Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Huu ulikuwa mpango maalum wa kurudisha imani ya wananchi kwenye serikali yao ambayo imepoteza mvuto kwa kiwango kikubwa, hiyo ndio miujiza inayo fanywa hapa tz, TWAWEZA walipotoa utafiti unao lenga ukweli na hali halisi yule bwana alishambuliwa vibaya mno.
 
Ndugu yangu hao wote waliandaliwa kwajili yakujaribu kuwarejesha wananchi imani iliyokwishapotea. Lkn pia limegonga mwamba.
 
Huu ulikuwa mpango maalum wa kurudisha imani ya wananchi kwenye serikali yao ambayo imepoteza mvuto kwa kiwango kikubwa, hiyo ndio miujiza inayo fanywa hapa tz, TWAWEZA walipotoa utafiti unao lenga ukweli na hali halisi yule bwana alishambuliwa vibaya mno.

Wakaleta na watoto wa Sekondari ili na wenyewe washriki mdahalo , mtoto mmoja akasema eti tunahitaji Magufuli kama watatu hivi wafuatane ili tuweze kuendelea, kimoyomoyo nikasema Child you don't know what you are talking about! hahahaha
 
Jambo lolote likimuhusisha jiwe utengemee janga tu...sikuwa hata na muda wa kufuatilia nilijua upuuzi tu
 
Hayo ni mawazo yako mtoa post na hukatazwi kuyawaza.

Acha ukweli ujitenge na uongo.

Rais anafanya kazi kubwa na anastahili pongezi za dhati na wala si kana kwamba walikuwa wanamsifia.
 
So touching
Kongamano la Tathmini ya hali ya kiuchumi na kisiasa likawa kongamano la kumsifia Magufuli. Ni mpango ulioandaliwa kabla, ili kumjengea Rais Magufuli imani kwa wananchi, imani inayopotea kila kukicha kutokana na matendo ya hovyo ya serikali ya awamu ya tano.
Sikusikia mambo mazito yakigusiwa, matukio ya utekaji, upoteaji wa watu yenye viashiria vya uhusika wa vyombo vya usalama, ongeza na jaribio la mauaji ya Mh. Tundu Lissu.

Mauaji ya raia ndani na nje ya vituo vya polisi.

'Uchuro' wa tume ya uchaguzi iliyogeuzwa kuwa idara ya chama cha mapinduzi.
Utumwa wa bunge kwa serikali.
Serikali kuingilia kazi za mahakama.
Kauli za Rais, zinazofifisha hadhi ya taasisi ya Urais, kama ile ya kuwapiga mashangazi wa wabunge wa kusini, kauli ya kupinga uzazi wa mpango, kauli za kuchochea chuki kati ya jeshi la polisi na raia wenye mawazo kinzani hususani viongozi wa vyama vya upinzani.

Hayo ni baadhi ya hoja nzito zilizopaswa kujadiliwa.

Maprofesa wetu, hasa Kitila Mkumbo na Kabudi Paramaganda, waliamua kwa makusudi, au pengine ndio ulikuwa mpango, kugeuza kongamano na kuwa mkutano wa kampeni. Mambo mengi waliyogusia ni mambo Mtambuka, wajibu wa serikali.
Ingependeza kusikia mjadala wa kifalsafa zaidi kama alivyofanya Profesa Mukandala. Hayo ya mambo ya mipango ya serikali kila mwaka tunayasikia ni masuala Mtambuka. Tangu awamu ya kwanza utasikia ujenzi wa barabara ile, kiwanda kile, reli ile, daraja lile, uchumi unakua, tumeongeza fedha za manunuzi ya dawa, ruzuku ya mbolea nk.
Tumeyasikia hayo tangu na tangu.
Hayo si ya muhimu kama masuala mazito yanayohusu uhai na hadhi ya binadamu, haki za binadamu, uhuru na amani. Nk.
Mjini Damascu, Syria kuna ma'flyovers' madaraja na miundombinu mingi ya kisasa, lakini raia wa Syria wanakimbia nchi yao na kwenda kuishi kama wakimbizi kwenye nchi za watu.
Kama viongozi wetu wataendelea kutumia ujenzi wa 'vitu' kama kisingizio cha kuhalalisha falsafa mbovu ya utawala wa awamu ya tano, watatupoteza.

