Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Mkuu kuna kauli zingine za kifedhuli kama hizi zinasababisha mtu awe hasira. Huyu kila anapoongea anatoa kauli tata zinazosababisha mijadala na hana tofauti na Mkuu wa mkoa wa Tanzania. Hata kama hataki kuwasaidia lakini hakupaswa kutoa kauli chafu hasa kipindi hiki cha majonzi
 
Maafa ni fykofyoko? Lete fyokofyoko uone ya magu
 
Hivi ingetokea Chato kauli hizi zingetoka ?!
Ulitakiwa umuone wakati anasema ili uone body language yake na tone yake wakati anaongea, ungekuwa umemuelewa, ila mwenzangu naona unachukulia kama vile alikuwa anaongea kwa ukali, wenye akili na uelewa wamemuelewa rais.
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Tatizo tunafanya kazi na social media sana siku hizi hadi shida.. Tufanye reality sio SM..
 
Huyu rais ni wa ajabu kwelikweli. Ndiyo maana hata ameshindwa kutoa shukrani kwa mwenzie Kenyatta kwa msaada alioutoa kwa Tanzania! Anafedhehesha sana na kukatisha tamaa kwa kiwango cha hali ya juu kabisa.

Hayo maneno kutolewa na mkuu wa nchi bila hata kutoa shukrani kwa waliojitolea kuchangia misaada mbalimbali ni laana! Hivi haelewi ni yapi hasa majukumu yake?

Tanzania kwa sasa tuna janga!
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Ndio wapo wanaoamini hivyo maana wapo pia wanaoamini kupatwa kwa jua kuliletwa na serikali hivyo mkuu yupo sahihi kabisa. Nimeipenda sana hii maana lawama kwa serikali hazikomi utadhani serikali ni ya kinabii. Fanyeni kazi
 
Kuna jambo ambalo halijakaa sawa ambalo ukiona halileti faraja
 
Sasa kama ukuta umeanguka,ajengee kwa nini?,mate au tope,manake hapo anahitaji saruji ya kutumia,hela hana afanyeje au akaibe. Au kakusudia watu wajenge Nyumba zao za fito na tope, ndio tu arudi kule kuishi kama shetani,ulimbukeni mbaya sana.🙁
 
Ulitakiwa umuone wakati anasema ili uone body language yake na tone yake wakati anaongea, ungekuwa umemuelewa, ila mwenzangu naona unachukulia kama vile alikuwa anaongea kwa ukali, wenye akili na uelewa wamemuelewa rais.
Ndugu yangu kumbuka waathirka wengine kule Bkb ni majeruhi, wengine ni wazee wanahitaji faraja tena mapema si makavu na michakato

Mfuko wa maafa ni hewa ?! Mpaka michango ya wiki mbli na zaidi ?!
 
Anachonishangaza ni kuwa misaada hii ilitolewa haraka na Nchi rafiki na aliowaita mashetani wakitegemea itawafikia haraka walengwa kutokana na madhara yaliyowapata. Badala ya kuipeleka haraka kupunguza majonzi anatoa kauli chafu. Huyu ni mtu asiye na huruma kwa watu wake cha msingi hapa wana kagera wanapaswa kuwa wavumilivu wasubiri 2020 ili wamtibu kupitia sanduku la kura
 
Duh???

Kwa kauli hii ya Mweshimiwa Rais kwangu Binafsi sijaipokea katika mtizamo chanya, alipaswa awatie moyo katika kipindi hiki kigumu walichopo na si kuwasimanga kwa maneno makali kiasi hiko.

Kwa hakika naanza kuona awamu hii itakuwa chungu sana juu ya wale wanaokaa jangwani endapo wakikumbwa na Mafuriko, ama wakazi wenzangu wa kule Kilosa, Mikoa ile yenye historia ya ukame kama Dodoma nao wajiandae kisaikolojia kwa maneno makali wakosapo chakula.

Nimeanza kukusoma Mkuu wa Kaya, Asanteeeeeee...!
 
Kenya Uganda wameguswa wametoa msaada serikal ya Tanzania bado haijaguswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…