilizoandikwa na kuongea ni vitu viwili tofauti.

Ivi rais wa Kenya Uhuru Kenyata tutasema kweli anajuwa kuongea kiswahili kwamfano - watu wingi = watu mingi, kaja mtu = ukuja mutu nk.
 
Kuna watu Wenye ewezo wa kujitolea, sasa kama kigezo ni fedha, basi Wadau wote ianze kampeni ya kuchangia na nitachangia, mbona zitatimia na kubaki chenji tena ndani ya wiki moja tu na nina uhakika.

Ila tahadhari, mchango usipite serikalini maana si mnajua mzee wa kukwapua kwapua, hii tunaita weka mbali na ********.
 
No 3.wacha colonial mentality.ficha uchi wako.unadharau kiswahili na kutukuza kiingereza?maendeleo hayaletwi kwa kuzungumza kiiingereza.

mdanganyika wa ukweli,
Si ajabu wahenga walisema mficha uchi hazai. Tatizo ni uelewa wako. Mimi sijadharau Kiswahili.maana ni Lugha yangu ya Taifa/Mama. Ninachosema kulazmisha Kiswahili kiwe ndo mworabaini wa Uchumi wa Tanzania hakika ni kujidanganya. Tumeongea Kiswahili miaka yote tangu tupate Uhuru umekusaidi nini wewe mdanganyika? Darasa la Kwanza mpaka la 7 unasoma kwa Kiswahili ukifika Secondari unaanza Kiingereza, matokeo yake jitu linanaza kukarairi siyo kuelewa maana Kiingereza hakipandi,

Matokeo yake hakuna Mwanasayansi yeyote KItanzania atakuja kuingia kwenye Vitabu vya Ugunduzi wa chochote kiwe cha Kisayansi au Kiteknolojia.Ndo maana Maprofedha wetu wanaongea kama makasuku tu lakini kichwani hakuna lolote...!! Nenda hapo Kenya uone Waafrika wenzetu walivyo mbele ya Tanzania katika kila kitu...!

Kama kuna watu wanajidanganya ati Kiswahili kitaleta maendeleo au kuinua Uchumi wa nchi wanapoteza muda wao bure. Kumbuka hata nchi mabazo haziongei Kiingereza kama China, India, Urusi, Ujerumani zimeendelea kwasababu zina ELIMU IMARA, TEKNOLOJIA KUBWA na Uchumi IMARA. Je,Tanzania una Teknolojia gani ya kuwauzia huko Ughaibuni? Chukulia mfano mdogo wa madini.....Mungu ametupa Raslimali za asili lakini tunashindwa kuzitumia ili kuwa na Uchumi imara kwasababu elimu tunayopata ni ya kukariri tu,
 
JK alikua ni muungwana sana ila alikosea aliposhindwa kujipanga na kuweza kuacha katiba mpya.

Sitegemei watawala wanaoishi maisha ya kifalme na kimiungu wawaze suala la katiba.
Suala la katiba Mara nyingi linaanzia kwa wananchi.

Pesa zinazotumika ni Mali ya umma sio pesa toka kwenye mshahara wa mtu . Kwa hiyo ni wananchi tu bado hawajajua umuhimu wa katiba mpya.
JK alitumia mbinu aliyotumia Mwalimu wakati wa kuanzisha mfumo wa vyama vingi, alianzisha katiba mpya kabla wananchi hawajawa na mwamko mkubwa wa kuidai.

Hata hivyo bado waafrika tuna bahati Mbaya sana ; ukiangalia fedha zilizotumika kwenye chaguzi za marudio za makusudi ya watu binafsi kuanzi wabunge na madiwani unaona kuwa zingeweza kutumika kwenye katiba Mpya na kuweka misingi imara ya Taifa badala ya misingi ya maslahi binafsi huku taifa likisambaratika vipande vipande kutokana na nchi kuendeshwa na mtu mmoja na jamaa zake wa karibu. Wengine kuitwa maadui wasiofaa .

Afrika bado tuna safari ndefu sana hata kwenye mambo yasiyohitaji Teknolojia yoyote bado tunashindwa kujua kesho njema ya nchi zetu ni ipi!!
 
Rais Magufuli ametoa msimamo wake kuwa kwa sasa hana mpango wowote wa kuendeleza mchakato wa katiba mpya, na yeye atatumia zaidi rasilimali za nchi kuboresha mambo ya muhimu na yenye mchango kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla, ... Unaweza kumsikiliza hapo chini

huyu jamaa hatabiriki,kwa ninavyomfaham usishangae katiba mpya ikija kupatika ndani ya utawala wake,kuna possibility kubwa katiba mpya ikawa ndyo sera yake kwny kampeni za uchaguzi ujao,mm ninaiman huyu namhala atatuachia katiba mpya,ni jambo la muda tuu
 
Shida sio elimu ni itikadi za chama ccm wanafata itikadi za ujamaa na Ukisema ujamaa tafsiri yake ni umasikini. Ujamaa uendana na udikteta

Back
Top Bottom