Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Sisi tuliokosa fursa ya kuzungumza pale Nkuruma Hall katika kongamano la uchumi na siasa tutoe maoni yetu.

Mawazo yangu
Kuhusu uchumi - Kilimo kipewe kipaumbele sawa na sambamba na viwanda. Tafiti za kilimo, Mifugo na miradi mikubwa ya umwagiliaji vfanyike. Miundo mbinu ya umwagiliaji ni muhimu saaana, itatengeneza ajira kubwa sana na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja.

Kiswahili - ni moja ya utambulisho wa taifa. Rais ndio Tanzania one. Huyu ndio anapaswa kuwa no. 1 kuongea kiswahili bila kuchanganya ma-lugha mengine ya kigeni. Wasaidizi wake wafanye jitihada za kumpatia msamiati wa kiswahili ulioshiba ili kuwezesha hotuba zake zisheheni kiswahili kisicho kuwa na chenga wala pumba.

Huduma za jamii- utaratibu wa elimu bure uendelezwe. Bima za afya za bei nafuu zisambazwe hadi vijijini. Kupitia vitambulisho vya taifa, Ruzuku ya matibabu toka serikalini itolewe kwa kila mtanzania.Hapa ninamaana ya Matibabu BURE.

Kuhusu Siasa: Acha vyama vya sasa vifanye kazi zake. Tuipe theory ya struggle of opposites ifanye kazi zake. Kwenye kukinzana ki mawazo au mtizamo kunazaa kitu bora.

Mengineyo.
Michezo: Sector hii haipewi uzito unaostahili. Michezo ni ajira, ni biashara, ni afya, ni mahusiano mazuri ya jamii, ni Mjumbe mzuri wa taarifa yeyote ile. Nashauri uongozi wa awamu hii ya 5 inayosomeka kwa namba T2025 JPM Ichukue hatua za maksudi kuimarisha sects ya michezo.
 
Kufuatia kauli ya Rais Magufuli aliyotoa jana kwenye Kongamano la kujadili miaka yake mitatu madarakani, kwamba yeye hatathubutu kutoa hata senti kwa ajili ya Mchakato wa Katiba mpya, wengi wamesononeka na kusikitika, hasa wale ambao wanaona kwamba suluhisho la matatizo ya kiutawala na utendaji katika ngazi za juu za serikali yetu, ni Katiba Mpya, hasa kwa maudhui ya Muswada wa Tume ya Warioba.

Namkumbuka Askofu NiweMugizi, ambaye kuhusiana na suala hili la katiba mpya, aliapa kwamba yuko tayari kuitwa mchochezi. Na kwa kweli ameitwa mchochezi na serikali inamshughulikia kwa kumnyanyasa kwa uchunguzi usio na mwisho kuhusu uraia wake, na kuipa fursa serikali kushikilia paspoti yake kwa muda mrefu na usiojulikana.

Lakini ukifikiria "Nje ya Boksi", kwanza utafurahi kwamba Magufuli hataki Mchakato wa Katiba Mpya, na utakwenda kanisani kumshukuru Mungu kwa hilo, au utasoma dua kumshukuru Mnyaazi Mungu kwa hatua hiyo ya Magufuli.

Kwa nini? Kwanza kabisa, Magufuli haheshimu Katiba na sheria. mpaka sasa ameshavunja vipengele vingi tu vya Katiba na sheria mbalimbali za nchi. mojawapo ya uvunjaji wa Katiba ni kuzuia vyama vya upinzani vinavyotambulika kisheria na kikatiba, kufanya kazi zake. pili amevunja vifungu vya Katiba vinavyomhakikishia mwananchi uhuru wa kutoa maoni yake na haki mbalimbali. amevunja sheria mbalimbali za matumizi ya fedfha za serikali na sheria za manunuzi. Hivi kwa akili za Magufuli, Katiba ni yeye mwenyewe na kauli zake na anavyojisikia. na kwa hiyo huwezi kumlaumu pale anapofikia hitimisho kwamba kutumia mabilioni kuandika maelezo ambayo yeye mwenyewe hatayafuata, ni kupoteza fedha bure, heri akajengee barabara. ukiwa na Rais aina ya Magufuli, hiyo ni LOGICAL CONCLUSION.

