Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Kati ya vitu ambavyo hukujaaliwa ni kujenga hoja.
Mkuu huyu bwege si kwamba hakujaliwa kujenga hoja,bali hakujaliwa akili,hana akili kabisa,ana ubongo wa kuku,kichwani mwake anajua kuichukia Chadema tu basi,hana kingine ajuacho zaidi ya chuki
 
Kwa Mara ya kwanza baada ya kupita miaka mingi tume shuhudia kongamano ambalo kwa kiasi Fulani lilikuwa na muelekeo wa kutupatia japo kwa kiwango muelekeo wetu wa kiuchumi na kisiasa na kiuchumi kama Taifa. Hilo lilikuwa ni wazo zuri ila kwa upande wangu binafsi niliona kama kuna baadhi ya dosari ambazo zilijitokeza, na hili nalisema kwa nia njema kabisa na nikiwa nimelenga kuwa siku za usoni kama itatokea fursa kama hizi basi tunaweza kufanya maboresho.
1: Niliona wasomi wetu wakikosa ujasiri wa kujieleza, ulikuwa ukiwatazama vizuri usoni walionyesha kama vile kuna jambo la kuongelea ila uoga uliwatala.
2: Baadhi yao hawakujikita kwenye uhalisia wa mada na badala yake walilenga kwenye kumsifia mh jambo ambalo najua kabisa kuwa hata mh hakufurahishwa nalo kwa sababu hawakulenga mkusaidia isipokuwa walilenga kujipendekeza.
3: Jambo jingine lilo jitokeza ni ubaguzi wa elimu kama kuna mtu aliskiliza kwa makini ilionyesha wazi kuwa kama umepata shahada yako mbali na UDSM basi hiyo shahada yako ni ya mashaka, nazungumzia vyuo vya kwetu Tz.
4: kushiriki kwa mh kwenye kongamano kulipunguza uwazi wa washiriki kujieleza, nadhani kwa Mara nyingine kama itatokea napendekeza mh Rais asihudhurie ili wachangiaji japo kwa kiasi Fulani wapunguze ule uoga wa kuwa huru kujieleza.
5: Swala la katiba kama kweli na ndivyo ilivyo kuwa kiwango kikubwa kiu ya wa Tanzania nikupata katiba mpya , hili ni kwa nia njema kabisa ili mambo mazuri yanayo fanyika sasa yaweze kupewa ulinzi wa kikatiba , lakini kama tutakuwa na mawazo kuwa swala la katiba lina lenga kudhohofisha malengo ya watu Fulani kisiasa tutakuwa hatulitendei Taifa letu haki na wananchi kiujumla na hasa vizazi vitakavyo kuja baada yetu.
Pamoja na hayo pia kuna mambo mazuri ambayo niliyasikia kwa baadhi ya wachokoza mada, kuna professor yule aliye kuwa wa kwanza kuchangia alizungumzia swala la kilimo kinavyo weza kutengeneza upacha na maendeleo ya viwanda, akasema wazi kuwa hatuwezi kufikia maendeleo ya viwanda kama hatutawekeza zaidi kwenye kilimo, hili lilinifurahisha nakuonyesha ni jinsi gani alivyokuwa amejipanga kumsaidia Rais na Taifa lake kiujumla.
Kwa hilo siwezi kupita bila kumpatia kongole mh Rais kwa jinsi alivyo kuwa muwazi na kusema kuna fedha zipo zimetengwa kwa ajili ya kukopesha wale watakao taka kuwekeza kwenye kilimo, hili ni jambo jema, jambo ninalo liona hapa sasa ni serikali kutoa hamasa kwa wananchi ili wajiingize kwenye sekta ya kilimo kwa wingi zaidi.
Mwingine niliyeona amechangia vema ni yule mama Professor alijaribu kuonyesha ni kwa jinsi gani lugha ilivyo kuwa ni kiunganishi kizuri katika kukuza uchumi, ni jambo zuri kuwa tumebahatika kuwa na lugha inayo tuunganisha kama Taifa , lakini tukubali kuwa lugha za kutuunganisha kibiashara na mataifa mengine bado zitakuwa ni hizo lugha zilizo zoeleka, sasa basi jambo la muhimu kwetu ili tufanikiwe kukiingiza kiswahili ni kufanya jitihada ya kukiambukiza kwa mataifa mengine hasa tuki yalenga hayo mataifa makubwa ya ulaya na Asia. Kwa upande huku kwetu afrika hakuna shaka kuwa dalili ni kubwa sana za kufanikiwa kwa hili.
Asanteni sana wadau .
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Nilikua nikirudi kwenye mishe mishe na sikujua nin kinaendelea mara katika radio ndo nikaskia hilo jambo la number 3.

