Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Mleta mada nikukumbushe tu kwamba Rais hakoseagi, Lakini pia tulimchagua wenyewe, na tuna mwamini,


Nb:mheshimwa Jpm unikumbuke kwenye UDC popote ntakwenda, naunga mkono juhudi zako.
 
Bora isiwe hivyo... Hatuwezi kupata katiba bora chini ya utawala huu. Chansi ya katiba huru tulikwamishwa na wana siasa akina Mh. SITA (R.I.P).
Katiba mpya ilishindikana kwa sababu ya unafki wa JK. Alitoa nafasi ile kinafki na baadaye alihakikisha wabunge hawawi wamoja !!.

Ratiba ya lile bunge ilikuwa Rais alifungue kisha Mzee Warioba awasilishe .
Lakini maksudically ratiba ilibadilisha ili aje aiponde !! Na tangia hapo CCM walikuwa radhi hizo fedha zipotee kulinda mfumo uliopo kwa vile unawahakikishia kutawala watakavyo.

Kwa hili la Maghufuli ni ile ile kwa katiba iliyopo, atafanya chochote atakacho na hakuna wa kumhoji. Na kwa jinsi anavyotumia vyombo vya dola na hata hazina inahitaji katiba hii ya zamani. Vinginevyo anafikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka.
 
Mchakato ulikuwa ni batili kwa sababu Watanzania wenzetu wanaojulikana kama UKAWA, walisusia. Kwa hiyo ili haki itendeke, ni vema mchakato ukaanza upya ili nao washiriki.
 
Nchi ni Mali yake
 
Rais ndiye katiba kwa sasa, msitake kuchezea pesa, bora tukajengee Stiegler's gorge
 
Alichokiongea kwa mujibu wa uvunjaji katiba ni sahihi kwa sababu Hata uwepo wa katiba Hakuna kiongozi wa ngazi Kama ya uraisi anayeifuata katiba na anachokifanya anakujua ndio maana amesema sio mwarobaini lkn anaumiza kwa kauli zake
 
Kwani anachokosea ni nini wakati hata kwenye kampeni alisema hatashughulikia issue ya katiba. Tatizo mkiambiwa ukweli mnafura hasira. Alishasema mara nyingi tu katiba si kipaumbele kwake. Hii ya sasa tu hatuifuati je hiyo mpya ndio tutaifuata.
 
Reactions: Oii
Mleta mada nikukumbushe tu kwamba Rais hakoseagi, Lakini pia tulimchagua wenyewe, na tuna mwamini,


Nb:mheshimwa Jpm unikumbuke kwenye UDC popote ntakwenda, naunga mkono juhudi zako.
Naomba utuombe radhi Watanzania, hatujawahi kumchagua huyu MTU ila Lubuva aliambiwa amtangaze kwa sababu wanazozijua wao na kwa faida zao, naomba samahani kama nimekukera my brother ila ukweli ndo huo.
 
"Malaika" hataki kuweka misingi ya uongozi anayoitenda kwenye Katiba Mpya. "Malaika" kasema wazi suala la kuweka misingi yake kwenye katiba mpya ni kupoteza pesa. Na mimi naona "Malaika" atukimbize hivyo hivyo mpaka tunyooke hata kama ni miaka 20!
 
Mkuu kwanini unataka Katiba Mpya?
Unafikiri nini Kitabadilika Katika Utekelezaji ikija Katiba Mpya?
Unahisi mambo "Yako"Ambayo unatamani yawe yanashindikana kwasababu hayamo katika Katiba ya Sasa?
Je Yale unayoyapenda ambayo yapo kwenye Katiba ya sasa Ni Kwa Kiasi gani Yanatekelezwa?
Au unadai tuuuu Mpyaaa,Mpyaaa Ili ionekane una kitu Kipya?
Ni Kupoteza hela tuu.Maendeleo Kwanza!
 
Naomba utuombe radhi Watanzania, hatujawahi kumchagua huyu MTU ila Lubuva aliambiwa amtangaze kwa sababu wanazozijua wao na kwa faida zao, naomba samahani kama nimekukera my brother ila ukweli ndo huo.

Sema wewe hujawahi mchagua mtu.Mie nilimchagua Magufuli na nitamchagua tena.
 
Walokula wengi bado wako CCM.

Warudishe salio.

Mchakato haujakamilika.
 
Kwanza kabisa magu akitaka kuongea huwa haandaliwi hotuba kama mnavodhan, anaongeaga lolote kutokana na mood aliyonayo ndo maana asilimia kubwa ya hotuba zake ni pumbaa tupuu huku majitu na elimi zao wanachekelea chekelea tuu,

Nikimwangalia kwa undani zaidi huyu mtu utagundua kuwa kawa raisi kwa bahati mbaya na nchi ishamshinda, sema tuu ndo hivo tena hana namna, watanzania wachache wanaoliona hili,
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Mkuu utakufa kabla ya wakati si wako!

Narudia tena tafuta mshauri nasaha
Jiwe ndio wa kutafuta ushauri nasaha,katiba ni mali ya wananchi yeye anaweka kauzibe.
 
Sitegemei kutenga fedha kwa ajili ya watu kula wakakae bungeni kujadili katiba, hata kama kuna mtu anataka kutupa hizo fedha, atupe tukatengeneze reli. Watu wanakaa wanapiga kelele katiba mpya, utadhani katiba ndio mwarubaini wa kila kitu.
Hapa nadhani ndio pa kumwambia ukweli mheshimiwa, pamoja na mazuri anayoyafanya katiba itamsaidia sana, maana bila katiba imara yeye akiondoka akija mwingine legelege tutarudi kule kule kwenye upigaji
 
Lakini hela za kuwahonga wabunge/madiwani wa upinzani anazo. Na kutumia mabilioni kurudia chaguzi za watu ambao wako hai hawajafa anazo.
Tuna shauri hizo ndizo ziende kwenye reli na umeme. Za katiba zitoke maana katiba ndio hutoa dira na mustakabali wa raia.
 
Lakini za kununua wabunge wa upinzani na kurudia chaguzi zenyewe zipo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…