Janga lingine kubwa ni la viongozi wa ngazi za chini, wakuu wa wilaya, mikoa na wenzao, ambao wameamua kwa makusudi kuwa manyapara wa wananchi. Sijalisikia likigusiwa, isipokuwa mchangiaji mmoja alilisema kwa uchache.
Rai, yangu kwa waandaaji wa Kongamano, ikiwa kuna mpango wa kuandaa Kongamano lingine, ni vema wachangiaji wakuu wagusie masuala ya kifalsafa, tafakuri, fikara, tathmini nk. Sio kufanya kampeni.

Halafu la mwisho, Tumuache Nyerere apumzike. Hili jambo la kumlinganisha Magufuli na Nyerere, linaweza kutuletea ukame ambao haujawahi kutokea. Laana zingine tunajitakia wenyewe.View attachment 918223
 
jamani, Magufuli kajitahidi san, tumpe haki yake
Aliteuliwa kufanya nini? Je alichotakiwa kukifanya kimeshakamilika na amefanya ziada ya matarajio kustahili bonus ya sifa na pongezi? Just thinking aloud!
 
Kitu cha msingi katika kongamano lolote ni kumpa Rais idea za kuliokoa hili taifa,ukimsifia sana ata yeye atafahamu unamsifia, ila ukimpa nafasi ya upeo wako nini kifanyike katika lile analofanya ili mambo yawe bora lazima atashukuru ndani ya roho yake.Ukileta dharau hakika utapata tabu..sasa watu ni waoga wanaogopa kumpa mpango wanahisi ataikataa (Kitu ambacho si kweli).Mtu AKIKUSIFIA SANA inabidi UMCHUNGUZE hivyo hivyo Mtu AKIKUKASHIFU inabidi umchunguze
 
Kutumia jeshi kujenga ukuta Marerani ni kukiri kwamba kampuni au taasisi za kiraia za ujenzi zina kasoro hazifai. Solution sio kutumia jeshi, ni kurekebisha kasoro. Ili kulinda au kukuza ajira.
 
