Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki

Pascal Mayalla,
Pascal,

Kuita kilichotokea mwaka Jana kuwa ni uchaguzi ni keleta dhihaka kwenye mfumo mzima wa demokrasia. Ule hauluwa uchaguzi hata kidogo, na haukidhi hata nusu vya kufanya uchaguzi, achilia mbali uchaguzi ulio guru na haki.

Kama kilichitokea mwaka jana ndio kitatokea kwenye uchaguzi mkuu (ambapo imejitokeza Mara kadhaa kwenye uchaguzi ndogo) basis ni dhahiri uchaguzi hautakuwa hiru na haki.

Naleta tena swali langu ambalo ulilikwepa kwenye post nyingine " ni nini kinakufanya useme tume ya uchaguzi ni huru"??
 
Pascal,
Naleta tena swali langu ambalo ulilikwepa kwenye post nyingine " ni nini kinakufanya useme tume ya uchaguzi ni huru"???
Mkuu Ngambo Ngali, nakumbuka hili swali nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na kila siku huwa nalijibu jibu lile, Tume yetu ya uchaguzi, NEC ni tume huru kwa mujibu wa sheria ya uanzishwaji wake, na uchaguzi wetu kwa mujibu wa kanuni ni uchaguzi huru na wa haki.

Tatizo la tume sio kuwa sio huru bali sio shirikishi, not inclusive, ni tume huru kama ilivyo bunge na mahakama.
Uchaguzi ni huru na wa haki kwa mujibu wa the electoral process.

  1. Uchaguzi unafanyika kwenye kituo, kutumia transparent ballot boxes kura zinapigwa mawakala wa vyama wakishuhudia, na matokeo yote hadi ya urais yanabandikwa kituoni, hivyo manouvers utafanyia wapi.
  2. Niliuliza kama hakuna maneuvers zozote, kwanini walizuia independent tallying, sikupata jibu, kinachokatazwa kisheria ni kutangaza matokeo na sio kufanya tallying.
  3. Hoja ya mmoja wa wagombea kuteua tume na wasimamizi hivyo wote ni makada haina mashiko kwasababu ballot boxes ni transparent.
  4. TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!
P
 
Hii ni ahadi nzuri sana, na victory margin ni ile ile ya 99.9% kama kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
P
Hivi Bwana Mayalla nikuulize Suala, Hivi wewe ndio yule yule tunayefikiria kuwa ni msomi?
Kwa nini hujipamabanui ukabakia maskani tu ya CCM ikifika mwisho wa wiki ukapewa buku 7.5 kwa kazi mzuri mitandaoni? Kama kweli wewe ni yule Msomi mwandishi wa habari, ningetegemea mada zako ziwe za uchambuzi zaidi ambazo mtu hawezi kukuelewa uko mrengu gani. Venginevyo unatupa mashaka. Nenda kajifunze Tena kwa waandishi kama Ahmed Rajabu
 
Uchaguzi huru na haki utanguliwe ya yafuatayo.

Kufungua majarida mapya ya upelelezi kwa wote waliopotea ama kupigwa risasi na waliouawa hasa katika harakati za kisiasa.

Kuruhusu mikutano ya kisiasa ya hadhara. kuwahakikisha watanzania usalama wao hasa wanasiasa wa vyama vya upinzani. Kuondoa uhasama uliopo kati ya wana CCM na wanachama wa vyama vingine vya siasa.

Kufuta kesi zote za kisiasa zilizoko mahakamani ambazo watanzania wengi wanaona ni za kukomoana
Kutangaza vita kwa kundi la utekaji na kulitokomeza kabisa.

Kupata muafaka wa kisiasa wa kitaifa, kusameheana ili tujenge nchi yetu. Kulaani vikali na kutoa onyo kwa wale wote waliosimamia ule uhuni wa Serikali za mitaa wakauita uchaguzi.

Baada ya hayo then Rais atakuwa tayari sasa kuwaambia watanzania kwamba uchaguzi 2020 utakuwa huru na haki.
 
