Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Kongamano linaanza leo tarehe 01/11/2018 kuanzia saa 3:00 asubuhi hii.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ni Mshiriki Maalum kwenye Kongamano hilo. Watoa Mada ni Wanazuoni wabobezi katika masuala ya Uchumi, Siasa ya Uchumi,Siasa ya Jamii, Sheria n.k

Nitawaletea kila linalojiri kupitia Mada hii. Unaweza pia kufuatilia moja kwa moja kupitia Runinga ya TBC1


======

UPDATES

Kongamano UDSM: Hali ya Uchumi na Siasa nchini Tanzania 2018

- Kanuni 3 zitazingatiwa ktk mjadala: Uwazi na Uhuru, heshima na staha, kuzingatia muda

- Rais Magufuli hatazuiliwa kuongea hata akizidisha muda

Prof. Humphrey Moshi: Nitazungumzia “Umuhimu wa Viwanda ktk Uchumi wa Nchi hii”

- Kwa miaka 15 Uchumi wa TZ ulikuwa ukikua kwa 6-7% lakini haukuwa Uchumi Shirikishi

Prof. Moshi: Sekta ya Madini haikuweza kupunguza kasi ya umasikini na ajira

- Bado mfumo wetu wa uchumi haukuwa umebadilika; hakukuwa na mfumo mbadala

Prof. Moshi: Ukitaka kupunguza umasikini kwa haraka na kufikia uchumi, viwanda ni lazima

> Viwanda ni sekta vuguvugu, ni kiwanda cha uvumbuzi. Hakuna sekta yoyote katika taifa lolote iliyo na mahusiano na uchumi kama viwanda

Prof. Moshi: Kwa nchi za Afrika hasa Tanzania viwanda ni sekta kombozi, kwahiyo kwa Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kitu sahihi kinachopaswa kufanyika

> Wakati wa Mwalimu, tulikuwa na viwanda vya kila aina na viwanda vinazalisha ajira zenye hadhi

Prof. Moshi: Kulikuwa na mpango wa SAPs lakini baadaye tukaja kuwa na ubinafsishaji ambao ulifyekelea mbali viwanda

> Wafadhili wanatoa mapendekezo yao ambayo hayaendani na mipango ya Taifa
> Wakati huo kulikuwa na viwanda vya umma lakini hakukuwa na wataalamu, sasa wapo

Prof. Moshi: Miaka ya nyuma hatukuwa na uwezo wa kununua katika masoko ya kimataifa

> Kulikuwa na uwekezaji katika tafiti za mipango na hakukuwa na utekelezaji, watu wa nje wanakuja kuchukua mipango Tanzania na kwenda kuitekeleza

Prof. Moshi: Serikali ni lazima ikae mbele wakati wa kuendeleza viwanda, tulikaa miaka 25 tukisubiri sekta binafsi ituletee umeme

> Tulikaa miaka mingi tukisubiri sekta binafsi ituletee kilimo cha miwa. Miradi mikubwa ya Marekani inamilikiwa na serikali

Prof. Moshi: Elimu, miundombinu na viwanda lazima viende pamoja. Tuboreshe uhusiano na nchi za Asia

> China wakati wanajenga SGR walikuwa wana kipato cha 1/3 ya Watanzania lkn sasa ni zaidi ya mara 10
> Tuimarishe mahusiano na nchi hizo, tupunguze utegemezi kwa nchi za Magharibi

Prof. Hudson Nkotagu anasema:

Pro. Nkotagu: Nitazungumzia Nishati na Miundombinu katika kuendeleza uchumi wa viwanda

> Vyanzo vya nishati ni vingi vikiwemo vanzo 'jadidifu na vile visivyo jadidifu'

#KongamanoUDSM

Pro. Nkotagu: Chanzo jadidifu kama Mto Rufiji kufikia 2020-2025 kitakuwa kinachangia asilimia 21 ya nishati ya umeme nchini

> Yako maeneo yenye dalili za kuwa na mtiririko wa mafuta. Serikali imejipanga kuzalisha Mewati 5,000 na kufikia 2020-2025 kupitia Stieglers Gorge itafikia Megawati 10,000
Ili Serikali imeweza kutekeleza miundo mbinu wezeshi ikiwemo Reli, barabara ya kuunganisha mikoa na nchi za jirani. Barabara za vijijini. Usafiri wa anga na Majini vimeboreshwa. Ndege zimenunuliwa karibu 9. Kuimalisha usafiri wa angIa. Meli zinatengenezwa na nyingine zinakarabatiwa. Hiyo ni miundombinu wezeshi ya kuinua uchumi

Kuna changamoto

Wataalamu ni wachahce sana. tunatakiwa tuwe na injinia 1 kwa mafundi watano na wafundi michundo 25. Tnatakiwa tuwe na Injinia 10 Mafundi 50 na fundi michundo 250,hiyo ni ya kitaifa.

