Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Punguzeni Matumaini hewa

Kenya wamekuwa Na Katiba Mpya lakin kilio chao ni kile kile
Kwahiyo unaweza kulinganisha Kenya na Tanzania? Hizi ni nchi.mbili tofauti tunaweza kufika mbali zaidi kuliko Kenya. Hivi yule mwanafunzi aliye Sema tunahitaji kuwa na kina Magufuli wengi mlimuelewa? Kwamba yes probably our president he is doing good ila hayo anayoyafanya tusipoyarasimisha akiondoka tutarudi kulekule. Au nyie m naamini Rais wetu ni Mungu kwa.mba at a dumu milele?
 
Sasa kongamano ni la uchumi halafu lijadili mambo ya ulinzi na usalama wapi na wapi. Maswala ya usalama yana vyombo vyake si mambo ya kuitishia makongamano ndo mana kuna kamati za ulinzi na usalama ngazi ya kijiji, kata, Wilaya, Mkoa n.k.
Na bila kupepesa macho na kuwek unafiki pembeni Dr JPM kafanya mengi mazuri na anastahili pongezi. Haya anayofanya yalitakiwa yaanze muda mrefu kujenga nchi wenzetu tuliokuwa nao wakati tunapata uhuru walichukua hatua za kujenga uchumi sasa wanaitwa nchi zinazoendelea, wakati sisi bado tupo kwenye nchi maskini pamoja na kuwa na raslimali nyingi.
Badala ya kubuni mbinu za kuzalisha tunabuni mipasho, fitina, unafiki, figisufigisu tu. Kulalamika lalamika, unakuta dume zima linapiga kelele kijiwe cha kahawa Rais hafanyi lolote, mara uchumi mbovu wakati mkewe anapambana peke yake kuinua uchumi wa familia kwa biashara ndogo ndogo na halina msaada kwake zaidi ya kuomba hata hela ya kahawa.
Tuache ujuaji wa kwenye mitandao ya kijamii, tutumie muda kuzalisha, na tuache kulalamika, tushauri.
Yanayofanywa sasa na Serikali ya awamu ya tano hata km sisi hatutafaidi lakini kizazi chetu kitanufaika, tuungane kwa pamoja kujenga Taifa letu
 
Nilipenda Prof. Shivji aliposema kitu pekee anachojivunia kwa Magufuli mpaka leo ni hili kongamano la leo la kuwasikiliza watu!! Na akasisitiza ili maisha yetu yabadilike kilimo ndio cha mkazo, kwa mtazamo wake hivyo viwanda ni porojo za kisiasa tu.
 
Maprof,dk wako pale kusifia ili wapate ajira,hii awamu ya hovyohovyo sana
 
mm naungana na mh rais hakuna haja ya kuwa na wabunge ambao hawajui kazi yao ni nn ni bora wafutwe bunge lote tubaki na rais na wakuu wa wilaya wanatosha.hzo fedha tutumie kwnye maendeleo

Lakini hapo umeona Rais kwa kusema hivyo anajua majukumu yake
 
unapotosha makusudi kw faida ya nani??mbona umetumia hisia zaidi kuliko ubongo ku synthesis hiyo kauli nyepesi???nawachukia wanaopongeza kila kitu na wanaoponda kila kitu,hiyo kauli ya mheshimiwa sidhani kama inauhusiano na kufuta bunge,hangaisha ubongo kuchanganua mambo

Boss; uwe unasoma posts angalau mara mbili kabla hujaitolea maoni. Ulichokiandika na alichokiandika huyo unaemjibu ni mashariki na magharibi.
 
Kuna Mambo Mengine Yanayoendelea Nchini Inakubidi Ucheke weee, Kisha Baada Ya Hapo Ushike Tama!
 
Sijui waliwaza nini kufanya kile walichokifanya. Lakini tukumbuke hata shetani hutamani kutenda mema lakini anajikuta badala ya kutenda jema arudikulekule
 
Ulitegemea nini kwani mkuu,what did you expecti?.sku nyengine ujiandae kisaikolojia
 
Natoa ono moja ambalo naliona juu ya JPM na mchakato wa Katiba Mpya! JPM sio kama hataki kabisa Katiba mpya lah-hasha ila anaitka lakini haitaki ile Pendekezwa anaitaka Rasimu ya Pili japo Rasimu ya Pili inampa changamoto sehemu moja tu ni juu ya Muungano wa Serikali tatu hilo litamfanya asiurudishe mchakato wote.
 
JPM kapangua hoja ya Katiba kibabe sana. Kwa mtazamo wake ni kama sheria za kawaida ,kwamba likitokea hitaji ni simple una badili kipengele via Mbunge. Kwa mtazamo wangu hana dhamira nzuri atafanya apendavyo kwa matakwa yake , kalisifia sana bunge na uongozi wake! Wanafanya kazi nzuri!!!Tufikiri mkakati kudai Katiba na isiwe hisani ya mtu.
 
Back
Top Bottom