Unajua tatizo ni kutokujua uelekeo wa dunia kwa sababu ya elimu mbovu (failures ndiyo wanapewa madaraka), kutokujisomea vitabu na kukosa exposure. Ushamba ni mzigo.
Hayupo vizuri hata kidogo na suluhisho lake ni la hovyo.
Labor intensive industries ni mambo ya karne ya 18 na 19 wakati industrial revolution inaanza. Katika karne ya 21 automation ndiyo mwendo wa viwanda vya sasa. Hivyo anachosema tuwekeze kwenye labor intensive industries haelewi muelekeo wa dunia. Huwezi kumlaumu kwa sababu hana elimu nzuri, hasomi vitabu na kaanza kusafiri ukubwani. Unapoona watu wanamshangilia unajua tatizo la ujinga ni kubwa zaidi.
Pili, labour intensive industries asilimia kubwa unaongelea cheap and unskilled labour. Hiyo haihitaji wahitimu wa chuo. Tatizo la ajira la sasa ni kubwa kwamba kuna wahitimu hawana kazi.
Hili ni onyesho la ujinga. Mawazo ya kijima na watu wasioelewa dunia inaenda wapi lakini kwa sababu wamevaa "uprofessa" na "madaraka" wanapata sauti ya kusikika.