Tuhakikishe nishati zetu hazipotei, mfano taazinawaka na jua linawaka

Stiegler's Gorge

Faida ya Huu Mradi wa Stiegler's Gorge

tutatumia asilimia 3 tu ya eneo lile.

Itapunguza ukataji miti

Hii nishati ni endelevu sababu haihitaji wabia.

Itavutia wawekezaji

Itaongeza ukuaji wa miji

Mapendekezo

Napendekeza Serikali iweze kuendekeza vyanzo mbalimbali vya nishati, Kuongeza Wataalam, Kuongeza Tafiti na kuwawezesha watafiti na kuelimisha raia.

Prof. Martha Qorro anasema;

Fursa ya lugha na Maendeleo

Katika mada hii ntazungumzia mchango wa lugha ya kiswahili katika kuleta maendeleo, Mawasiliano na maendeleo,Tafiti zilizofanyika na changamoto katika ufundishaji wa lugha

Lugha ni chombo au nyenzo kuu ya mawasiliano. Na kwa nafasi hiyo lugha huwa inamuwezesha mwanadamu kufikiri, kuchambua kupanga kuamua na kutekeleza kwa pamoja kuboresha maisha.

Mawasiliano na maendeleo

Lazima lugha iwe inaeleweka kwa pande mbili. Msemaji na msikilizaji. Yasipokamilika, lugha haiwezi kuleta maendeleo.Bila kusikilizana hakuna maendeleo

Kuna Elimu, Maendeleo na lugha. [Mawasiliano ya maendeleo]

Uhusiano wa Elimu na Lugha wengi hawaufahamu

Tafiti zilizofanywa africa zinasema moja ya sababu ya kutokuwa na maendleo africa ni kwamba mipango ya maendeleo yanafanyika kanika lugha za kigeni ambazo ni kileno, kingeleza Kifaransa wengine kiarabu. Ili kuapata maendeleo lazima tuingize lugha za jamii kwenye maendeleo.

Tanzania tunakabiliwa na changamoto za elimu katika kufundisha lugha. Mtoto anaanza na lugha ya Nyumbani shule msingi anafundishwa kiswahili na sekondari anafundishwa kingeleza. Tunajenga misingi tofauti za Lugha.

Tafiti zinasema ili mtoto aweze kujifunza lugha ya kigeni anatakiwa awe vizuri katika lugha mama. Mtoto anakosa msingi wa llugha yoyote

Unapowakataza watoto kuzungumza lugha za jamii inamaana unamwambia mtoto hizi lugha hazina maana kwa lugha nyingine hizi ni dhalau

Katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 1969 hadi 1974 ulisema

Tuna msingi wa lugha za kiswahili na kingeleza, litasbabisha matabaka na elimu ya Sekondari haitakuwa na maana kwa jamii.

Kutumia lugha mbili unatenga wasomi na Jamii.

Miaka mitatu ya awamu ya tano

Wanaona fahari kuzungumza kiswahili hata rais wetu. Tunaposhiriki lugha moja na viongozi tunajiona tupo pamoja na viongozi

Hii ya elimu pasipo ada imeongeza fursa ya kuzungumza kiswahili.

Nini kifanyike?

Mfumo wa elimu wa sasa duniani, unafaa kuzungumza lugha za kigeni nyingi tofauti na kingeleza tu. tufundishe lugha zaidi na moja

Kiswahili kitumike katika ngazi zote za elimu, hii itaunganisha jamii

Baba wa taifa alisema Wasomi ni watu waliotumwa. Nchi nyingine wakienda kusoma wanarudi kwenye jamii kuwatafsiria kile walichokisoma. Hivyo kila mtu aludishe kwa jamii kile walichokisoma kwa kiswahili. kuna tafiti nyingi sana ili zimefungiwa katika ngome za lugha na wenye ufunguo ni wasomi.

