Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki

Hata hivyo mpaka sasa hivi mm kwa upande Wangu bado sijaona ambae atapambana na mkuu kwenye urais Kama VIP aendelee tu mpaka atakapoachia kijiti 2025
Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkono hoja, hata mimi niliwahi kushauri
P
 
Tafsiri ya uchaguzi huru na haki aliyonayo Jiwe sio ile inayofahamika na wengi! Ana yakwake kama ilivyokuwa kwenye chaguzi za marudio na serikali za Mitaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

AHahaa ahaaaa Paskali bana, ni sawa na kusema timu ambazo hazibebi kombe la ligi hapa nchi zisishiriki maana hazitabeba hilo kombe! Kwani sisi tuliposhiriki Afcon ilikuwa ni kwakuwa tutabeba hilo kombe? Ni hivi, Magufuli hawezi siasa za ushindani na wala hatakaa aziweze, hata kama atashinda huo uchaguzi hana uwezo wowote wa kushinda kwa zaidi ya 50%+ kama uchaguzi ni wa haki.

Na isitoshe kura za urais pia hata kama hutashinda zinachangia viti maalum vya ubunge. Sema unamtetea asipate ushindani sio kwamba kwakuwa anakubalika sana, bali hutaki apite kwa ushindani maana hana uwezo wa kushindana. History yake inaonyesha toka akiwa mbunge hakuwa anashinda kwa box la kura bali figisu.
 
Hii ni ahadi nzuri sana, na victory margin ni ile ile ya 99.9% kama kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
P
Bila Tume Huru ya uchaguzi ni kudanganyana tu na hiyo 99.9% wataipata kwa kutumia polisi, tume na wakurugenzi ambao ni Makada wa CCM na huo si ushindi wa kujivunia ni kupoka tu uchaguzi.
 
Hawezi siasa za ushindani na wala hatakaa aziweze, anachotegemea ni madaraka yake kumfanya atangazwe mshindi fullstop.
Hizi kauli za hawezi na hatakaa aweze, huku mtu anaendelea kudunda, ni kauli za kujifariji tuu, sasa 2020 Magufuli na CCM wanakuja na tsunami ya kisulisuli, CCM itakomba kila kitu!.
P
 

Viongozi wa ccm wanatugeuza watz kama vifaranga wa kuku......."nyonyo kesho"
 
Pascal kujua mshindi wa uchaguzi mkuu na kujua mpaka asilimia ya mshindi miezi 9 kabla ya uchaguzi ni kiashiria tosha kuwa uchaguzi hautakuwa huru na haki
Mkuu Ngambo Ngali, hizi ni trends, baada ya kushuhudia kilichotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, na kimekubalika, then hicho ndio kiwango chetu cha uchaguzi huru na wa haki na hiki ndicho kitakacho tokea kwenye uchaguzi Mkuu.

Trends za uchaguzi Mkuu wa mwaka huu niliziweka hapa mwaka jana baada ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa

P
 
Hizi kauli za hawezi na hatakaa aweze, huku mtu anaendelea kudunda, ni kauli za kujifariji tuu, sasa 2020 Magufuli na CCM wanakuja na tsunami ya kisulisuli, CCM itakomba kila kitu!.
P

Kwa mfumo wa uchaguzi ulivyo hata mbuzi akiwa rais anaweza kushinda kwa maelekezo tu, na akapanga kiwango cha kutangazwa mshindi. Ni kweli CCM itakomba kila kitu, ila sio kwa box la kura, sasa hapo kuna tofauti gani na serikali iliyoingia kwa kupindua nchi?

Huo ushindi wa mezani unaweza kusimama mbele ya wanaume wanaokojoa kwa kusimama na kujisifia? Bila tume huru ya uchaguzi hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kusimama kwenye mstari wa kura kushiriki huo uhanithi. Acha CCM wajitangaze washindi ila sio kwa ushindani, hilo hatuna tatizo nalo kwani pia kuna serikali zinapatikana kwa kupindua nchi. Habari ndio hiyo.

Kwa taarifa yako bwana Paskali tulishatoka utumwani Misri enzi za mfumo wa chama kimoja. Hakuna kiongozi au kikundi chochote kinaweza aidha kwa ushawishi au kwa mabavu kuturudisha kwenye mfumo wa chama kimoja kwa ridhaa yetu.

Wanachoweza ni kwenda kujazana bungeni na kwenye mabaraza ya madiwani kwa ajili ya uchu wa madaraka, lakini sio kwa ridhaa yetu. Huo ndio ukweli, tulishamka, na huu uhuni utaendelea kwa muda fulani kwa ajili ya hofu ya muda, lakini ni jambo litakalobackfire. Tuombe uzima tutakuwa hapa hapa nitakukumbusha ukweli huu.
 
Muongo mkubwa Kama aliuharibu uchaguzi mdogo ambao haumgusi yeye moja kwa moja tutamuaminije katika UCHAGUZI huu ambao yeye ndio kiini? Aache uongo wapinzani msikubali kuingia kwenye huu uchaguzi mtakuwa mmeuhalalisha.

figganigga
 
Ndo shida yahuyu ndg. Badala aseme nafuta ile kauli yangu kuhusu wakurugenzi kutotangaza wapinzani wameshinda, anadhani aliokua anaongea nao NI wananchi wa MTERA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…