Uchaguzi 2020 Rais Magufuli, Una hofu na matusi gani wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu!?

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli, Una hofu na matusi gani wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu!?

Nawambieni hoja ya watumishi wa umma kutelekezwa ni hoja kubwa sana mwaka huu, kumbukeni kundi hili ndilo lina uelewa mpana sana kwenye jamii kwasababu ya kuelimika nakumbuka miaka ya 2005 nilifanya ushawishi mkubwa kwa ndugu na jamaa wampigie kura Kikwete, wapinzani kete hii ambayo haija pindapinda miaka mitano danadana za maslahi ya watumishi na kejeli,nawambieni hii ni hoja kubwa chama kitakacho itumia vizuri kitapata odds za kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Bonge la Point,wakiweka na mafao ya wastaafu wamemaliza kazi.
 
Bonge la Point,wakiweka na mafao ya wastaafu wamemaliza kazi.
Hao wastaafu wanaingia mkenge tu kwa kupigwa sound nyepesi tu kuwa "tuchagueni tena tukamalizie mafile yenu mlipwe malipo yalikua kwenye hatua ya mwisho kabisa yani nyie wenyewe mtafurahi account zenu zinajaa mapesa mwezi mmoja baada ya kutuchagua tena"
 
Rais yupo sawa sheria za nchi zinazuia matusi. Kwa hiyo wanaotukana watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Mfano kifungu cha 89(1)(a)(b) kipo wazi kwamba mtu akitumia lugha kutukana au lugha chafu kiasi cha kuhatarisha amani anafanya kosa. Kwa hiyo matusi na lugha chafu ni makosa msidhani mtapona.

Huyo Pambalu mnafagilia kwa kipi cha maana alichoongea? Kama Budget Act, 2015 kifungu cha 41 kimeweka wazi kuhusu reallocation of funds. Kama budget kubwa ya serikali ilipitishwa alafu yakafanyika mabadiliko ya matumizi ya pesa na kununua ndege au kujenga uwanja Chato tatizo liko wapi?
 
Wanajitahidi kujificha vichwa mchangani,walijisahau wakawa wanajinadi kwa vitu hewa ambavyo wamekeza matrilioni ya fedha za Watanzania na mikopo ya kila aina.Miradi yao bado IPO kwenye unproductive stage, haizalishi na haitaleta faida yoyote pre election na wanashuku wapinzani watautumia huo udhaifu kuwapondea kwa wapiga kura. Ndiyo maana hoja hizi wanaanza kuzipa jina LA matusi.Kuna watukanaji zaidi ya CCM nchi hii?

Ukimsikiliza Mzee Baba anavyojitetea mbele ya Cameras kwa miaka mitano hadi huruma,kila siku vitu vile vile hadi vinakera,maamuzi nje ya ilani na bajeti kama ya kununua ndege kwa cash bila kufuata taratibu za manunuzi ya umma. Haikosi pia yamempatia 10% ambazo anahofia wapinzani wanafahamu yote.Hayo ndiyo matusi wanayoyaogopa kulikoni ya nguoni.
 
Jiwe mwizi,jiwe muuaji,jiwe ameteka,amepoteza ni dikteta!!hayo ndio matusi!!!
Bahati mbaya kayafany yote hayo,nafsi yake inavuja damu hivyo anataka kujipooza kwa kuwatishia watu nyau.Eti hakuna matusi,hayo wanayomsemea Mh.Mbowe baada ya lile shambulizi yanaitwaje?

Tusidanganyike,jamaa hayupo tayari kukosolewa kwa hoja.Ana stress zake.
 
Rais yupo sawa sheria za nchi zinazuia matusi. Kwa hiyo wanaotukana watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Mfano kifungu cha 89(1)(a)(b) kipo wazi kwamba mtu akitumia lugha kutukana au lugha chafu kiasi cha kuhatarisha amani anafanya kosa. Kwa hiyo matusi na lugha chafu ni makosa msidhani mtapona.
Huyo Pambalu mnafagilia kwa kipi cha maana alichoongea? Kama Budget Act, 2015 kifungu cha 41 kimeweka wazi kuhusu reallocation of funds. Kama budget kubwa ya serikali ilipitishwa alafu yakafanyika mabadiliko ya matumizi ya pesa na kununua ndege au kujenga uwanja Chato tatizo liko wapi?
Ni nani hiyo anayeweza kuamua kama hili ni tusi na hili siyo tusi??

Huo ni mkakati wake tu wa kuwajaza wapinzani magerezani
 
Bahati mbaya kayafany yote hayo,nafsi yake inavuja damu hivyo anataka kujipooza kwa kuwatishia watu nyau.Eti hakuna matusi,hayo wanayomsemea Mh.Mbowe baada ya lile shambulizi yanaitwaje?
Tusidanganyike,jamaa hayupo tayari kukosolewa kwa hoja.Ana stress zake.
Kwa kifupi tuseme kuwa Jiwe hayuko tayari kwa siasa za ushindani.......

Yeye anapenda kusifiwa na kuabudiwa tuu...

Hivi wapinzani kwa mfano wakisema uwanja wa ndege wa Chato, umejengwa bila kuidhinishwa na Bunge, nalo ataliita kuwa ni tusi??
 
Kampeni bila vijembe wapi na wapi. Hata uende Marekani, Uingereza, Ujerumani nk wembe ni huo huo.

Kama yeye anaanza kujihami kwa kuvurunda kwake hiyo haituhusu sisi lkn yeye aelewe kuwa kwenye kampeni watu hawawezi kumsifu kwani kila chama kinataka kiunde serikali sasa wewe ukikaa kumsifia mwanaume mwenzako hiyo serikali utaundaje.
 
Hauna hoja! Rais na CCM mmekuwa dhaifu sana wa kujenga hoja. Na hii imetokana na kudekezwa na dola mnayoitumia vibaya.

Pambalu kama hizo hoja zake zilikuwa nyepesi kwa nini kipindi kilisitishwa!? Vijana wa CCM mmekuwa watoto mayai, ubongo wenu umesinyaa na kuwa kama wa ndege!
We unatumia akili? Yaani sheria inaruhusu kubadili matumizi ya pesa alafu we unataka kushupaza shingo eti nayo ni hoja?
Mbona alipobadili pesa za sherehe za uhuru zijenge Hospital ya Uhuru hamkuhoji? Au sababu mlikuwa hamtaki mkoa wa Geita uwe na kiwanja cha ndege.
 
Back
Top Bottom