Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Amesema hawezi kutenga fedha kwa ajili ya katiba mpya na kwamba ni kula pesa bure ambazo angezitumia kujenga standard gauge railway line. Kwa kauli hii na kama angekuwa na uwezo angefutilia bunge la Tanzania ili apate pesa za kujenga standard gauge!!!
Amesahau kwba yeye alipata uwaziri baada ya kuwa mbunge
 
Hakuna cha katiba mpya wala ya zamani.
Iliyopo inatosha Sana,kwa maana hakuna kitakachobadilika!! Na hizo chaguzi ndogo zinazorudiwa no sababu ya wanaohama chama sasa uwaulize wananchi wanaoenda kumchagua tena huyo huyo wana machungu na kodi zetu au la??Kama ndio basi Hakuna haja ya kumchagua if no basi wamchague mwingine maana tunaoumizwa ni sisi tunaokatwa kodi huku maendeleo ni ya kuvuta na kamba
 
Amesema hawezi kutenga fedha kwa ajili ya katiba mpya na kwamba ni kula pesa bure ambazo angezitumia kujenga standard gauge railway line. Kwa kauli hii na kama angekuwa na uwezo angefutilia bunge la Tanzania ili apate pesa za kujenga standard gauge!!!
ZILIZOTUMIKA KWENYE UCHAGUZI WA BUNGE HAZIONI
 
Hakuna dikteta anayependa kuweka misingi imara ya kiuongozi mahala popote duniani, kutegemea kupata katiba imara inayozingatia misingi ya usawa kati ya mtawala na mtawaliwa kwa huruma ya Rais dikteta ni sawa na kuchoma mahindi kwa kutumia mwanga wa mbalawezi huku ukiwa na matarajio chanya ya jambo hilo.

Madikteta hutengeneza katiba zenye kulinda na kudumisha madaraka, hivyo kutengeneza katiba mpya inayobeba matarajio ya wananchi ni kujipiga kitanzi kwa dikteta husika

Madikteta hupenda sifa binafsi ndio maana utasikia 'nafanya' 'nimefanya' 'nchi yangu' n.k, lakini ukweli hakuna dikteta hupenda sifa ziende kwa mwingine zaidi yake, na wale ambao huwapinga kwa nianjema/mbaya hukiona cha mtema kuni

Madikteta huwaaminisha watu kuwa katiba bora siyo msingi wa maendeleo ikiwa wanaozisimamia hizo katiba watakuwa wabaya, lakini msingi wa yote haya huyafanya kwa lengo moja tu, nalo ni kulinda na kudumisha madaraka na si kinyume chake
 
Hakuna cha katiba mpya wala ya zamani.
Iliyopo inatosha Sana,kwa maana hakuna kitakachobadilika!! Na hizo chaguzi ndogo zinazorudiwa no sababu ya wanaohama chama sasa uwaulize wananchi wanaoenda kumchagua tena huyo huyo wana machungu na kodi zetu au la??Kama ndio basi Hakuna haja ya kumchagua if no basi wamchague mwingine maana tunaoumizwa ni sisi tunaokatwa kodi huku maendeleo ni ya kuvuta na kamba
Unatakiwa utambue kwamba Wananchi huwa hawawachagui hao makahaba wa kisiasa. huwa wanapitishwa Na polisi na tume.
 
Nimekuwa namuangalia Rais akiwa akijadili hoja mbalimbali zilizozungumzwa na wana kongamano tofauti pale Mlimani walipokuwa wanajadili hali ya uchumi nchini alipofika hoja inayohusu Katiba hali ilibadilika kabisa na inaonyeshwa hapendezwi kabisa kabisa na wale wasomi ambao bado haelewi mikakati ya awamu ya tano inataka nini na misimamo yake ni ipi huku wao bado wakipenda kujadili mambo ambayo alishayatolea maelezo huko nyuma.

Nakumbuka alishasema kuhusu Katiba kuwa sio kipaumbele chake wala hakuna nadi katika kampeni.

Kiukweli mtazomo wake kimwili tu unaonyesha kuwa hapendi wanaotaka kucheze pesa za umma kwa vitu ambavyo Rais hajavipa kipaumbele kabisa.
Aisee..Kichaa ni Kichaa tu.
 
Sasa cha ajabu cha huyu mtu asie na kumbukumbu ni kwamba SGR, Ndege alizonununua, Uwanja wa ndege Chato, vyote hakuvinadi iweje afanye vile visivyonadiwa hawezi leta katiba sababu itamtoa madarakani
 
Huyu wa pili ndo haeleweki kbsaa...wanajidharirisha mbele za wanafunzi wao.
Anasema taa kumulika barabarani pengine labda ni sola inapotea.

Kisha anajikita ktk sigilas gorge.
Wanazuoni wetu asilimia kubwa ni mtihani
 
kwa afrika katiba in vichwa vya viongozi na sio katiba za wananchi.Leo nimeamini wasomi wetu in mizigo.yaani wanashangilia kitendo cha rais kukataa katiba mpya
 
Basi itabidi tuhairishe kikao kijacho cha bunge ili kubana matumizi nadhani tutakuwa tumeokoa pesa mingi sana
 
mm naungana na mh rais hakuna haja ya kuwa na wabunge ambao hawajui kazi yao ni nn ni bora wafutwe bunge lote tubaki na rais na wakuu wa wilaya wanatosha.hzo fedha tutumie kwnye maendeleo
 
Back
Top Bottom