Tunahitaji kukipeleka kiswahili nchi za nje kwenye balozi zetu. Mabalozi wafundishe kiswahli. Google wanasema Kiswahili Kenya, kwanini sio Kiswahili Tanzania? Tunarudi nyuma kwa kukataa vitu vyetu.

Profesa Kitila Mkumbo anasema:

Atazungumzia Huduma za Jamii.

Ataongelea

1, Ni muhimu tujue tumetoka wapi. Mwalimu Nyerere alipigania uhuru, huduma za jamii zilikidhi wakati huo

2, Mwinyi alingoza mageuzi ya kisiasa na kiuchumi

3, Mkapa alijenga taasisi Imara za

4. Kikwete alijitahidi kulinda mafanikio yaliyopatikana kipindi cha mkapa

Sisi tulioingia awamu ya tano tumekuta Uchumi unaokuwa, Ujenzi wa Miundo mbinu nk.

Changamoto ilikuwa inakuwa bila kupunguza umasikini, Kulikuwepo kulegalega kwa uwajibishaji. Awamu ya nne ubora wa huduma za jamii tuliyumba.

Mpango wa pili wa maendeleo

Bajeti yake ni Til 129 huduma za jamii, Afya elimu na maji. Maji pekee til 10.4

Mkazo wa awamu hii ni nini? Rais alipohutubia bungeni alisemawananchi wamechokana wana Chuki dhidi ya ufisadi pamoja rushwa, mimi nmeahidi wananchi kwamba ntapambana na rushwa na ufisadi bila haya yoyote

Serikali hii imefanikiwa kulinda uchumi wa awamu iliyopita

Serikali imedhamilia kusimika weredi katika nyanja mbalimbali katika Siasa, ajira, utumishi nk

Serikali imedhamilia Kujenga uwajibikaji katika utumishi wa Umma

Serikali imedhamilia Kupambana na rushwa. Mfano saga la IPTL. Lipo kipindi kirefu kwa miaka 25.

Elimu bure imekuwa mkombozi sana. Hili liliwahi kutajwa lakini ndani ya Serikalini walikuwa wanakataa, awamu ya tanno imewezekana.

Maji​
1 Maji imechukuliwa kama ni sekta mtambuka ambayo ndio kiini cha uchumi. Inatakiwa tulinde rasilimali za maji. Kama kila mtu ukimgawia maji, kila mtu anaweza kupata Mapipa 9000.

Kila awamu imejitahidi kupiga hatua katika usamabazaji wa maji hadi 50% ndani ya kipindi cha mikata mitatu tumeongeza asilimia 6. Upande wa uwekezaji miradi ya maji ilikuwa til2, kwa miaka mitatu tumeongeza til 2 nyingine japo zinahitajika til 8.

Tnahitaji kuchangisha kununisha Mfuko wa maji

NIni kimefanya tufanikiwe?

Ujasili wa kufanya maamuzi makubwa

Uwezo wa kufanya maamuzi sahihi bila halama za kisiasa za muda mfupi

Ana uwezo wa kufuatilia utekelezaji

Ujasili wa kuwawajibisha wasaidizi wake bila woga wala upendeleo

Na ameweza kupambana na Ruswa

Tunakoelekea tunatalinda mafanikio ambayo tumeyapata

Tuna mpango wa kutumia maji ya ziwa Victoria, nyasa kupeleka maji kwenye maeneo yenye ukame wa kudumu.

Katika kipindi cha miaka mitatu rais amefanikiwa kuvuruga na kutibua mtandao wa watu wajanja wajanja.