Ilibaki najiuliza sasa wala walosoma college na university tofauti na hizi zinazojulikna wao nafas yao ikatukua wapi kutokna na alivyosema.
 
Wateule wa mheshimiwa wamejiandalia kongamano, kisha wakatumia jukwaa kumsifu aliyewapa kula!

Nilitegemea wakazungumzie habari za nchi kwa kina, kwa data, kwa nguvu ya hoja na ushahidi wa wazi, lakini wakaishia kumzungumzia Magufuli utadhani Magufuli ndiyo nchi yenyewe!,

Maprofesa wetu badala ya kudiscus ideas, wakaanza kudiscuss kuhusu Mtu (Magufuli), eti kafanya hili, kafanya lile, bila Data, Bila Critical analysis yoyote!

Kwa mfano unaposema Mheshimiwa kanunua ndege, tuambie kwa takwimu mpaka sasa hivi ndege zilizokweisha nunuliwa zimeiingizia nchi kiasi gani na matumizi yamekuwa kiasi gani na Je Tusingenunua hizo ndege pesa tukaziingiza mathalani sehemu nyingine kama vile elimu, barabara utofauti katika maisha ya Mtanzania ungekuwaje?

Au Je Mathalani tungewekeza katika chuma chetu cha liganga na mchuchuma kisha tukajengea hiyo reli kwa mataaluma kwa mataaluma ya chuma chetu wenyewe tungesevu kiasi gani?. Haya ndiyo mambo nilitegemea maprofesa watu wamwambie mheshimiwa!

Ndiyo maana Tundu Lissu akatumia maneno makali ya "Professorial Rubbish" kwa baadhi ya kazi za Maprofesa. Wanashindwa kusimama na kutoa mawazo kwa uhuru na kwa nguvu ya hoja wanabaki kuimba sifa tu kama Polepole na Lusinde

Jana kazi ya Maprofesa watoa mada hata Msemaji wa CCM Polepole haoni ndani kwa jinsi walivyokuwa wakimwaga misifa na kuimba mapambio mbele ya mheshimiwa!. AIBU!!
 
Sijui kama nitakuwa nimenukuu katiba sawa sawa! Naomba ksahihishwa ikiwa nimekwenda kombo

Serikali na watu Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;

(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;

(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;

(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Jokakubwa Pascal Mayalla Mag3
 
Kongamano lile lilikua ni kujadili hali ya uchumi ndani ya miaka mitatu ya Magufuli
Maprofessor wote waliainisha njia walizopitia katika kuandika mada zao
Chaso andaeni kongamano lenu mana mlitegemea Rais atukanwe haikua
 
Kongamano la Tathmini ya hali ya kiuchumi na kisiasa likawa kongamano la kumsifia Magufuli. Ni mpango ulioandaliwa kabla, ili kumjengea Rais Magufuli imani kwa wananchi, imani inayopotea kila kukicha kutokana na matendo ya hovyo ya serikali ya awamu ya tano.
Sikusikia mambo mazito yakigusiwa, matukio ya utekaji, upoteaji wa watu yenye viashiria vya uhusika wa vyombo vya usalama, ongeza na jaribio la mauaji ya Mh. Tundu Lissu.

Mauaji ya raia ndani na nje ya vituo vya polisi.

'Uchuro' wa tume ya uchaguzi iliyogeuzwa kuwa idara ya chama cha mapinduzi.
Utumwa wa bunge kwa serikali.
Serikali kuingilia kazi za mahakama.
Kauli za Rais, zinazofifisha hadhi ya taasisi ya Urais, kama ile ya kuwapiga mashangazi wa wabunge wa kusini, kauli ya kupinga uzazi wa mpango, kauli za kuchochea chuki kati ya jeshi la polisi na raia wenye mawazo kinzani hususani viongozi wa vyama vya upinzani.

Hayo ni baadhi ya hoja nzito zilizopaswa kujadiliwa.

