Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Bora Mhe. Rais kasema. Unakuta mtu ukuta tu umepata ufa, analalama ooooh mim sijakula siku mbili sasa. Hebu oanisha mwenyewe. Its true baadhi yao wanataka kutumia tetemeko kama fursa ni tabia ambayo sote tunatakiwa kuikemea.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mi nadhani itakuwa vyema misaada itumike kusaidia wahanga.

Suala la miundombinu ibaki kuwa jukumu la serikali.
 
Kusahidiana wakati wa matatizo ni hulka ya binadamu wajibu wa serikali katika majanga makubwa hayakwepeki
 
Hii yote shauri ya Pasco kung'ang'ania eti "sema neno moja tuu na roho yangu itapata ahueni"
Ona sasa neno gani hilo? Kwani nani kasema tetemeko limeletwa na Ccm?
Halafu hata hilo la kusema watu wafanye kazi wasibweteke hata kama ni ukweli sio wakati wake huu wakiwa msibani.
Mzee aendelee kukaa kimya inatosha
Mnataka atoe ahadi hewa?
 
hapo anatamani ile misaada yote iliyotolewa ilipiwe kodi...
 
Kumlaumu mkulu kwa hizo kauli zake nikumuonea, maana mi nimeona yaani kajitahidi mpaka mwisho kuwa mpole na mwenye “busara”. Ametumia alichonacho
 
Mnataka atoe ahadi hewa?
Mani anataka ahadi wakati huu? Kuna misiba Kule, watu wanalala nje watoto na kina mama, hata chakula ni shida.
Atoe basi kauli za kiungwana kuonyesha anajali au anyamaze kama hawezi kuji control.
Hivi kauli kama zile mtu kama mtendaji wa kata akizitolea Kule Bukoba atashuka hai kweli jukwaani? Sii mvua ya mawe itamfuata alipo!
 
Hio ndio inapaswa kuwa kauli ya kiongozi...sio kuwapa watu matumaini hewa...
Sio kuwapa matumain hewa watu wanashda saaana mkuu kama jana umechek taarfa ya (H) nadhan umeona wazeeee wakilia kuhus ishu nzima,
kama serikal haina hela bas hata hzo zilizochangwa wapelekewe haraka si tathmin imefanyka tayar???, why people still crying en blaming to Gvt ????
 
Oh watanzania fanyeni kazi, hivi miaka yote hii hadi ujio wa Magu Watanzania walikuwa wanacheza? Nonsense.
 
Nilitegemea kusikia serikali imetenga kiasi gani kwa ajiri ya wahanga wa tetemeko badala yake anaongelea juu ya hela iliyochangwa na wasamaria wema wa ndani na nje ya nchi.
Ambazo serikali imeshindwa kuzipeleka Kagera kusaidia matatizo ya awali wakati rehabilitation ikifuatia baadae.
Kwenye taarifa hiyo hiyo ya saa mbili wahanga wamelalamika kwa mwandishi ya ITV Audax Mutiganzi kuwa siku 7 zimepita bado wanalala nje bila msaada wowote kila kukicha wanapita watu wa kutathimini madhara as if huo ndio msaada.

Kwanini walale nje? Hivi taifa hili halina wataalamu wa disaster management? Kuna vitu vya kufanya hatua kwa hatua kuanzia saa la kwanza hadi msala unapoisha....disaster management ni taaluma ambayo husomewa miaka minne chuo kikuu.


Nakumbuka mwaka juzi mh Jennister aliongelea muswada fulani bungeni wa kuhuisha kitengo cha maafa kipesa. Ilikuwa ni paukwa?
 
Back
Top Bottom