Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

kwa afrika katiba in vichwa vya viongozi na sio katiba za wananchi.Leo nimeamini wasomi wetu in mizigo.yaani wanashangilia kitendo cha rais kukataa katiba mpya
sasa ulitaka wafanyeje wakati walikuwa kwenye mazingira ya kushangilia hivi hujui kuzimu nguvu za mungu huitwa nguvu za g........za
 
Mbowe ameruhusu hiyo katiba mpya?
Mbowe siyo Rais, na hana impact ya maisha ya watanzania,kiuchumi,Elimu,Afya,Siasa wala ulinzi.
Impact ya Mbowe ipo kisiasa na tena ndani ya chama chake tu,nje ya chama chake hana impact.
Sasa sijui unamtakia nini Mbowe,tafuta mume kwingine,Mbowe ana mke tayari hawezi kukuoa.
 
Yaani atafute pesa kwa jasho vile halafu watu wachache waende kula hhela za bure NOOO Waay!
Kwani ni hela zake? Ametoka nazo kwao? Amepewa na wazazi wake au kodi za watu?
 
Niko na bibi angu hapa nimemwonyesha comment yako kaangalia jina lako kanipa maana yake kikwetu naogopa hata kuandika nkihisi bibi kanitukana mimi
Wasomi wa nchi hii ni shida wanashindwa kujadili uhalisia wa hali ya uchumi badala yake wana kwenda kumsifia mtu ,yani unadhani Taifa zima halina wasomi
 
tusiwapangie cha kuongea kwani kila MTU ana namna take ya kutafuta fursa
Lengo la kongamano lilikuwa kujadili changamoto na jinsiya kutatua, kuonyesha tuko wapi na tunaelekea wapi changamoto tunazopitia tutashinda vipi
 
Nilifuatilia lile kongamano (siyo mjadala ule) kwa kweli nilishangaa kweli, Yaani Waandaaji wanawaleta Wateule wa Serikali ya awamu ya tano kuongoza "mjadala" wa kujadili hali ya kisiasa ya serikali ya awamu yao ambayo wao ni wateule wa serikali hiyo hiyo halafu eti wanaita Mdahalo!. Absurd

Hakukuwa na neutrality yoyote ya kisomi, Wazungumzaji zaidi ya asilimi 80 ni wateule wa serikali hiyohiyo ya Magufuli, Kwa mfano
Kitila ni mteule wa Magufuli, Kabudi ni Mteule wa Magufuli, Mkandala ni Mteule wa Magufuli halafu mwisho akaja Magufuli mwenyewe!. Ni dhahiri huu siyo mjadala wa Kisomi wenye hadhi ya mijadala ya kisomi, Bali ni Kampeni ya waziwazi kabla ya muda wa kampeni.


Katika kongamano hilo la Serikali sijasikia substance haswa ya ni wapi tulipotoka na ni wapi tunapokwenda, Sikusikia wakizungumzia hali ya Usalama wa wananchi, suala la Kupotea kwa Ben Saanane, Suala la Kupotea kwa mwandishi Azory Gwanda, Suala la Kupigwa risasi Tundu Lissu, Suala la Kutekwa kwa Mo, na haya yamefanyika walioyafanya hawajatiwa nguvuni na kwa kweli ni kama hakuna utashi wa serikali kuyatatua. Nilitegemea Waziri wa Katiba na Sheria ayazungumze haya badala ya kusimama katika podium na kuimba sifa tu, kiufupi ni aibu kwanza binadamu kusimama na kuanza kuimba sifa kwa binadamu mwenzio utafikiri yeye ni Mungu

Sijasikia wakizungumzia maslahi ya wafanyakazi, nyongeza za kila mwaka kwa mujibu wa sheria, sijasikia wakizungumzia kulipa malimbikizo ya wafanyakazi ambayo wanaidai serikali kutokana na serikali kusitisha nyongeza hizo ili kupisha zoezi la uhakiki, sijsikia wakizungumza habari za wafanyakzi kupandishwa madaraja kama sheria inavyosema, Hawakutoa Statistics zozote, zaidi ya kutamka kwa maneno matupu kuwa wamefanya hili na lile, kiukweli kabisa mjadala wa kisomi hauwi hivi, labda kama walitaka kuwafikia malaymen, lakini wajanja tumeng'amua, ni kongamano la kisiasa siyo la kisomi!

