Kwenye makungamano kama haya, ukiona mchangiaji anafanya kazi ya kusifia tu, lazima mtu huyo ni mnafiki mkubwa.
Katika nchi hii watu wanaoongoza kwa unafiki na woga ni hawa wasomi ucgwara wanaojiita wasomi.
Tunawalalamikia viongozi lakini tukipewa nafasi ya kutoa maoni, kikubwa tunachokifanya ni kusifia. Huo ndiyo unafiki mkubwa.
Kiongozi anatakiwa kuambiwa ukweli, wapi anafanya vizuri na wapi anafanya vibaya. Ili mazuri yalindwe, mabaya yaondolewe, mapungufu yajadiziliwe na kupatiwa ufumbuzi.
Hivi hawa akina Mkumbo na Moshi, hawajaona lolote lenye mapungufu? Huu ni unafiki!
Pongezi nyingi kwa Prof. Mukandala (nimemtaja kama professor kwa vile nadhani anastahili. Hawa wengine siamini kama kweli ni maprofesa). Mukandala ameeleza maeneo ambako awamu hii wamefanya vizuri lakini kataja mapungufu.
Huyu askofu ametoa summary nzuri sana, amataja maeneo ya kutazamwa na kuboreshwa. Viongozi wanatakiwa kuoneshwa maeneo wanayofanya vibaya ili wafanye vizuri.
Padre Kitima wa Baraza la Maaskofu anasema
Kuna tatizo kwenye tume ya Uchaguzi naomba iongelewe
Kuna tatizo kwa watendaji wa chini wananyanyasa wananchi mfano Wakuu wa Wilaya
Uchumi umekuwa lakini kwa wananchi haionekani. Sekta binafsi ijengwe ambayo itasaidiana na Serikali. asanteni