Msingi wa yote haya ni Uongozi, ujasiliwa kufanya mageuzi makubwa ya kisiasa, kiuchumi nk

Ili tufanikiwe tunatakiwa tuwe utulivu na kisiasa na Utawala wa Sheria

Profesa Rwekaza Mukandala

Anazungumzia Hali ya Siasa na Utawala

Nabaini mambo matatu

Mtanziko wa wanasiasa

Siasa ni mchezo mgumu wa mikakati ya wanasiasa

Malengo ya mwanasiasa ni

Kuapata madaraka na kudumu ofisini

kutawala nkuongoza kwa mafanikio

kujenga chama chenye utiifu kwake

Tathimini ya kupima utendaji wa rais ni Mgumu

Wapo wanaoshabikia Maendeleo[ Quantity na quality]

Kuna vigezo vingine havionekani mfano watu wanavyojisikia, watu wanafurahi, wana morali,watu wameridhika nk

Kundi la tatu ni wale wanaoichukulia nchi kwa ujumla wake. je kuna amani? Kuna maendeleo

Mchakato tunapima bidii au juhudi sio matokeo

Nyerere hajatoa umasikini lakini tunampenda.

Ukitaka kupima vita ya rushwa unaangalia dhamira na juhidi japo rushwa haijaisha

Kigezo kingine unaangalia uwezo. Majeshi yanaangalia uwezo. Wanaweza kuwa na vifaa vita ikija watu wanaingia mitni

Swali la kwanza

Je kumekuwa na uelewa na ulimwengu na changamto zake?

kumekuwa na uchbmuzi na uelewa katika nchi yetu?

Ameweza kuongoza kuwa msitaliwa mbele kwa vitendo?

Ameweza kubuni lugha ya kufanya watu wamfuate?

Ameweza kujenga chaa kinachomuunga mkonno?

Utawala umezingatiwa?

Tulikotoka uelewa wa Ulimwengu na mifumo yake ulieleweka sana mfano wa wakoroni na mabeberu.

Magufuli hajaandika machapisho juu ya misimamo yake. Ila misimamo yake ni kama ya Mwalimu

Kuhusu uelewa wa nchi. Mwalimu aliongozwa na azimio la Arusha, Magufuli ana uelewa mzuri wa changamoto za nchi.

Rais ndio kiongozi na mwanasiasa wa nchi, anatakiwa kuwa mfano. ufuasi hauhitaji nguvu bali hiari. anafanya kazi sio hadi waziri, haendi nje, hospitali anatumia za ndani. amejirundikia mtaji wa jamii. amekuwa mwepesi wa kutenda na kuchukua hatua. ameweza kubuni msamiati. Mwalimu alikeea kupe Magufuli anakemea kajipu.

Kuna aina mbili za Viongozi, Viongozi mageuzi na viongozi nipe nikupe/Wapiga dili. Mwalimu na nyerer ni Viongozi Mageuzi

Kukisafisha na kukinyosha chama ni kazi kubwa sana, Mwalimu alianzisha vyama vingi. Kazi ya kukisafisha na kukinyosha chama ndio imeanza. Viongozi na wanachama wanahitajika ili kumuunga mkono rais.

Kuna tatizo kukosekana kwa itikadi yenye mvuto katika chama.

Dola na taasisi zake ni muhimu sana. Swala la muundo ni muhimu. Benki ya dunia ilizoofisha dola. Serikali ya awamu ya tano inaonekana kupendele Serikali kuu.Mishahara inalipwa kwa wakati, Serikali inahamia dodoma,Wafanyakazi hewa wameodnolewa, uzembe vinakemewa, Ufuatiliaji wa miradi unafanywa, kodi inakusanywa. Miradi midogo na mikubwa inajengwa. Mifuko ya jamii imeungamishwa

Mchakato wa katiba utakapolejewa kuna umuhimu wa kurejewa upya kwa rasimu ya katiba mpya sababu miaka minne imeshapita.

Mahakama ya kupambana rushwa imeundwa, mahakimu wameongezeka. Uamuzi wa kujipima kwa kila jaji unatekelezwa. Ofisi DPP imerekebishwa. Kubambwa na kuwekwa ndani kiholela inaendelea kupungua, kamisheni ya kupiga ita madawa kulevya imepewa meno zaidi.

Uwezo wa Polisi kiutendaji bado mdogo hata Magereza nao hivyo hivyo. Bado kuna changamoto ya kupata haki. Hakuna uhakika wa kupata haki. Rushwa na ufisadi bado adui kwani vimeenea katika vyombo. Takukuru inatakiwa kuongeza juhudi.

Bunge limeendelea kutimiza wajibu wake na kuboresha utendaji.