Lakini sababu kubwa zaidi ni kwamba kwa utaratibu tulionao hapa nchini, Mchakato wa Katiba mpya ukianza, utasimamiwa na Rais, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa CCM, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama. Ni kitu gani kitatokea hapo? Kwa sababu kama kwa katiba hii tu, Magufuli anaendesha aina hii ya chaguzi za marudio, je akiambiwa sasa simamia katiba mpya, tutapata katiba ya aina gani hasa? huyo mtoto atakayezaliwa, tunayetarajia kwamba atakuwa suluhisho la matatizo yetu, atakuwa ni binadamu anyway? siamini kama kitazaliwa kiumbe cha kueleweka.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete alimruhusu Jaji Warioba kuandaa katiba ya kweli na nzuri. Lakini hata yeye mahali fulani akahujumiwa na CCM, kikatokea hicho kichotara kinaitwa KATIBA PENDEKEZWA. Hicho kichotara mimi hata sitaki kukisikia kabisaa. sasa tunapomtaka Magufuli "aendeleze" mchakato wa katiba mpya, hivi akiamua kutoa "decree" kwamba hiyo KATIBA PENDEKEZWA ikapigiwe kura ya maoni, na kwa aina ya uendeshaji wa chaguzi zetu ulivyo, katiba hiyo si itapata 99.99999% ya kura za ndio? Na hapo tutakuwa tumeingia kwenye MTANZIKO mkubwa zaidi. Maana kimsingi watu wa CCM watasema mambo ya katiba yamemalizika sasa tuangalie mengine. hapatakuwa tena na hoja ya katiba mpya yenye nguvu na itakayosimama, kwa miaka mingi ijayo.

Na hata kama Magufuli akikubali tuanze upya mchakato, hivi unadhania huyu Polepole wa sasa atakuwa kama yule wa zamani enzi za katiba ya Warioba? hapo si ndio tutapata kitu cha ajabu kabisa na Magufuli ataharakisha kukitia saini?

Mimi naona ni heri tu kwamba Magufuli hataki kusimamia mchakato wa Katiba mpya, kwa sababu hana uwezo wa kutoa katiba halali yenye kubeba matarajio ya watanzania kwa miongo mingi ijayo. Kazi hiyo isubiri tu rais mwingine ajaye huko mbele. Ni aheri tujue tu kwamba mchakato wetu haujakamilika, Inshaalah atapatikana mtu aina ya Kikwete wa pale mwanzoni, na Inshaalah Warioba atakuwa bado na nguvu za kuendelea, au kutapatikana mrithi wake mwenye busara na hekima kukutanisha watu wa bara na visiwani wakae na kutoa kitu maridhawa kama hiki cha sasa.

Magufuli tumwache tu aendelee kujenga mabarabara yake, maflyover, kununua ndege, kuchimba mitaro, hizo ndio kazi anazoweza. hayo mengine tunamtwisha mzigo asiouweza na ataharibu kazi kwa hasara ya vizazi na vizazi. hizo hasara anazolitia taifa kwa sasa zinatosha, hatuhitaji kuongeza hasara zingine.
 
Pesa za kununua wabunge na kurudia uchaguz izo anazo. We subir 2020 ataelezac1.5t kazipeleka wapi.
 
Rais dikteta hawezi kuleta katiba yenye kubeba matarajio ya wananchi kwa miaka mingi ijayo, kwa sababu katiba hii mbovu inampa kiburi cha kufanya chochote kile akijua hakuna wa kumfanya kwa sasa na hata baada ya kuwa nje ya madaraka
 
yale ndiyo yalikuwa malengo ya baraza lile la kahawa.
ona namna yule mwanafunzi alivyojipanga. ati anaulizia upatikanaji wa MAGUFULI kwamba hakukuwa na mtu aloandaliwa / succession planning ye kajuaje? kwamba asitokee mtu akagombea na kuharibu mipango ya MAGUFULI, hii imetokana na yale makelelee ya twende na membe 2020 hapo wiki iliyopita! anakwenda anasema waje MAGUFULI wengine watatu mbele. huyu ni amma anawandaa wananchi kisaikolojia au anawatisha washindani wake kisiasa
Kwa hilo umenena
 
Roving journalist imekuwaje Uzi wangu ukaungwa na wako ?
 