Maprofesa wetu, hasa Kitila Mkumbo na Kabudi Paramaganda, waliamua kwa makusudi, au pengine ndio ulikuwa mpango, kugeuza kongamano na kuwa mkutano wa kampeni. Mambo mengi waliyogusia ni mambo Mtambuka, wajibu wa serikali.
Ingependeza kusikia mjadala wa kifalsafa zaidi kama alivyofanya Profesa Mukandala. Hayo ya mambo ya mipango ya serikali kila mwaka tunayasikia ni masuala Mtambuka. Tangu awamu ya kwanza utasikia ujenzi wa barabara ile, kiwanda kile, reli ile, daraja lile, uchumi unakua, tumeongeza fedha za manunuzi ya dawa, ruzuku ya mbolea nk.
Tumeyasikia hayo tangu na tangu.
Hayo si ya muhimu kama masuala mazito yanayohusu uhai na hadhi ya binadamu, haki za binadamu, uhuru na amani. Nk.
Mjini Damascu, Syria kuna ma'flyovers' madaraja na miundombinu mingi ya kisasa, lakini raia wa Syria wanakimbia nchi yao na kwenda kuishi kama wakimbizi kwenye nchi za watu.
Kama viongozi wetu wataendelea kutumia ujenzi wa 'vitu' kama kisingizio cha kuhalalisha falsafa mbovu ya utawala wa awamu ya tano, watatupoteza.

Janga lingine kubwa ni la viongozi wa ngazi za chini, wakuu wa wilaya, mikoa na wenzao, ambao wameamua kwa makusudi kuwa manyapara wa wananchi. Sijalisikia likigusiwa, isipokuwa mchangiaji mmoja alilisema kwa uchache.
Rai, yangu kwa waandaaji wa Kongamano, ikiwa kuna mpango wa kuandaa Kongamano lingine, ni vema wachangiaji wakuu wagusie masuala ya kifalsafa, tafakuri, fikara, tathmini nk. Sio kufanya kampeni.

Halafu la mwisho, Tumuache Nyerere apumzike. Hili jambo la kumlinganisha Magufuli na Nyerere, linaweza kutuletea ukame ambao haujawahi kutokea. Laana zingine tunajitakia wenyewe.View attachment 918223
Rais anapostahili kusifiwa lazima asifiwe. Watu wengine waache ugonjwa wa kupinga kila kitu Hautawafikisha mbali.
 
Sasa cha ajabu huyo mtu anaizungumzia Shahada utadhani alianzia Shahada, wakati alianzia Diploma huko Iringa - Mkwawa ila kwa kawaida watu wa mikoani ndo hua walivyo Udsm wanaonaga ni sehemu moja ya hatari sana yani wanasomaga utafikiri wametumwa na kijiji hivyo wakifika Udsm wanajiona sijui wamefika wapi..
 
Kila siku anasema yaleyale kama unafatilia utagundua hotuba yake hiyo kila siku anizungumza .watumishi hewa. Bodi ya mikopo.strigls .barabara na reli.safari xa nje na posho hana lingine
Huyu siyo mtu wa kusikilizwa na watu wenye akili zao elite community for that matter. Sawana enzi zile maprofesa wa Makerere kumsikiliza Idd Amin
 
KONGAMANO LA KUSIFU NA KUABUDU.mwenye mchango wa mana pale ni huyo padre tu.maprofesa wote sifuri tu hadi kinyaa
Sawa ni una uhuru wa kusema utakalo,mbona mdomo huulipii?Sasa ulitaka wamsulubu Rais eh,na kwa lipi hasa,hebu tuambie mwenzetu tuchangie.
 
Kila siku anasema yaleyale kama unafatilia utagundua hotuba yake hiyo kila siku anizungumza .watumishi hewa. Bodi ya mikopo.strigls .barabara na reli.safari xa nje na posho hana lingine
alipopewa nafasi ya kuzungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha mzee mengi aliyasema yaleyale ya jana, akimwapisha hata mjumbe wa nyumba 10 huyasema yaleyale. huyu mtu hana vision anayoisimamia? mana kama una vision yenyewe ndiyo inazungumza sio hata ukikuta watto wa sm unawambia madaraj sijui nn? inakera
 
Wasomi muda wote wanatakiwa wazungumze mstakabali wa Taifa hasa mambo ya Uchumi na usalama haiitaji kongamano ndio wazungumze sasa ukiona muda wote wapo kimya usitegemee anaewateua akiwaita wazungumze kuna la maana litazungumzwa ni kusifia tuu ili kutafuta fursa basi....
 
Yote ulyoyataja nilyategemea yangetokea tu. TANZANIA WASOMI WENGI NI WAKUJIPENDEKEZA, HAWAJIAMINI.

ukijaribu linganishaa na kongamano la wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda. Apo utagundua kuwa elimu yetu inapumbaza hata uwezo wa kufikiria wa watu. Wafanyabiashara ambao hata chuo hawakufika waliweza jieleza vizur na kwa kujiamini.