Tunakuaminia mkuu wetu. We piga kazi tu. Hao wapinzani watafanya mikutano mingapi huku weshaambiwa kuwa; Hata bunge likivunjwa hawapewi chao hadi baada ya uchaguzi?? Wadhani kugombea ni mchezo?? Hata hela ya kumnunulia banana mpiga kura huna! Wenzako wakifika wanamwaga maji ka takataka. Tutawapa walio tupa hayo maji kura zetu
Unajisifia kwa kutoa rushwa, tena eti rushwa ya banana na maji! Hiyo siyo sera ya CCM
 
Hivi Bwana Mayalla nikuulize Suala, Hivi wewe ndio yule yule tunayefikiria kuwa ni msomi?
Kwa nini hujipamabanui ukabakia maskani tu ya CCM ikifika mwisho wa wiki ukapewa buku 7.5 kwa kazi mzuri mitandaoni? Kama kweli wewe ni yule Msomi mwandishi wa habari, ningetegemea mada zako ziwe za uchambuzi zaidi ambazo mtu hawezi kukuelewa uko mrengu gani. Venginevyo unatupa mashaka. Nenda kajifunze Tena kwa waandishi kama Ahmed Rajabu
Ni mimi, ila sijawahi kujipambanua kuwa ni mwandishi msomi, ila ni mwandishi mzoefu, mwaka huu ni mwaka wangu wa 30, nime cover chaguzi zote 5 za vyama vingi tangu 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, nikicover na mwaka huu utakuwa ni uchaguzi wa 6, hivyo ninachoeleza ni kitu cha kweli from eksipiriensi.
P
 
figganigga,

I think alipotamka maneno haya alidhani audience iliyomzunguka ni kama ile ya kina propesa pumbavu jalala.

Surely he's in for one hell of a lifetime shock come October 2020!
 
Pascal Mayalla,
Rule of bias inaifanya tume ya uchaguzi kuitoendesha na kusimamia uchaguzi katika misingi ya haki na Uhuru. Chini ya katiba yetu tume ya uchaguzi inateuliwa na Rais. Rais anayeteua tume hiyo kwa vigezo ambavyo havijaainishwa ni mgombea kwenye uchaguzi unaoendeshwa na kusimiwa na tume hiyo hiyo aliyoiteua. Hii ni kinyume rule of bias na kitendo chochote kinachofanywa na kuonesha uwezekano wa bias hakiwezi kusimama mbele ya mahakama yoyote.

Pili, nafasi za wajumbe wa tume zinapatikana kwa njia ya uwazi na ushindani, kama ni kwa ushindani ni vigezo vipi vinatumika lupata wajumbe.

Je, wajumbe wanapatikana kwa uwazi, hapana, aghalab husikia kwenye vyombo tu kuwa Fulani kateuliwa, nafasi ilitangazwa hapana hill nalo ni tatizo.

Vitu hivi viwili vinafanya tume isiwe huru kabisa. INCLUSIVENESS inaweza kutatuliwa kwenye transparency and openness katika kupata wajumbe wa tume.
 
Ni mimi, ila sijawahi kujipambanua kuwa ni mwandishi msomi, ila ni mwandishi mzoefu, mwaka huu ni mwaka wangu wa 30, nime cover chaguzi zote 5 za vyama vingi tangu 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, nikicover na mwaka huu utakuwa ni uchaguzi wa 6, hivyo ninachoeleza ni kitu cha kweli from eksipiriensi.
P
Hiyo Experince umeichukulia wapi Tanzania tu? Hio sio Experiecnce ni Mazoeya. Bora ungelipitia chaguzi zanchi mbali mbali duniani hala ukalinganisha, hio ndio itakuwa experience
 
Hiyo Experince umeichukulia wapi Tanzania tu? Hio sio Experiecnce ni Mazoeya. Bora ungelipitia chaguzi zanchi mbali mbali duniani hala ukalinganisha, hio ndio itakuwa experience
Eksipiriensi yangu ni kwa uchaguzi wa Tanzania tuu. Hapa tunazungumzia uchaguzi wa Tanzania na demokrasia ya ki Tanzania ambayo ni sehemu ya African democracy.
P
 
Back
Top Bottom