Kufuatia kauli ya Rais Magufuli aliyotoa jana kwenye Kongamano la kujadili miaka yake mitatu madarakani, kwamba yeye hatathubutu kutoa hata senti kwa ajili ya Mchakato wa Katiba mpya, wengi wamesononeka na kusikitika, hasa wale ambao wanaona kwamba suluhisho la matatizo ya kiutawala na utendaji katika ngazi za juu za serikali yetu, ni Katiba Mpya, hasa kwa maudhui ya Muswada wa Tume ya Warioba.

Namkumbuka Askofu NiweMugizi, ambaye kuhusiana na suala hili la katiba mpya, aliapa kwamba yuko tayari kuitwa mchochezi. Na kwa kweli ameitwa mchochezi na serikali inamshughulikia kwa kumnyanyasa kwa uchunguzi usio na mwisho kuhusu uraia wake, na kuipa fursa serikali kushikilia paspoti yake kwa muda mrefu na usiojulikana.

Lakini ukifikiria "Nje ya Boksi", kwanza utafurahi kwamba Magufuli hataki Mchakato wa Katiba Mpya, na utakwenda kanisani kumshukuru Mungu kwa hilo, au utasoma dua kumshukuru Mnyaazi Mungu kwa hatua hiyo ya Magufuli.

Kwa nini? Kwanza kabisa, Magufuli haheshimu Katiba na sheria. mpaka sasa ameshavunja vipengele vingi tu vya Katiba na sheria mbalimbali za nchi. mojawapo ya uvunjaji wa Katiba ni kuzuia vyama vya upinzani vinavyotambulika kisheria na kikatiba, kufanya kazi zake. pili amevunja vifungu vya Katiba vinavyomhakikishia mwananchi uhuru wa kutoa maoni yake na haki mbalimbali. amevunja sheria mbalimbali za matumizi ya fedfha za serikali na sheria za manunuzi. Hivi kwa akili za Magufuli, Katiba ni yeye mwenyewe na kauli zake na anavyojisikia. na kwa hiyo huwezi kumlaumu pale anapofikia hitimisho kwamba kutumia mabilioni kuandika maelezo ambayo yeye mwenyewe hatayafuata, ni kupoteza fedha bure, heri akajengee barabara. ukiwa na Rais aina ya Magufuli, hiyo ni LOGICAL CONCLUSION.

Lakini sababu kubwa zaidi ni kwamba kwa utaratibu tulionao hapa nchini, Mchakato wa Katiba mpya ukianza, utasimamiwa na Rais, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa CCM, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama. Ni kitu gani kitatokea hapo? Kwa sababu kama kwa katiba hii tu, Magufuli anaendesha aina hii ya chaguzi za marudio, je akiambiwa sasa simamia katiba mpya, tutapata katiba ya aina gani hasa? huyo mtoto atakayezaliwa, tunayetarajia kwamba atakuwa suluhisho la matatizo yetu, atakuwa ni binadamu anyway? siamini kama kitazaliwa kiumbe cha kueleweka.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete alimruhusu Jaji Warioba kuandaa katiba ya kweli na nzuri. Lakini hata yeye mahali fulani akahujumiwa na CCM, kikatokea hicho kichotara kinaitwa KATIBA PENDEKEZWA. Hicho kichotara mimi hata sitaki kukisikia kabisaa. sasa tunapomtaka Magufuli "aendeleze" mchakato wa katiba mpya, hivi akiamua kutoa "decree" kwamba hiyo KATIBA PENDEKEZWA ikapigiwe kura ya maoni, na kwa aina ya uendeshaji wa chaguzi zetu ulivyo, katiba hiyo si itapata 99.99999% ya kura za ndio? Na hapo tutakuwa tumeingia kwenye MTANZIKO mkubwa zaidi. Maana kimsingi watu wa CCM watasema mambo ya katiba yamemalizika sasa tuangalie mengine. hapatakuwa tena na hoja ya katiba mpya yenye nguvu na itakayosimama, kwa miaka mingi ijayo.