Kwa Mara ya kwanza baada ya kupita miaka mingi tume shuhudia kongamano ambalo kwa kiasi Fulani lilikuwa na muelekeo wa kutupatia japo kwa kiwango muelekeo wetu wa kiuchumi na kisiasa na kiuchumi kama Taifa. Hilo lilikuwa ni wazo zuri ila kwa upande wangu binafsi niliona kama kuna baadhi ya dosari ambazo zilijitokeza, na hili nalisema kwa nia njema kabisa na nikiwa nimelenga kuwa siku za usoni kama itatokea fursa kama hizi basi tunaweza kufanya maboresho.
1: Niliona wasomi wetu wakikosa ujasiri wa kujieleza, ulikuwa ukiwatazama vizuri usoni walionyesha kama vile kuna jambo la kuongelea ila uoga uliwatala.
2: Baadhi yao hawakujikita kwenye uhalisia wa mada na badala yake walilenga kwenye kumsifia mh jambo ambalo najua kabisa kuwa hata mh hakufurahishwa nalo kwa sababu hawakulenga mkusaidia isipokuwa walilenga kujipendekeza.
3: Jambo jingine lilo jitokeza ni ubaguzi wa elimu kama kuna mtu aliskiliza kwa makini ilionyesha wazi kuwa kama umepata shahada yako mbali na UDSM basi hiyo shahada yako ni ya mashaka, nazungumzia vyuo vya kwetu Tz.
4: kushiriki kwa mh kwenye kongamano kulipunguza uwazi wa washiriki kujieleza, nadhani kwa Mara nyingine kama itatokea napendekeza mh Rais asihudhurie ili wachangiaji japo kwa kiasi Fulani wapunguze ule uoga wa kuwa huru kujieleza.
5: Swala la katiba kama kweli na ndivyo ilivyo kuwa kiwango kikubwa kiu ya wa Tanzania nikupata katiba mpya , hili ni kwa nia njema kabisa ili mambo mazuri yanayo fanyika sasa yaweze kupewa ulinzi wa kikatiba , lakini kama tutakuwa na mawazo kuwa swala la katiba lina lenga kudhohofisha malengo ya watu Fulani kisiasa tutakuwa hatulitendei Taifa letu haki na wananchi kiujumla na hasa vizazi vitakavyo kuja baada yetu.
Pamoja na hayo pia kuna mambo mazuri ambayo niliyasikia kwa baadhi ya wachokoza mada, kuna professor yule aliye kuwa wa kwanza kuchangia alizungumzia swala la kilimo kinavyo weza kutengeneza upacha na maendeleo ya viwanda, akasema wazi kuwa hatuwezi kufikia maendeleo ya viwanda kama hatutawekeza zaidi kwenye kilimo, hili lilinifurahisha nakuonyesha ni jinsi gani alivyokuwa amejipanga kumsaidia Rais na Taifa lake kiujumla.
Kwa hilo siwezi kupita bila kumpatia kongole mh Rais kwa jinsi alivyo kuwa muwazi na kusema kuna fedha zipo zimetengwa kwa ajili ya kukopesha wale watakao taka kuwekeza kwenye kilimo, hili ni jambo jema, jambo ninalo liona hapa sasa ni serikali kutoa hamasa kwa wananchi ili wajiingize kwenye sekta ya kilimo kwa wingi zaidi.
Mwingine niliyeona amechangia vema ni yule mama Professor alijaribu kuonyesha ni kwa jinsi gani lugha ilivyo kuwa ni kiunganishi kizuri katika kukuza uchumi, ni jambo zuri kuwa tumebahatika kuwa na lugha inayo tuunganisha kama Taifa , lakini tukubali kuwa lugha za kutuunganisha kibiashara na mataifa mengine bado zitakuwa ni hizo lugha zilizo zoeleka, sasa basi jambo la muhimu kwetu ili tufanikiwe kukiingiza kiswahili ni kufanya jitihada ya kukiambukiza kwa mataifa mengine hasa tuki yalenga hayo mataifa makubwa ya ulaya na Asia. Kwa upande huku kwetu afrika hakuna shaka kuwa dalili ni kubwa sana za kufanikiwa kwa hili.
Asanteni sana wadau .
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
yale ndiyo yalikuwa malengo ya baraza lile la kahawa.
ona namna yule mwanafunzi alivyojipanga. ati anaulizia upatikanaji wa MAGUFULI kwamba hakukuwa na mtu aloandaliwa / succession planning ye kajuaje? kwamba asitokee mtu akagombea na kuharibu mipango ya MAGUFULI, hii imetokana na yale makelelee ya twende na membe 2020 hapo wiki iliyopita! anakwenda anasema waje MAGUFULI wengine watatu mbele. huyu ni amma anawandaa wananchi kisaikolojia au anawatisha washindani wake kisiasa
 
Kila siku anasema yaleyale kama unafatilia utagundua hotuba yake hiyo kila siku anizungumza .watumishi hewa. Bodi ya mikopo.strigls .barabara na reli.safari xa nje na posho hana lingine
Maigizo yamechina. Ulimwona Prof Kabundi, msanii wa makinikia akiwa na Prince Makonda waalivyokuwa wanashangilia kwa pamoja kutupwa kwa katiba mpya?
 
Ndicho tulichotarajia wengi kwani baada ya kuona majina ya wale ma-prof. tukajua ni mwendo wa kusifias mwanzo mwisho na ukweli hautasemwa!
Kwa taarifa tu ni kuwa Ethiopia wana miundo mbinu bora na ma-fly over kila eneo lkn wananchi wake kila kukicha wanakimbia nchi yao kutokana na utawala.
 
