Hata Magufuli mwenyewe anajua Watanzania wanataka katiba mpya, lakini maneno yake yanaonesha woga wa mabadiliko kwa sababu anafaidika na ubovu wa katiba uliopo. Ndo maana kasema hata akipewa hiyo fedha na mtu ataitumia kujenga reli. Ninachoungana naye ni kutokubali watu kulundikana Dodoma kupiga soga huku wakidanganya kila mmoja yuko busy kutunga katiba wakati wengi hakuna wanachofanya zaidi ya kutumika kishabiki. Ukiangalia bunge la Katiba lililopita utashangaa baadhi wa wajumbe walikwenda kufanya nini Dodoma na kwa nini walilipwa? Mtu kama Aeshi Hilary, Ally Kessy, Kibajaji, Sugu, Makonda....!!"Jesca John - Mwanafunzi wa kidato cha Sita chang'ombe.
Tutathini ni nini kifanyike ili rais ajaye asiharibu kile kilichofanywa na Magufuli, tunahitajij wakina Magufuli katika Miongo mitatu. Asante "
Sijui kama hoja ya mwanafunzi huyu kuna aliyeizingatia. Ana hoja nzito. Sawa kwa wale tunaoamini kuwa tumepata 'malaika', je huyu 'malaika' akimaliza muda wake au Muumba akampenda zaidi ya sisi tunavyompenda, haya mambo yake ya kimailaka nani atayaendeleza? Je tutapata 'malaika' mwingine? Je, tunafanya maandalizi yo yote ya kuendelea kupata 'wamalaika' tuseme katika miaka 50 ijayo? Kwa maoni yangu huyu binti alikuwa anasisitiza suala la uwepo wa Katiba mpya iliyobora itakayohakikisha kila zuri lililotendwa na 'malaika' litadumishwa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Vinginevyo vitukuu vyetu kuna siku vitapiga bakora makaburi yetu! nachema tu
Wazungu hawakwepeki kabisa hata tufanyeje Hali ikizidi Kuwa mbaya lazima magoti yapigwe Nyerere alibana wee akaona anaumiza wananchi akajiuzulu. Tunahtaji kushirikiana nao in positive wayTulipo fikia kama taifa hatuwezi kuwakwepa hawa wazungu tunadanganyana tu kila kitu tunacho tumia wametengeneza wao. Taifa kama ujeruman mkuu wao wa nchi alikuwa anarecodiwa. Sasa huku kwetu sindiyo balaa kabisa! mkuu wetu pengine wanamwona kila anacho fanya. [emoji3][emoji3]
Anaogopa katiba mpya. Iliyopo ndio inampa umungumtu.*YALIYOSEMWA NA RAIS MAGUFULI UDSM 01/11/2018*
"Nchi yetu ina akiba ya Dola Bilioni 5.4, fedha hizo zinaweza kununua bidhaa kwa kipindi cha miezi 6, hatujawahi kuwa na kiasi hicho cha fedha tangu tupate uhuru." - Rais Magufuli
"Mfumuko wa bei umeendelea kuwa imara kwa asilimia 3.4 hadi 3.6 na kutokana na hilo nchi yetu ni miongoni mwa nchi tano za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi." - Rais Magufuli
"Katika kipindi cha miaka mitatu zaidi ya viwanda vipya 3066 vimejengwa, na tukishatengeneza viwanda tayari tumeshakuza ajira." - Rais Magufuli
"Nchi yetu ni ya pili kwa kuwa na mifugo mingi Afrika lazima tujiulize na tuweze kuchukua hatua ya kutumia malighafi hizo kujitengenezea bidhaa zetu wenyewe." - Rais Magufuli
"Si vyema kwa nchi yetu ambayo ina utajiri wa kila kitu tukaendelea kuwa watengenezaji wa malighafi pekee hivyo ni lazima viwanda viwepo ili tutengeneze bidhaa wenyewe na kukuza ajira." - Rais Magufuli
"Kazi ya urais ina changamoto nyingi sana. Nimekuwa Waziri kwa miaka 20, ila hizi changamoto ni zaidi. Ukienda chumbani kwangu kuna mafaili hadi kitandani. Huwa najiuliza, wenzangu waliwezaje kuyamaliza yote? Huwa natamani niwaoneshe hayo mafaili." - Rais Magufuli
"Watoto wangu wamefunga harusi, tena wengine wamefunga nikiwa Rais, lakini hamkuwahi kusikia sherehe zao." - Rais Magufuli
"Siku mimi nimefunga ndoa, sikuvaa koti, wala mke wangu hakuvaa shela. Tulienda kanisani Chuo Kikuu (UDSM), Padri alitununulia pete, ilikuwa ya shaba, kisha akatununulia soda, nikanywa pepsi, mke wangu akanywa mirinda, mambo yakaishia hapo." - Rais Magufuli
“Dk. Bashiru alipigwa vita CCM wakasema huyu ni CUF na mimi nikasema nataka CUF wa namna hii CCM, CCM wenyewe ni kwasababu hawakutaka mabadiliko namshukuru huyu CUF wa CCM aliyetoka chuo kikuu kwa kunisaidia"-Rais Magufuli
"Demokrasia nayo ina mipaka yake sio fujo na mkishamaliza uchaguzi mahali pa mabishano ni Bungeni"-Rais Magufuli
"Hii sheria ya madini wapo walioipinga bungeni, leo nimewaambia tumekusanya Bilioni 301 hizi fedha haziendi CCM zinaenda kwenye miradi ya wananchi"-Rais Magufuli
*Shilatu E.J*
Utawala bila katiba ni vurugu tupu.Wakati mchakato wa Katiba Mpya ukiwa umesimama na haijulikani utaendelea lini, Rais John Magufuli amesema hawezi kutenga fedha kuendelea na mchakato huo, ni vyema fedha hizo zikatumika katika ujenzi wa reli ya kisasa.>>>Magufuli asema hawezi kutenga fedha za mchakato wa Katiba Mpya
Kwa maana hiyo kuwa na katiba ya kuwabana wanaoitwa watawala ni upotevu wa hela ila wao kila siku kutunga sheria kuwabana raia ni sahihi kabisa. Na kurudia chaguzi za maigizo ni sahihi kabisa