Rais Magufuli: Sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani (Covid19), tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya. Akemea Chanjo

Rais Magufuli: Sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani (Covid19), tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya. Akemea Chanjo

Jamani mimi naomba sana Watanzania waendelee kumsikiliza Rais wetu, anajua mengi na ana watu wamemzunguka wanaojua mengi sana
 
Nmesikitika sana ,nmesikitika sana nikiwa kama Mtaalam wa Afya

Kauli hii ya Kubeza Chanjo

Maana yake anawaaambia wamama sasa wajawazito na watoto, waanze kuzikimbia Chanjo.

Ivi nin hii???
Machanjochanjo hayafai....
Au nasema uongo Ndugu zangu?

😀
 
Akili kichwani mwako,sio kwamba ukivaa barakoa utakamatwa,hujazuiwa kuepuka misongamano,ukitaka kujifungia utajua mwenyewe,hata ukitaka kunawa mikono Mara 1000 kwa siku hakuna atakayekuzuia,sio lazima mpaka Raisi aseme ndo uanze kunawa mikono,watanzania ni watu wa kulalamika sana
 
Mtatishwa sana ndugu zangu Watanzania lakini simameni imara, ninajua wapo baadhi ya Watanzania wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa na walipochanjwa huko, wamekuja huku wametuletea Corona ambayo ni ya ajabu ajabu, simameni imara...
hapo kwenye machanjomachanjo (tahadhari)
 
Naona waraka wa TEC umefanya mzee afunguke kidogo. Kwa ufupi waraka wa TEC na mh Rais wote wamekiri lipo tatizo hivyo dawa ni tusisitizane kujikinga badala ya wengine kudanganya tatizo halipo.

Mh Rais kasema tuendelee na nyungu na leo mimi na familia yangu tunaanza nyungu [emoji41]

Magufuli anawachanganya wananchi.

Nadhani tatizo ni kwamba " ameu-personalize " huu ugonjwa.

Anakosea kuchanganya masuala ya covid-19 na vita yake dhidi ya " mabeberu. "

Nia AIBU chombo kama TEC kuanza kuwatahadharisha wananchi kuhusu maambukizi ya covid-19[au ugonjwa wowote] kabla ya mamlaka za serikali.

cc Nguruvi3
 
Leo ndo nmegundua kanisa katoliki lina nguvu kubwa..baada ya waraka wa corona kutoka na Askofu Ruachi kuongea watu kujilinda na kujikinga na corona leo mzee kaja kuongea
Corona ipo ni kidogo
Ooh haipo kabisa
Ohh watanzania wametuletea yaani anajiuma uma tu.
Bakwata huwaamini?
 
..Magufuli anawachanganya wananchi.

..nadhani tatizo ni kwamba " ameu-personalize " huu ugonjwa.

..anakosea kuchanganya masuala ya covid-19 na vita yake dhidi ya " mabeberu. "
Hakuna alichochanganya, ameongea kama mtaalamu siyo kisiasa.
 
Nmesikitika sana ,nmesikitika sana nikiwa kama Mtaalam wa Afya

Kauli hii ya Kubeza Chanjo

Maana yake anawaaambia wamama sasa wajawazito na watoto, waanze kuzikimbia Chanjo.

Ivi nin hii???

Ndiyo kawaida ya JPM hiyo.

Akizungumza neno moja la ukweli, ataongeza mengine matatu ya uongo.
 
Kama wazungu wabaya amtolee mama ake Ventilator, asiende hospitali na asijenge hospitali maana hakwepeki.
 
Safi sana Magu kawapiga spana wazungu, HIV miaka 40 hakuna chanjo, kansa miaka 100 hakuna chanjo, malaria miaka 50 no chanjo, korona miezi 6 chanjo tano wazungu wamezoea kuwafanya wengine mazwazwa...hakuna chanjo hapo ni biashara tu inafanyika..
 
JPM amekuwa madarakani miaka 5+, ktk kipindi cha utawala wake Tz tungeweza kutengeneza chanjo za magonjwa mbalimbali ambazo ni salama na tunaziamini.

Tusilaumu tu chanjo walizotengeneza wenzetu, wakati sisi wenyewe hatujatengeneza chanjo ya ugonjwa wowote ule.
 
Back
Top Bottom