Rais Magufuli; ubanaji matumizi; na kujichanganya [contradict]

Ila mkuu unadhani ni matumizi mabaya kupeleka makao makuu dodoma, kama kitu kinafanyika kwa nchi ya tanzania si ndo kazi ya fedha ya mlipa kodi hiyo, asipofanya sahivi atafanya nani, ulikuwa ni mpango uliotakiwa kufanyika miaka ya zamani sana, ndo anafanya sahv, fair enough, labda uniambie matumizi mabaya yasiyo na manufaa kwa nchi ndo nikuelewe,

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kutembelea kwa minajili ipi?
 
Cha kushangaza kuhamia Dodoma ni moja ya mambo machache nampongeza. Nchi haiwezi kutegemea mji mmoja tu. Dar ni kero bora watu tugawane maendeleo na maeneo ya kuishi.
 

Mpango ulikuwa wa zamani.

Miaka karibu 50 imepita.

Hakuna tena sababu ya msingi ya kuhamia huko.
 
Ahsante NN,
Sio wewe peke yako, wapiga vigelegele wenzio wote wameanza kurejewa na akili zao!!

Ni kitambo kidogo tu wote tutaongea lugha moja!

Umeanza kunisoma lini wewe?
 
Mpango ulikuwa wa zamani.

Miaka karibu 50 imepita.

Hakuna tena sababu ya msingi ya kuhamia huko.
Tatizo tunajaribu kutafuta kila kitu kinachotufaa sisi binafsi ndo tuone cha maana, bunge kuwa dodoma kila mtu anakubali, historia ya nchi yetu inasema mji mkuu wa tanzania ni dodoma, nyerere alivision makao makuu ya nchi, hadi ikulu iwe dodoma tatizo alilolikumba yeye kipindi hicho nchi changa akafanikiwa kukuta bunge lipo dodoma akaishia hapo, waliofata hawakutaka kufuatilia hilo swala wakala bata zao wakamaliza majukumu yao fresh, sasa kaja huyu kaona mi nataka nimalize hili swala kabisa, sasa kila mtu anaona oooh huu ni upuuzi, how come wakati ilikua ndo moja ya plan ya nchi, kwangu mi naon kwakuwa ni mpango wa kuinufaisha nchi na dodoma ikiwa imejengwa itanufaisha tanzania nzima wala sioni matumizi mabaya yapo wapi hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewahi kujiuliza kwa miaka zaidi ya 30 tumetumia shs ngapi kwa ajili ya allowance ya watumishi wa umma waliokuwa wanaenda Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge?
 
Kusafiri kwenda Dodoma toka mikoani ni rahisi kuliko kutoka Mikoani kwenda Dar es Salaam

Kwani Watanzania wanaendaga Dar tu?

Serikali ingepaswa kuwa na ofisi zake muhimu kwenye kanda, kama hawana mpaka hivi sasa.

Hiyo ni bonge la option.

Mtu wa Simiyu akitaka huduma flani flani basi anaenda Mwanza.

Wa Iringa akitaka huduma flani kama Iringa haipo basi anaenda Mbeya.

Lakini siyo kuhamisha serikali nzima iende Dodoma..
 
Kazi kweli kweli... Dodoma imekua kero na catalyst ya kuvunja ndoa na chachu ya mifarakano ya familia, Wanataka wenzao waende Dodoma huku wao wako mjini kila siku na familia zao huku wenzao wakiwa wanaishi maisha ya big brother na kulala bar!

Ukiona maVX V8 ya viongozi waandamizi yanavyojiachia Dar unajiuliza sijui nani kaenda dodoma!
 
Mwisho wa siku huoni tatizo lolote,

- Kurudiwa kwa chaguzi za kijinga kuwahi kutokea nchini,

- Tundu Lissu kupigwa risasi 38 bila hatia yoyote na kunyimwa haki zake.

- Mtu mmoja kuamua kununua ndege kwa gharama kubwa mara mbili ya bei halisi wala huoni tatizo.

- Mtu kuhubiri chukiii na migawanyiko huku akiwa-brand watu wengine uovu wala huoni tatizo.

Unachokifanya ni kuokoteza masuala machache kujaribu kudanganya watu kuwa uko neutral. Kumbe wala huoni tatizo lolote ..
 
Hivi rais alishahamia Dodoma? Aliahidi kuhamia kabla ya Desemba 2018.
 

Ulikuwa ni mpango wa enzi hizo.

Miaka karibu 50 imepita.

Nchi ina changamoto nyingi mno kuliko wakati ule.

Kipaumbele sasa hivi kinapaswa kuwa ni kukabiliana na changamoto zilizopo ili kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa miaka yote hiyo nchi imeenda vizuri tu.

Mji mkuu uendelee kuwa Dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…