Hoja ya Katiba mpya nayo wameijibu kisiasa, kuanzia kwa Mkandala mwenyewe na Magufuli Mwenyewe, Huwezi kuweka kapuni mjadala wa katiba mpya eti kwa sababu miaka minne tangu rasimu ya Warioba itoke imepita!. Kupita kwa miaka minne kunazuia vipi uhitaji wa Katiba mpya?, Nani alisema kuwa kila mwaka unaopita katiba au rasimu yake inapaswa kubadirishwa?. Mbona tuna Katiba hii ya sasa na mara ya mwisho kuifanyia mabadiriko ni miaka kadhaa iliyopita mbona tunaenda nayo hiyohiyo?.
Suala la Katiba mpya haliepukiki, Magufuli anaweza kulichelewesha tu lakini Watanzania tutaendelea kuidai katiba mpya iliyo bora, hii ya sasa imepitwa na wakati na inatuchelewesha kuleta maendeleo tunayoyataka. Taifa lilishafikia muafaka katika suala hili kuwa katiba ya sasa haitutoshi.


Nimesikia hoja ya Kupambana na Ufisadi na rushwa lakini wakati huohuo shilingi Trilion 1.5 mahesabu yake hayakuonekana katika vitabu vya CAG, CAG alilizungumza hili, akataka wabunge waiulize serikali, na mpaka sasa serikali haijatoa majibu ya kuridhisha, katika mazingira kama haya utasemaje tunapambana na ufisadi kwa dhati?.
Hoja ya rushwa, wateule wa Magufuli pale kwenye kongamano wanasema kuwa serikali hii inapambana na rushwa, lakini ambacho hawajatuleza ni kwamba kuna vashiria vya waziwazi ya rushwa katika siasa katika nchi hii, Video iliyomrekodi DC Mnyeti akitoa Rushwa iko wazi, kila mtu ameiona lakini badala ya kufikishwa katika vyombo vya sheria ajibu mashitaka ya rushwa, amepandishwa cheo. Katika mazingira kama haya utasemaje unapambana kwa dhati na rushwa?. Ukiachilia mbali hilo hawa wanaojiuzulu katika vyama vyao na kisha kupewa teuzi kupitia katika chama tawala kugombea bila hata ya kuwahusisha wanachama wengine wa CCM kama siyo rushwa ya kisiasa kutafutwa uungwaji mkono ni nini?


Hali ya utawala bora, na double standard katika maamuzi, Tumefukuza wenye vyeti feki lakini Bashite tunamwambia chapa kazi. Tunakamata watu kwa makosa ya kiuchumi lakini kuna mkuu wa mkoa anaagiza makontena kinyume cha sheria, anaachwa ofisini badala ya kumwajibisha ili iwe mfano kwa wengine. Tunawavunjia watu nyumba katika sehemu moja ya nchi lakini katika sehemu nyingine ya nchi hatuvunji zao kwa sababu za kisiasa

Sijasikia mathalani wakizungumza suala la ajira kwa vijana, ni ajira ngapi wamezitengeneza ndani ya miaka mitatu ya utawala wao, Vijana maelfu kwa malaki wanahitimu masomo yao katika ngazi mbalimbali za elimu, hawana ajira, hawana mitaji, tueleze serikali imefanya nini kutatua suala hili, haya ndiyo mambo niliyotegemea kuyasikia

Kiufupi, lile kongamano kwa mtazmao wangu limefeli kujibu maswali mengi ambayo wananchi wanayo dhidi ya serikali hii. Na kiufupi walichozungumza jana wateule wa Magufuli (Maana ni kama wamejiandalia kongamano la kumsifu aliyewateua) ni kumwaga sifa tu kwa aliyewateua!

Niwakumbushe tu, Haitokuwa Mwanzo wala Mwisho kwa kila mtawala kusifiwa, kuimbiwa vigelegele, kuchezewa ngoma n.k. Kwa Nyerere tuliimba sana, tena tukampa hadi Slogan ya Zidumu Fikra za Mwenyekiti, je zilidumu?, alipokuja Mzee Mwinyi naye tulimuimbia sana, Mkapa hivyohivyo na Kikwete naye tukamuimbia lakini yeye inaonekana hakupenda saana mambo ya kuabudiwa abudiwa. hata hivyo linapokuja suala la Wasomi, tena Chuo Kikuu chenye heshima kama cha Dar es salaam kuanza kuimba nyimbo za kipropaganda za kisiasa badala ya kuwa objective na kushusha Nondo kwelikweli juu ya hali halisi ya nchi na wananchi kwa ujumla, Chuo kikageuza ukumbi adhimu wa Nkrumah kama Altare ya kuimba sifa kwa mtawala, kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana. Chuo kimegeuzwa kama Ofisi Ndogo ya Uenezi hapo Mtaa wa Lumumba!!

