Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Nimemsikia Rais Magufuli akisema serikali Ina akiba ya Dola za Kimarekani Bilioni 5 zinazoweza kuendesha nchi Kwa takriban miezi sita huku mfanyabiashara MO Dewji akimiliki utajiri wa Dola za Kimarekani Bilioni 2 kwa mujibu wa Jariba la Forbes ambao ni karibia nusu ya akiba iliyo nayo serikali!

My take : Wafanyabiashara siyo wa kubezwa maana wameshikilia sehemu kubwa ya uchumi wa nchi ,pia viongozi wetu wawe Na hekma siyo kila data ya kuweka hadharani huenda zikatumiwa vibaya Na maadui.
 
Hizo dollar billion 5 ni akiba au ni fedha za kigeni zilizoko mfukoni mwa serekali??!
 
Sitaweza kuhudhuria kongamano la uchumi linalofanyika UDSM, hatahivyo maoni yangu ambayo ningeyatoa kuhusu ukuaji wa uchumi kama ningeweza kuhudhuria kongamano ni kama ifuatavyo:

"Uchumi unakua kwa kasi kubwa sana kiasi kwamba mabenki na makampuni yanafunga biashara, yanapunguza wafanyakazi na kufiliska kwa kasi kubwa kwa sababu benki hizo na makampuni hayo yameshindwa kuhimili kasi kubwa sana ya ukuaji wa uchumi au kwa maneno mengine yameshindwa kwenda na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi. Kwakweli tunayo kila sababu ya kujivunia kasi ya kuaji wa uchumi"
mkuu mbona kuna mabenki yanaongeza matawi na kuongeza wafanyakazi kila siku?
 
Aliposema serikali ina bil 5,hakuhesabu na za Mo Bavicha mmekuaje siku hizi?.
Chadema akaunti yao wana balance ya milioni 37, Lowassa benki ana bil 37 sio sahihi kusema utajiri wa Chadema wanadaiwa na Lowassa mara 1000
 
bunge lilipewa fursa ya kutunga kabita likaivuruga mwishowe pesa zilipotea bure bila kuunda katiba mpya,,,,ndio maana bunge linazahaulika
 
unapotosha makusudi kw faida ya nani??mbona umetumia hisia zaidi kuliko ubongo ku synthesis hiyo kauli nyepesi???nawachukia wanaopongeza kila kitu na wanaoponda kila kitu,hiyo kauli ya mheshimiwa sidhani kama inauhusiano na kufuta bunge,hangaisha ubongo kuchanganua mambo
Umeelewaje aliposema vyama vya siasa vinatuchelewesha??
 
Kongamano la Tathmini ya hali ya kiuchumi na kisiasa likawa kongamano la kumsifia Magufuli. Ni mpango ulioandaliwa kabla, ili kumjengea Rais Magufuli imani kwa wananchi, imani inayopotea kila kukicha kutokana na matendo ya hovyo ya serikali ya awamu ya tano.
Sikusikia mambo mazito yakigusiwa, matukio ya utekaji, upoteaji wa watu yenye viashiria vya uhusika wa vyombo vya usalama, ongeza na jaribio la mauaji ya Mh. Tundu Lissu.

Mauaji ya raia ndani na nje ya vituo vya polisi.

'Uchuro' wa tume ya uchaguzi iliyogeuzwa kuwa idara ya chama cha mapinduzi.
Utumwa wa bunge kwa serikali.
Serikali kuingilia kazi za mahakama.
Kauli za Rais, zinazofifisha hadhi ya taasisi ya Urais, kama ile ya kuwapiga mashangazi wa wabunge wa kusini, kauli ya kupinga uzazi wa mpango, kauli za kuchochea chuki kati ya jeshi la polisi na raia wenye mawazo kinzani hususani viongozi wa vyama vya upinzani.

Hayo ni baadhi ya hoja nzito zilizopaswa kujadiliwa.

Maprofesa wetu, hasa Kitila Mkumbo na Kabudi Paramaganda, waliamua kwa makusudi, au pengine ndio ulikuwa mpango, kugeuza kongamano na kuwa mkutano wa kampeni. Mambo mengi waliyogusia ni mambo Mtambuka, wajibu wa serikali.
Ingependeza kusikia mjadala wa kifalsafa zaidi kama alivyofanya Profesa Mukandala. Hayo ya mambo ya mipango ya serikali kila mwaka tunayasikia ni masuala Mtambuka. Tangu awamu ya kwanza utasikia ujenzi wa barabara ile, kiwanda kile, reli ile, daraja lile, uchumi unakua, tumeongeza fedha za manunuzi ya dawa, ruzuku ya mbolea nk.
Tumeyasikia hayo tangu na tangu.
Hayo si ya muhimu kama masuala mazito yanayohusu uhai na hadhi ya binadamu, haki za binadamu, uhuru na amani. Nk.
Mjini Damascu, Syria kuna ma'flyovers' madaraja na miundombinu mingi ya kisasa, lakini raia wa Syria wanakimbia nchi yao na kwenda kuishi kama wakimbizi kwenye nchi za watu.
Kama viongozi wetu wataendelea kutumia ujenzi wa 'vitu' kama kisingizio cha kuhalalisha falsafa mbovu ya utawala wa awamu ya tano, watatupoteza.

Janga lingine kubwa ni la viongozi wa ngazi za chini, wakuu wa wilaya, mikoa na wenzao, ambao wameamua kwa makusudi kuwa manyapara wa wananchi. Sijalisikia likigusiwa, isipokuwa mchangiaji mmoja alilisema kwa uchache.
Rai, yangu kwa waandaaji wa Kongamano, ikiwa kuna mpango wa kuandaa Kongamano lingine, ni vema wachangiaji wakuu wagusie masuala ya kifalsafa, tafakuri, fikara, tathmini nk. Sio kufanya kampeni.

Halafu la mwisho, Tumuache Nyerere apumzike. Hili jambo la kumlinganisha Magufuli na Nyerere, linaweza kutuletea ukame ambao haujawahi kutokea. Laana zingine tunajitakia wenyewe.
FB_IMG_1541093672196.jpeg
 
Kwa mazingira ya sasa hapakuwa na sababu ya kuwa na upuuzi kama ule maana ilijulikana kuwa hakuna mtu wa kumkosoa Jiwe hadharani. It was a wastage of time! haya tuliyaona sana wakati wa Idd Amin, maiti zinaelea mto Kagera lakini akina Musiba wa Uganda wanaimba mapambio! Nyie watoto ndio hamjui haya mambo!
 
ilinishangaza sna kwa maprofesa wetu kuwa shallow namna ile siju nikujipendekeza?mtu aliyeongea cha maana ni yule padre aliyesema hatuna tume huru.maprofesa wetu wameshndwa hata kuona hali ya usalama hali ya uchumi bei ya mazao imeshuka huku bidhaa ya dukani bei juu.very sad
 
Andaa na wewe la kumsifia Lisu na Mbowe!
 
Back
Top Bottom