RockCarnegie
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 963
- 1,927
Habari wana JF
Leo wakati Rais Magufuli akivunja bunge, katika hali inayoonyesha hofu ya kutojiamini kuelekea Kampeni za Uchaguzi Mkuu ujao, ametadharisha kuwa watakokuwa wanatoa matusi watashughulikiwa!
'Matusi' ni neno la jumla sana, na sidhani kuna watu waliomuelewa ni matusi gani ambayo hayataki kuyasikia Rais wetu mtukufu!
Ninavyofahamu vyombo vya ulinzi na usalama husimamia sheria, je haya matusi yanayomkwaza Rais yapo kwenye sheria ipi na ni yapi ili tuwe makini tusije tukaingia kwenye matatizo wakati tukishusha nondo majukwaani wakati wa kampeni!?
MATAGA tusaidieni kujua kipi hampendi kusikia, maana nyundo mbili tu za ununuzi wa midege na ujenzi wa uwanja wa Chato za John Pambalu zlitosha kusitishwa kwa kipindi cha Ajenda 2020 cha Star TV!
Nionavyo ni kuwa rais na CCM wana hofu kubwa hawana uhakika kama wataungwa mkono na wananchi wakati wa kampeni na hatimaye uchaguzi.
Nawasihi watakaokuwa majukwaani kunadi hoja na sera kutoka upinzani wajiamini na washushe nyundo za ukweli bila hofu, kwani wananchi wameshachoka kusikiliza mapambio ya kusifu na kuabudu!