Na hata kama Magufuli akikubali tuanze upya mchakato, hivi unadhania huyu Polepole wa sasa atakuwa kama yule wa zamani enzi za katiba ya Warioba? hapo si ndio tutapata kitu cha ajabu kabisa na Magufuli ataharakisha kukitia saini?

Mimi naona ni heri tu kwamba Magufuli hataki kusimamia mchakato wa Katiba mpya, kwa sababu hana uwezo wa kutoa katiba halali yenye kubeba matarajio ya watanzania kwa miongo mingi ijayo. Kazi hiyo isubiri tu rais mwingine ajaye huko mbele. Ni aheri tujue tu kwamba mchakato wetu haujakamilika, Inshaalah atapatikana mtu aina ya Kikwete wa pale mwanzoni, na Inshaalah Warioba atakuwa bado na nguvu za kuendelea, au kutapatikana mrithi wake mwenye busara na hekima kukutanisha watu wa bara na visiwani wakae na kutoa kitu maridhawa kama hiki cha sasa.

Magufuli tumwache tu aendelee kujenga mabarabara yake, maflyover, kununua ndege, kuchimba mitaro, hizo ndio kazi anazoweza. hayo mengine tunamtwisha mzigo asiouweza na ataharibu kazi kwa hasara ya vizazi na vizazi. hizo hasara anazolitia taifa kwa sasa zinatosha, hatuhitaji kuongeza hasara zingine.
Ilikuwa ni haki yako kabisa kuwa mmoja wa wanaJF.
 
Sisi tuliokosa fursa ya kuzungumza pale Nkuruma Hall katika kongamano la uchumi na siasa tutoe maoni yetu.

Mawazo yangu
Kuhusu uchumi - Kilimo kipewe kipaumbele sawa na sambamba na viwanda. Tafiti za kilimo, Mifugo na miradi mikubwa ya umwagiliaji vfanyike. Miundo mbinu ya umwagiliaji ni muhimu saaana, itatengeneza ajira kubwa sana na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja.

Kiswahili - ni moja ya utambulisho wa taifa. Rais ndio Tanzania one. Huyu ndio anapaswa kuwa no. 1 kuongea kiswahili bila kuchanganya ma-lugha mengine ya kigeni. Wasaidizi wake wafanye jitihada za kumpatia msamiati wa kiswahili ulioshiba ili kuwezesha hotuba zake zisheheni kiswahili kisicho kuwa na chenga wala pumba.

Huduma za jamii- utaratibu wa elimu bure uendelezwe. Bima za afya za bei nafuu zisambazwe hadi vijijini. Kupitia vitambulisho vya taifa, Ruzuku ya matibabu toka serikalini itolewe kwa kila mtanzania.Hapa ninamaana ya Matibabu BURE.

Kuhusu Siasa: Acha vyama vya sasa vifanye kazi zake. Tuipe theory ya struggle of opposites ifanye kazi zake. Kwenye kukinzana ki mawazo au mtizamo kunazaa kitu bora.

Mengineyo.
Michezo: Sector hii haipewi uzito unaostahili. Michezo ni ajira, ni biashara, ni afya, ni mahusiano mazuri ya jamii, ni Mjumbe mzuri wa taarifa yeyote ile. Nashauri uongozi wa awamu hii ya 5 inayosomeka kwa namba T2025 JPM Ichukue hatua za maksudi kuimarisha sects ya michezo.
Ili nchi iendelee yahitaji tukubali kujitazama kutoka moyoni na bila kupepesa macho: Je tuna
Siasa safi, Uongozi bora, na juhudi gani kupambana na umasikini, na kujenga uchumi wenye misingi imara na endelevu.
Wasomi wetu sasa hivi mmeacha wajibu wenu wa kuongoza tathmini kwa faida ya Watz, na kuwa waongoza mapambio kwenye ibada ya kumtukuza Mfalme Jiwe. Njaa zenu zimewafanya kuwa watumwa na zinatupeleka shimoni. Amen.
 
Back
Top Bottom