Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki

Hivi ushawahi kaa Dodoma hata siku 1?
Ule mji haufai

Sent using Jamii Forums mobile app
Dom kuna upepo wa dhiki. Kwa maendeleo sayansi na tekinologia e government, amani na utulivu hoja za Dodoma makao kwa zama hizi hazikuwa na mashiko. Uwekezaji Dom ungewekezwa ktk miundombinu umwagiliaji kilimo na kilimo tungelisha Africa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anawazuga hao mabalozi, ukweli ni kuwa yeye hasa ndio tatizo la chaguzi zetu kwa sasa. Kama kweli anaamini katika chaguzi huru na haki, tuwe na tume huru ya uchaguzi isiyoundwa wala kuchukua maagizo kutoka kwake. Kinyume na hapo ni kuwa anaongea maneno ya kufurahisha genge.
Subiri October!
 
Kuna ile clip Magufuli alisema "Mimi nikiwa Rais, watu watalimia meno"😂😂😂
 
Hakuna kitu hapo, hiyo ni janjajanja ya kuwashawishi wapinzani washiriki uchaguzi ambao CCM wanajua kuwa kitakachotokea ni kama kile kilichotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kama uchaguzi utakuwa ni huru na haki kwanini hajafuta kauli yake ya kuwapiga marufuku wakurugenzi kuwatangaza wapinzani watakao shinda kwenye uchaguzi?.
 
Amekumbuka kuwaambia hao Mabalozi kuwa kuna maagizo alishatoa kwa Wakurugenzi wake yakua amewateua yeye, magari amewapa yeye na mafuta amewapa yeye, aje asikie WAMETANGAZA MPINZANI KASHINDA?

Ukiwa mwongo usiwe msahalifu!

Rais anafikri watu wote ni mazuzu kama mashabiki wa CCM. Kesha sahau watu walisha record video na sauti Rais akitoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri (kama Wasimamizi wa Uchaguzi) kwamba atakayemtangaza MPINZANI KUSHINDA AHESABU hana kazi! Hawezi kuwapa magari ma mishahara halafu waruhusu mpinzani kushinda!

Dunia nzima ilishuhudia ile kesi ya Kikatiba kuzuia Wakurugenzi wasisimamie chaguzi na Mahakama ikaridhia bado Serikali wakakata rufaa na wakaruhusu waendelee kusimamamia!
 
Back
Top Bottom