Kwa kweli waandaaji kongamano wamefeli katika kongamano lao maalum la "Kumsifu Mheshimiwa", Nilitegemea kongamano liwe na hadhi ya kisomi, Pawepo na mtifuano kwelikweli wa Fikra huru kutoka kwa nguli wenye mitizamo tofauti. Sasa wameenda kuleta wateule walewale wa serikali ileile kujitathmin unategemea nini?. Ni sawasawa na kumleta Haji Manara Nkrumah kuzungumzia utendaji kazi wa Uongozi wa Simba Sports Club ambayo na yeye ni sehemu yake, What do you expect?

Mimi namshauri tu Raisi Magufuli, akiwasikiliza Watuele wake akina Kitila, Kabudi na Mkandala anaweza kudhani mambo swaaaaafi (ofcourse lazima wamsifie maana kawapa “kula"), Lakini ukweli ni kwamba huku Site panawaka moto, tunataka majawabu ya ajira , tunataka majawabu ya utawala wa sheria katiba na haki, tunataka majawabu ya ulinzi na usalama wetu hatutaki kutekwa na kupotezwa, tunataka majawabu ya nyongeza za kisheria na haki za wafanyakazi, tunataka tume huru ya uchaguzi, tunataka kilimo chetu kiboreshwe, kipewe kipaumbele, wakulima tupate uhuru na nafasi ya kuuza mazao yetu nje ya nchi bila vikwazo, na tunataka katiba mpya iliyo bora. Hayo mambo hayakwepeki Mheshimiwa!
 
Kuna umuhimu wa kuwa na Kongamano lingine, hapo hapo lilipofanyikia hili. Washiriki wawe huru kuunga mkono au kuwa na maoni kinzani ya yale yaliyotolewa leo.
 
Siku hizi wasomi wetu wamekuwa wajinga eti, wanaanzisha kongamano la uchumi halafu mwisho wa siku linakuwa kongamano la kumsifia mtu. Waache huo upuuzi ,kama wanataka waanzishe tu kongamano la kumsifia mkuu, kwani shida ipo wapi.
 
Kwa Mara ya kwanza baada ya kupita miaka mingi tume shuhudia kongamano ambalo kwa kiasi Fulani lilikuwa na muelekeo wa kutupatia japo kwa kiwango muelekeo wetu wa kiuchumi na kisiasa na kiuchumi kama Taifa. Hilo lilikuwa ni wazo zuri ila kwa upande wangu binafsi niliona kama kuna baadhi ya dosari ambazo zilijitokeza, na hili nalisema kwa nia njema kabisa na nikiwa nimelenga kuwa siku za usoni kama itatokea fursa kama hizi basi tunaweza kufanya maboresho.

1: Niliona wasomi wetu wakikosa ujasiri wa kujieleza, ulikuwa ukiwatazama vizuri usoni walionyesha kama vile kuna jambo la kuongelea ila uoga uliwatala.

2: Baadhi yao hawakujikita kwenye uhalisia wa mada na badala yake walilenga kwenye kumsifia mh jambo ambalo najua kabisa kuwa hata mh hakufurahishwa nalo kwa sababu hawakulenga mkusaidia isipokuwa walilenga kujipendekeza.

3: Jambo jingine lilo jitokeza ni ubaguzi wa elimu kama kuna mtu aliskiliza kwa makini ilionyesha wazi kuwa kama umepata shahada yako mbali na UDSM basi hiyo shahada yako ni ya mashaka, nazungumzia vyuo vya kwetu Tz.

4: Kushiriki kwa mh kwenye kongamano kulipunguza uwazi wa washiriki kujieleza, nadhani kwa Mara nyingine kama itatokea napendekeza mh Rais asihudhurie ili wachangiaji japo kwa kiasi Fulani wapunguze ule uoga wa kuwa huru kujieleza.