Alafu UChuMi unakuwa controlled na Wafanyabiashara sio wasomi. Apo wamepoteza muda tu. Wenyewe wanaongelea theories..wafanyabiashara wanaongelea practical.
Kwa hilo nime kukubali wafanya biashara walifanya vizuri sana kwenye kongamano lao.
 
Hivi kuna matumizi mabaya kama kurudia uchaguzi kwa mtu yule yule kwa nafasi ile ile??

Hivi kurudia uchaguzi wa "kizembe" namna ile na kutengeneza Katiba mpya ya nchi, ni kipindi cha muhimu zaidi nchi hii kwa hivi sasa??

Hivi inawezekanaje watu wengi wa nchi hii tukataka Katiba mpya, lakini Jiwe akagoma kutuletea Katiba mpya na uamuzi wa Jiwe ndiyo uonekane ni sahihi

Lakini kwa kuwa ONE MAN SHOW imefanya kazi kwa Mara nyingine tena na kusema kuwa serikali yake haitatoa kipaumbele kwa Katiba mpya, inabidi tukubali tu anachosema Mfalme wetu
Hili ni tabia ya tawala zote zinazo tawala kimabavu huwa hawapendi kugusiwa swala la katiba kabisa.
 
Ulimsikiliza Mukandara vizuri?na kisomi?
Hugo ndiye ulikuwa sifuri kabisa yeye alichofanya ni kuorodhesha mambo yaliyo kwisha fanyika, badala ya kuonyesha mbinu zipi zitumike ili kuinua uchumi.
 
Wateule wa mheshimiwa wamejiandalia kongamano, kisha wakatumia jukwaa kumsifu aliyewapa kula!

Nilitegemea wakazungumzie habari za nchi kwa kina, kwa data, kwa nguvu ya hoja na ushahidi wa wazi, lakini wakaishia kumzungumzia Magufuli utadhani Magufuli ndiyo nchi yenyewe!,

Maprofesa wetu badala ya kudiscus ideas, wakaanza kudiscuss kuhusu Mtu (Magufuli), eti kafanya hili, kafanya lile, bila Data, Bila Critical analysis yoyote!

Kwa mfano unaposema Mheshimiwa kanunua ndege, tuambie kwa takwimu mpaka sasa hivi ndege zilizokweisha nunuliwa zimeiingizia nchi kiasi gani na matumizi yamekuwa kiasi gani na Je Tusingenunua hizo ndege pesa tukaziingiza mathalani sehemu nyingine kama vile elimu, barabara utofauti katika maisha ya Mtanzania ungekuwaje?

Au Je Mathalani tungewekeza katika chuma chetu cha liganga na mchuchuma kisha tukajengea hiyo reli kwa mataaluma kwa mataaluma ya chuma chetu wenyewe tungesevu kiasi gani?. Haya ndiyo mambo nilitegemea maprofesa watu wamwambie mheshimiwa!

Ndiyo maana Tundu Lissu akatumia maneno makali ya "Professorial Rubbish" kwa baadhi ya kazi za Maprofesa. Wanashindwa kusimama na kutoa mawazo kwa uhuru na kwa nguvu ya hoja wanabaki kuimba sifa tu kama Polepole na Lusinde

Jana kazi ya Maprofesa watoa mada hata Msemaji wa CCM Polepole haoni ndani kwa jinsi walivyokuwa wakimwaga misifa na kuimba mapambio mbele ya mheshimiwa!. AIBU!!
Tens kibaya zaidi tukio lenyewe lilikuwa likirushwa hewani moja kwa moja najua kwa nchi jirani walioshuhudia walishangaa sana kuona aina ya wasomi tulio nao inasikitisha sana.
 
mm naungana na mh rais hakuna haja ya kuwa na wabunge ambao hawajui kazi yao ni nn ni bora wafutwe bunge lote tubaki na rais na wakuu wa wilaya wanatosha.hzo fedha tutumie kwnye maendeleo
Tunataka rais wa watu na siyo rais wa vitu!!!
 
Kongamano lile lilikua ni kujadili hali ya uchumi ndani ya miaka mitatu ya Magufuli
Maprofessor wote waliainisha njia walizopitia katika kuandika mada zao
Chaso andaeni kongamano lenu mana mlitegemea Rais atukanwe haikua
Huo nao ndio uwezo wako wakufikiri ulipofikia hongera sana kabombe.
 
Kwa hilo nime kukubali wafanya biashara walifanya vizuri sana kwenye kongamano lao.
Wafanya biashara hawahitaji uteuzi ndio maana hawakuweka unafiki.Maprofesa pale ndio ilikua ni fursa adhimu ya kutafutia uteuzi.
 
Back
Top Bottom