Mnachokifanya hapo UDSM siku hizi ni kukiua chuo kwa kasi kubwa. Hiyo hadhi mliyoikuta hapo UDSM ilijengwa na waliowatangulia, akina Dr. Lwaitama, Dr. Mvungi, Prof. Mpangala, Prof. Luhanga, Prof. Othman, Prof. Ngwale, Prof. Rugumamu, Prof. Chachage, n.k. Badala ya kuiendeleza hadhi ya chuo ninyi mmekuwa mstari wa mbele kufifisha chuo. Ona sasa hivi waziri anakuwa hata na ujasiri wa kuwapangia cha kufanya kwenye udahili wa wanafunzi. Kitakachofuata ni kupangiwa cha kufundisha. Ovyo kabisa UDSM kwa sasa. Ile chemchemi ya fikra mmeipoteza kwa kukumbatia kujipendekeza kwa watawala ili mpate vyeo.
Hakuna cha maana kitajadiliwa hapo. Kongamano lenyewe limeandaliwa kwa kusudi fulani kwa ajenda ya siri ya kutaka kutuaminisha kuwa jamaa anafanya kazi nzuri. Shame on you.