Swala la Zanzibar zilijitokesha tofauti 2015 na CUF walijiondoa kwenye uchaguzi. CUF wameendelea kutafuta haki kwa njia za amani na kisiasa.Serikali imeendelea kudumisha amani Zanzibar

Tathimini ya miaka mitatu ya Magufuli ni ngumu sababu hapakuwa na vigezo vya kutumia.

SASA HIVI KINACHOENDELEA NI MAJADILIANO

Watu watauliza maswali na kujibiwa.

Yeremia anatoa Ushauri

Anasema Serikali itoe fursa kwa vijana wa kitanzania kupata ujuze, kama wanavyotoa elimu bure

Padre Kitima wa Baraza la Maaskofu anasema

Kuna tatizo kwenye tume ya Uchaguzi naomba iongelewe

Kuna tatizo kwa watendaji wa chini wananyanyasa wananchi mfano Wakuu wa Wilaya

Uchumi umekuwa lakini kwa wananchi haionekani. Sekta binafsi ijengwe ambayo itasaidiana na Serikali. asanteni


Frank nasema

Rais kama itakupendeza tuandalie sisi vijana chombo cha kutuwezesha sisi vijana kukabiliana na ajira kwa vijana. Kituunganishe vijana na Serikali

Prof. Agness

Kilimo ni kichocheo cha Viwanda na biashara, Nchi zilizofanikiwa zimewekeza sana kwenye tafiti za kilimo hadi 10% lakini Tanzania tunachechemea kwa 1% kwenye utafiti.

Wale wenye dhamana waangalie kwa karibu kilimo kisaidiwe kwa namna gani

Mchango wangu wa pili, 52% kwenye nchi hii ni vijana tuwaangalie kwa karibu. Tnajitahidi kuwaweka kwenye mstali kielimu kiroho na Kimwili.Ila sasa hivi kuna vitu vya ajabu vimezuka sana kama Kucheza kamali. Tunajenga taifa la ajabu. Kiimani ni kosa. Marekani ukitaka kuchez akamali unaenda Las Vegas. Watoto hawawezi kutengenezea maua lakini anajua kucheza kamali. Hali iliyopo ni hatari.

Jesca John mwanafunzi wa kidato cha Sita chang'ombe.

Tutathini ni nini kifanyike ili rais ajaye asiharibu kile kilichofanywa na Magufuli, tunahitajij wakina Magufuli katika Miongo mitatu. Asante

Tumaini Boniface anasema

Natoa mapendekezo katika mada ya uchumi ni nishati. Sijasikia jinsi ya kuwasaidia wagunduzi wetu na wanasayansi wa hapa Tanzania. Kama serikali ikiwaangalia hawa na kuwainua, Tanzania itafika mbali sana.

Prof. Shivji anasema;

Hatuwezi kuendelea kwenye uchumintegemezi, hatuwezi kuendelea bila sekta binafsi

Tulikuwa na sera na maelekezo ya kujenga viwanda awamu ya kwanza.

Kwakuwa tumekuwa na uzoefu, jambo muhimu ni kujifunza kutoka awamu ya kwanza. Tulikosea wapi?

Mwalimu aliorodhesha makosa

1.sekta ya viwanda ilikuwa tegemezi kuanzia mali ghafi, vipuli na mashine

2. Sekta ya Viwanda na Kilimo havikuingiliana, kila moja ilikiwa huria.

3.menejimenti ilikuwa dhaifu na ubadhilifu wa mali ya Umma

Swala la Viwanda sio idadi ya Viwanda bali ni swala ambalo lazima inaendana na kujenga uchumi wa kitaifa.

Hatukuwa na mipango kamili ya kushirikisha wafanyakazonkatika mipango.

Tunifinze kutokana na hayo

Sisi hatuwezi kufuata njia ya Magharibinkufikia Viwanda. Sisi inabidi tujikite kwenye kilimo kupitia wakulima wadogo. Wanaweza kulima kilimo chemye tija.

Nampongeza rais Magufuli kwa jambo moja tu la tukio la leo la kukaa na sisi na kusikiliza maoni ya wanazuoni wake.

Prof. Kabudi anasema

Mwalimu mzuri ni yule anayotumia elimu na maarifa aliyoyapata shuleni katika kuongoza. Rais Magufuli amesoma hapa mambo ya Chemistry lakini somo la Development studies analitendea haki.

Malengo makuu ya kiuchumi ya awamu ya tano.

