Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Naomba aliye karibu / jirani na Profesa Mkandala ( Mtani wangu wa Kihaya ) ampe mkono wa hongera kwa niaba yangu na amwambie kuwa GENTAMYCINE nimemkubali na namkubali sana kwani ' uwasilishaji ' wake umenifanya nione tofauti kubwa kati ya Msomi wa Chuo Kikuu na Mhitimu wa Chuo Kikuu.

Ni Mwerevu sana
Ni Mzungumzaji mzuri
Ni Mkweli na hana Unafiki
Ni Mwenye Kujiamini na anakiamini kile anachokiwasilisha
Ni Mchambuzi wa Masuala aliyetukuka
Ni Hazina ya kweli kwa Wasomi wajao
Ni Mwanafasihi mzuri sana huku akijua kucheza vyema na ' Diplomatic Language '


Sijawahi kuona Mhaya ' Popoma ' na sishangai kuona au kusikia kwamba hata hapa Tanzania Elimu ilianzia Kwao Mkoani Kagera ( Bukoba ) ikaja kuweka Makao Makuu yake Kwetu Mkoani Mara ( Musoma )

Shikamoo Profesa Mkandala.
Wewe mkimbizi unatokaje Mara? Elimu ilianzia Kilimajaro kama ulikua haufahamu
 
Hapa tuliambiwa,rais hakujiandaaa kuhutubia ila hapa ukweli unakuja kuwa everything was organized.
 
Kwa kifupi hana jipya matangazo ya redio yani ni 1.Barabara
2. SGR - hapa hua anajichanganya mara kwa pesa zetu, mara mkopo
3. Wafanyakazi hewa
4.Tumenunua ndege
5.Tumewabana mafisadi
6. Elimu bure
7.Serikali inahela nyingi

Hua anakwepa maswala ya msingi yanayogusa watu moja kwa moja
1. Hali ya uchumi
2.kushuka kwa thamani ya hela
3.Kuboresha huduma za jamii i.e dawa za mahospitali
4. Umuhimu ya kuweka Levy ya Korosho
5. Yani hua hana jipya ukimsikiliza mpaka anatia huruma
 
Rais anakopa sana...
Na amesema anatumia hela za ndani...
Binafsi naunga mkono hoja Stiglers gorge
 
Kabudi hajadili Mada ya kongamano kabuni mada yake ya kutaja mafanikio.
Kikubwa ni kwamba kongamano kilipangwa Kuwa hivyo. Huyo mgeni mkuu ilikuwa asizungumze kabisa lakini alimpanga Prof Kabudi kutoa taarifa ya kiutwndaji ya miaka mitatu. Hatimaye kama ilivyokuwa 'imepangwa' mheshimiwa wa magogoni naye sasa anazungumza na watanzania kupitia kongamano hilo.
 
Rais anaomba asipongezwe sasa 'bado anachangamoto nyingi' apongezwe baadaye
 
Huyu inabidi apunguze unafki.

Anasema hapendi haya mambo ya vyama na hapo hapo ni mwenyekiti wa chama na wateule wake wanawanyima maendeleo waliochagua vyama vingine. Hawachukulii hatua yoyote.

Yeye mwenyewe anasema akuteue halafu utangaze mtu wa chama kingine. Hana kumbukumbu na maneno yake?
 
Sijui ni mimi tu nina waza mambo mengi sijui ni mchana umeingia njaa imeanza nishika sijui mawazo ya mshahara

Kwa kipindi kingi hua nikimsikiliza akiwa anahutubia hua anaongea mambo yale yale ya siku zote

Ila hotuba inaendelea......
Ndo vipaumbele vyake we unataka kumpangia vya kuongea,itisha press conference uzungumze kwa niaba yake unayotaka ayazungumze!
 
Kwa kifupi hana jipya matangazo ya redio yani ni 1.Barabara
2. SGR - hapa hua anajichanganya mara kwa pesa zetu, mara mkopo
3. Wafanyakazi hewa
4.Tumenunua ndege
5.Tumewabana mafisadi
6. Elimu bure
7.Serikali inahela nyingi

Hua anakwepa maswala ya msingi yanayogusa watu moja kwa moja
1. Hali ya uchumi
2.kushuka kwa thamani ya hela
3.Kuboresha huduma za jamii i.e dawa za mahospitali
4. Umuhimu ya kuweka Levy ya Korosho
5. Yani hua hana jipya ukimsikiliza mpaka anatia huruma
Huwa hapangiwi,we unataka umpangie!
 
haata wachungaji makanisani je huwa wana nini kipya zaidi ya kuhubiri kuacha dhambi?
 
Nashindwa kuchangia ila najiuliza, kwanini haandiki na kusoma alichoandika?
 
Back
Top Bottom