5: Suala la katiba kama kweli na ndivyo ilivyo kuwa kiwango kikubwa kiu ya wa Tanzania nikupata katiba mpya , hili ni kwa nia njema kabisa ili mambo mazuri yanayo fanyika sasa yaweze kupewa ulinzi wa kikatiba , lakini kama tutakuwa na mawazo kuwa suala la katiba lina lenga kudhohofisha malengo ya watu Fulani kisiasa tutakuwa hatulitendei Taifa letu haki na wananchi kiujumla na hasa vizazi vitakavyo kuja baada yetu.

Pamoja na hayo pia kuna mambo mazuri ambayo niliyasikia kwa baadhi ya wachokoza mada, kuna professor yule aliye kuwa wa kwanza kuchangia alizungumzia swala la kilimo kinavyo weza kutengeneza upacha na maendeleo ya viwanda, akasema wazi kuwa hatuwezi kufikia maendeleo ya viwanda kama hatutawekeza zaidi kwenye kilimo, hili lilinifurahisha nakuonyesha ni jinsi gani alivyokuwa amejipanga kumsaidia Rais na Taifa lake kiujumla.

Kwa hilo siwezi kupita bila kumpatia kongole mh Rais kwa jinsi alivyo kuwa muwazi na kusema kuna fedha zipo zimetengwa kwa ajili ya kukopesha wale watakao taka kuwekeza kwenye kilimo, hili ni jambo jema, jambo ninalo liona hapa sasa ni serikali kutoa hamasa kwa wananchi ili wajiingize kwenye sekta ya kilimo kwa wingi zaidi.

Mwingine niliyeona amechangia vema ni yule mama Professor alijaribu kuonyesha ni kwa jinsi gani lugha ilivyo kuwa ni kiunganishi kizuri katika kukuza uchumi, ni jambo zuri kuwa tumebahatika kuwa na lugha inayo tuunganisha kama Taifa , lakini tukubali kuwa lugha za kutuunganisha kibiashara na mataifa mengine bado zitakuwa ni hizo lugha zilizo zoeleka, sasa basi jambo la muhimu kwetu ili tufanikiwe kukiingiza kiswahili ni kufanya jitihada ya kukiambukiza kwa mataifa mengine hasa tuki yalenga hayo mataifa makubwa ya ulaya na Asia.

Kwa upande huku kwetu afrika hakuna shaka kuwa dalili ni kubwa sana za kufanikiwa kwa hili.

Asanteni sana wadau .