Maadili, vita ya ufisadi rushwa nk

2. Kuimarika kwa uchumi kwenye madini, uchukuzi, mawasiliano, kilimo, kuongezeka kwa mapato ya kodi na yasiyo ya Kodi.

Tunajenga Miradi ya umeme, barabara. Mradi wa umeme utatekelezwa, wapende wasipende utatekelezwa.

Ujenzi wa reli ya kati SGR unaendelea vizuri. Reli ya hatutaing'oa, zitaendelea kusaidoana.

Kufufua shirika la ndege la Tanzania. Ndege zimenunuliwa, zipo zilizofika na nyingine zinakuja.

Bomba la mafuta gafi kutoka Ohima hadi Tanga. Bandari ya Tanga itakua.

Kuboresha Viwanja vya ndege na Magati ya bandari, upanuzi wa bandari ya Tanga na Mtwara.

Ujenzi na ukarabati wa Hospitali 10 za Wilaya. Nyumba 306 za watumishi wa afya zimekamilika.

Tumeondoa ada kwenye elimu sasa wanafunzi wameongezeka. Mikopo ya elimu ya juu imeongezeka.

Huduma za maji zimeongezeka.

Rais Magufuli anasimmia mali zetu na raslimali.

Prof. Kabudi: Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara amerudi ndani ya CCM sio kwasababu ya rushwa bali ameguswa na mambo yanavyoendelea

Tufanye kazi tathmini zitakuja kuanzia mwakani kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020

Rais Magufuli anasema;

Leo sikutegemea kuzungumza. Nlipanga kuja kusikiliza tu na kijinoti changu. Nmeandika yote.

Chuo kikuu nakipenda, nimesoma na kukaa hapa. Nlifungia ndoa hapa. Mimi sikuvaa koti wala mke wangu hakuvaa shela lakini tulifunga noda kwenye kanisa la chuo kikuu. Pete alitununulie padre na soda. Mi nlikunywa Pepsi na mwenzangu Milinda.

Sio kwamba sikuwa na uwezo bali huo ni utaratibu. Watoto wangu watoto wamefunga ndoa na wengine nikiwa rais, haujawahi kusikia sherehe hizo.

Wote waliochangia mada wamezungumza kutoka moyoni. Yote yaliyozungumza tutayafanyia kazi.

Niseme kw auwazi kwamba uongozi ni kazi ngumu. Sikutegemea kwenye uongozi nipate kazi ngumu hivi.

Nlikiwa Waziri miaka 20,nlikiwa naona changamoto lakini si kama za rais. Chumbani kwangu ukiingia kina mafile hadi kitandani. Na kila file lina umuhimu huwezi kulipeleka kwa mtu mwingine. Saa nyingine inahitaji maombi maalum ili uweze kutenda haki.

Ni ukweli pia kwamba nchi yetu imepitia katika hatua mbalimbali. Ilikuwa imefika hatua ya hovyo katika maswala ya rushwa na ufisadi..

Ndugu zangu nafahamu yapo mambo tumeanza kuyafanya. Katika hali ya uchumi tunakiwa kwa asilimia 7, tunataka ukue zaidi ya hapo. Mfumko wa bei umeendelea kua 3. Nchi yetu ni miongoni mwa nchi tano ambauo uchumi wake unakuwa kwa kasi.

Viwanda 3066 vipya vimejengwa
Ni shivji tu ndio ameongea la maana, wengine wachumia tumbo tu hapo. Hatutatoka hapa tulipo Kama tunaukalia ukweli na kusifia sifia tu.
Mafanikio ktk number tu, sio quality. Madarasa xxx, viwanda yyyy, barabara zzzz.
Ndio tunasogea, this is positive, lakini tusogee strategically, tuwe na watendaji wanaoweza kuanzisha mambo, sio kusubiri mkuu anataka nini, Ooh, ktk kutekeleza maagizo ya rais,hii ni sentensi ambayo Hakuna kiongozi au mtendaji haitumii, Hii sentensi inaanza kukera Sasa, Kwa hiyo asipotoa maagizo ndio basi Tena.
Tujitafakari kama nchi, nchi haiwezi kuendeshwa kwa kutegemea maagizo ya Rais.
 