Kongamano la Tathmini ya hali ya kiuchumi na kisiasa likawa kongamano la kumsifia Magufuli. Ni mpango ulioandaliwa kabla, ili kumjengea Rais Magufuli imani kwa wananchi, imani inayopotea kila kukicha kutokana na matendo ya hovyo ya serikali ya awamu ya tano.
Sikusikia mambo mazito yakigusiwa, matukio ya utekaji, upoteaji wa watu yenye viashiria vya uhusika wa vyombo vya usalama, ongeza na jaribio la mauaji ya Mh. Tundu Lissu.

Mauaji ya raia ndani na nje ya vituo vya polisi.

'Uchuro' wa tume ya uchaguzi iliyogeuzwa kuwa idara ya chama cha mapinduzi.
Utumwa wa bunge kwa serikali.
Serikali kuingilia kazi za mahakama.
Kauli za Rais, zinazofifisha hadhi ya taasisi ya Urais, kama ile ya kuwapiga mashangazi wa wabunge wa kusini, kauli ya kupinga uzazi wa mpango, kauli za kuchochea chuki kati ya jeshi la polisi na raia wenye mawazo kinzani hususani viongozi wa vyama vya upinzani.

Hayo ni baadhi ya hoja nzito zilizopaswa kujadiliwa.

Maprofesa wetu, hasa Kitila Mkumbo na Kabudi Paramaganda, waliamua kwa makusudi, au pengine ndio ulikuwa mpango, kugeuza kongamano na kuwa mkutano wa kampeni. Mambo mengi waliyogusia ni mambo Mtambuka, wajibu wa serikali.
Ingependeza kusikia mjadala wa kifalsafa zaidi kama alivyofanya Profesa Mukandala. Hayo ya mambo ya mipango ya serikali kila mwaka tunayasikia ni masuala Mtambuka. Tangu awamu ya kwanza utasikia ujenzi wa barabara ile, kiwanda kile, reli ile, daraja lile, uchumi unakua, tumeongeza fedha za manunuzi ya dawa, ruzuku ya mbolea nk.
Tumeyasikia hayo tangu na tangu.
Hayo si ya muhimu kama masuala mazito yanayohusu uhai na hadhi ya binadamu, haki za binadamu, uhuru na amani. Nk.
Mjini Damascu, Syria kuna ma'flyovers' madaraja na miundombinu mingi ya kisasa, lakini raia wa Syria wanakimbia nchi yao na kwenda kuishi kama wakimbizi kwenye nchi za watu.
Kama viongozi wetu wataendelea kutumia ujenzi wa 'vitu' kama kisingizio cha kuhalalisha falsafa mbovu ya utawala wa awamu ya tano, watatupoteza.

Janga lingine kubwa ni la viongozi wa ngazi za chini, wakuu wa wilaya, mikoa na wenzao, ambao wameamua kwa makusudi kuwa manyapara wa wananchi. Sijalisikia likigusiwa, isipokuwa mchangiaji mmoja alilisema kwa uchache.
Rai, yangu kwa waandaaji wa Kongamano, ikiwa kuna mpango wa kuandaa Kongamano lingine, ni vema wachangiaji wakuu wagusie masuala ya kifalsafa, tafakuri, fikara, tathmini nk. Sio kufanya kampeni.

Halafu la mwisho, Tumuache Nyerere apumzike. Hili jambo la kumlinganisha Magufuli na Nyerere, linaweza kutuletea ukame ambao haujawahi kutokea. Laana zingine tunajitakia wenyewe.View attachment 918223

Mkuu wangu sasa hivi ni mwendo wa kusifu na kuabudu, PhD tupa kuleeeeeeeeeee!!!!
 
Niltegemea Hoja kuhusu uwanja wa ndege wa chatu, rushwa kubwa za vyeo vya ubunge na udiwani,double standard hewa kuhusu bomoabomoa ajira,watu wasiojulikana kuwa na nguvu kuliko dola.nk
 
Back
Top Bottom