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Un
Kwa Mara ya kwanza baada ya kupita miaka mingi tume shuhudia kongamano ambalo kwa kiasi Fulani lilikuwa na muelekeo wa kutupatia japo kwa kiwango muelekeo wetu wa kiuchumi na kisiasa na kiuchumi kama Taifa. Hilo lilikuwa ni wazo zuri ila kwa upande wangu binafsi niliona kama kuna baadhi ya dosari ambazo zilijitokeza, na hili nalisema kwa nia njema kabisa na nikiwa nimelenga kuwa siku za usoni kama itatokea fursa kama hizi basi tunaweza kufanya maboresho.
1: Niliona wasomi wetu wakikosa ujasiri wa kujieleza, ulikuwa ukiwatazama vizuri usoni walionyesha kama vile kuna jambo la kuongelea ila uoga uliwatala.
2: Baadhi yao hawakujikita kwenye uhalisia wa mada na badala yake walilenga kwenye kumsifia mh jambo ambalo najua kabisa kuwa hata mh hakufurahishwa nalo kwa sababu hawakulenga mkusaidia isipokuwa walilenga kujipendekeza.
3: Jambo jingine lilo jitokeza ni ubaguzi wa elimu kama kuna mtu aliskiliza kwa makini ilionyesha wazi kuwa kama umepata shahada yako mbali na UDSM basi hiyo shahada yako ni ya mashaka, nazungumzia vyuo vya kwetu Tz.
4: kushiriki kwa mh kwenye kongamano kulipunguza uwazi wa washiriki kujieleza, nadhani kwa Mara nyingine kama itatokea napendekeza mh Rais asihudhurie ili wachangiaji japo kwa kiasi Fulani wapunguze ule uoga wa kuwa huru kujieleza.
5: Swala la katiba kama kweli na ndivyo ilivyo kuwa kiwango kikubwa kiu ya wa Tanzania nikupata katiba mpya , hili ni kwa nia njema kabisa ili mambo mazuri yanayo fanyika sasa yaweze kupewa ulinzi wa kikatiba , lakini kama tutakuwa na mawazo kuwa swala la katiba lina lenga kudhohofisha malengo ya watu Fulani kisiasa tutakuwa hatulitendei Taifa letu haki na wananchi kiujumla na hasa vizazi vitakavyo kuja baada yetu.
Pamoja na hayo pia kuna mambo mazuri ambayo niliyasikia kwa baadhi ya wachokoza mada, kuna professor yule aliye kuwa wa kwanza kuchangia alizungumzia swala la kilimo kinavyo weza kutengeneza upacha na maendeleo ya viwanda, akasema wazi kuwa hatuwezi kufikia maendeleo ya viwanda kama hatutawekeza zaidi kwenye kilimo, hili lilinifurahisha nakuonyesha ni jinsi gani alivyokuwa amejipanga kumsaidia Rais na Taifa lake kiujumla.
Kwa hilo siwezi kupita bila kumpatia kongole mh Rais kwa jinsi alivyo kuwa muwazi na kusema kuna fedha zipo zimetengwa kwa ajili ya kukopesha wale watakao taka kuwekeza kwenye kilimo, hili ni jambo jema, jambo ninalo liona hapa sasa ni serikali kutoa hamasa kwa wananchi ili wajiingize kwenye sekta ya kilimo kwa wingi zaidi.
Mwingine niliyeona amechangia vema ni yule mama Professor alijaribu kuonyesha ni kwa jinsi gani lugha ilivyo kuwa ni kiunganishi kizuri katika kukuza uchumi, ni jambo zuri kuwa tumebahatika kuwa na lugha inayo tuunganisha kama Taifa , lakini tukubali kuwa lugha za kutuunganisha kibiashara na mataifa mengine bado zitakuwa ni hizo lugha zilizo zoeleka, sasa basi jambo la muhimu kwetu ili tufanikiwe kukiingiza kiswahili ni kufanya jitihada ya kukiambukiza kwa mataifa mengine hasa tuki yalenga hayo mataifa makubwa ya ulaya na Asia. Kwa upande huku kwetu afrika hakuna shaka kuwa dalili ni kubwa sana za kufanikiwa kwa hili.
Asanteni sana wadau .
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Unakywaje nxa Elimu kubwa na cheo kikubwa halafu bado hujiamini? Woga ni adui anaeishi ndani yako. Mifumo yetu ya Elimu na utangamano wetu wabkijamii unatusababishia kuzalisha watu waoga. Mungu tusaidie
 
Kama hawawezi kuwa huru kujieleza kwa kuwa tu rais yupo, hilo ni tatizo. Nadhani wanakuwa wanafiki ili kuvizia teuzi maana wanajua rais anapenda kuteua toka huko.

Ni vzr next time rais afanye kongamano na viongozi wa vyama vingine vya siasa, aambiwe ukweli utakaomuweka huru
 
Yote ulyoyataja nilyategemea yangetokea tu. TANZANIA WASOMI WENGI NI WAKUJIPENDEKEZA, HAWAJIAMINI.

ukijaribu linganishaa na kongamano la wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda. Apo utagundua kuwa elimu yetu inapumbaza hata uwezo wa kufikiria wa watu. Wafanyabiashara ambao hata chuo hawakufika waliweza jieleza vizur na kwa kujiamini.

Alafu UChuMi unakuwa controlled na Wafanyabiashara sio wasomi. Apo wamepoteza muda tu. Wenyewe wanaongelea theories..wafanyabiashara wanaongelea practical.
 
Hivi kuna matumizi mabaya kama kurudia uchaguzi kwa mtu yule yule kwa nafasi ile ile??

Hivi kurudia uchaguzi wa "kizembe" namna ile na kutengeneza Katiba mpya ya nchi, ni kipindi cha muhimu zaidi nchi hii kwa hivi sasa??

Hivi inawezekanaje watu wengi wa nchi hii tukataka Katiba mpya, lakini Jiwe akagoma kutuletea Katiba mpya na uamuzi wa Jiwe ndiyo uonekane ni sahihi

Lakini kwa kuwa ONE MAN SHOW imefanya kazi kwa Mara nyingine tena na kusema kuwa serikali yake haitatoa kipaumbele kwa Katiba mpya, inabidi tukubali tu anachosema Mfalme wetu
 
Back
Top Bottom