Hili la kuongeza bajeti kwenye development project ni jema sana maana litaspeed up maendeleo kwa haraka maana fedha nyingi kutumika kwenye maeneo ambayo hayana returns wala siyo kichocheo cha maendeleo ilikuwa wasteful of resources
 

Sasa hutaki au? Wana Kagera ( Bukoba ) wenyewe wanatambua kuwa Makao Makuu ya Elimu na Wasomi ipo Mkoani Mara na kwa wana Mara ( Musoma ) kama uko nao hapo jirani waulize watakupa majibu.

Watani zangu Wahaya mpo?
Watakuja kina ;Rutashobya ,Enjai ya kyasha, na msubili, Brtanica
 
huyu bwana aachane na kusema awamu zilizo pita na kuonesha kwamba hazikufanya kazi.

awamu yake hii ina makando kando kibao,anatumia nguvu kuyaficha yasihojiwe aachie uhuru kama j.k aone atakavyo anikwa.

kazi anafanya ila sio kiivo, kawaida sana
 
Ila Ukiitafakari serikali yetu unabaki ukishangaa.
Yani Bunge lenye mikutano ya wawakilishi wetu tuliowachagua na kuwatuma wapeleke hoja zeto limezuiliwa kutangazwa na kuonyeshwa Live lakini makongamano ya watu binafsi na hoja zao za kujipendekeza yanaonyeshwa Live.

Hii serikali ya CCM ina bahati sana watanzania wengi sana bado ni wajinga 2020 hakuna Mbunge wa CCM angepata kura mana tumewachagua ili watuwakilishe na kututungia sheria bora badala yake wanajipambanua kama sehemu ya serikali na kuitetea serikali na maslahi yake badala ya maslahi ya wapiga kura.
 
Kabudi ni mjinga sanaa.Hivi hawa maprof.wetu wanamatatizo makubwa sana.Aiseee inasikitisha sana.

Ukijalibu kuona hata hata hajaribu kutoa mapendekezo ya nini kifanyike lakin anasifu tu.Haoni mwenzie prof Shivji.? Kweli kwa namna hii kama kuna mtu anategemea Noah za Barrick basi afute kabisa mawazo yake.
waliokuwa wamekaa jirani naye walitakiwa kuwa na miamvuli sababu huyu jamaa kwa povu lile lazima uloane tu..!
 
Uchumi sio hadithi au filamu kiasi cha kumuelewesha mtu na kumlazimisha aunganishe matukio.
Uhumi ni kitu kinachoonekana kwa macho, kama mbaya utaonekana na kama mzuri utaonekana.

Ukimshusha mtu London, Cairo, Tunis, Paris, Casablanca, Durban, Beirut, Nairobi halafu ukamleta Dar es salaam sidhani kama itahitajika hadithi nyingi kwa huyu mtu kujua nafasi ya Dar es salaama na watu wake kufananisha na hao wengine.
Mkuuu umemaliza magufuli na watu wake hapa wameandaa mapambio mpaka watu wamechoka angalia padre na shivji maneno machache tu makofi mia
 
Anataka lazma usome kwa tabu hebu kama alaivosoma yeye inaaana hata kwenye maisha madam kaishi maisha ya tabu anataka kila mtu aishi kwa tabu seriously??
 
Si kweli, Nyerere huyu ni mjuaye?? Kuna hotuba yake ya mwaka 1969, anahimiza walimu wafunze vijana kuhoji mambo ya nchi yao. Ila ni huyuhuyu Nyerere amejenga kile tunachojivunia kama misingi ya taifa naomba rusha namba pm nikutumie clips zake akidai maendeleo ya kweli ya mtu ni uhuru.
Achana na hizo records, tafuta wakubwa unaowaamini waulize kama walikuwa huru Enzi za Baba wa Taifa.
 
hawa watu wanachekesha Kabudi kasha sema yote, Raisi kajikuta hana cha kusema ni kurudia yale yale

Yaani raisi anafanya remix ya kabudi.

anasema watendaji na yeye wamechukua mawazo ya watu na watayafanyia kazi, nikawaza mawazo gani maana mwanzo mwisho ni kusifia ujinga
 
"Nkrumah-UDSM: Yanayojiri kongamano la hali ya Uchumi na Siasa nchini Tanzania"

Kazi ipo, tuendelee kufuatilia.
 
Back
Top Bottom