Nikitafakari vurumai na vurugu alizowafanyia upinzani na akati yeye na akina Kakurwa, polepole wakitamba kila kona ya nchi wakinadi sera na mafanikio ya malaika lakini amegundua bado kuna mahala hapaja kaa sawa kila wakati anatafuta namna ya kujihami hii inadhihirisha ukweli kwamba mhalifu aweza kimbia hata asipofukuzwa.
Sasa hivi picha za sarakasi zake zote kuanzia utekaji, kupoteza, kupiga risasi, kunyonga, miili ya watu baharini na mitoni etc ktk uongozi wake zinamrudia na kujuta na hakuna muda wa kusahihisha, alijiamini kupita kiasi mbaya zaidi ni pale alipojiapiza kwamba hadi 2020 upinzani hususani CHADEMA hautakuwepo, maajabu ni kwamba upinzani umeimarika kupitiliza.
Hapo alipo anawaza kwama kuna sheria amesahau kuitunga nanukuu, "Wakati wa kampeni hakuna kwenda kwa wananchi wala kuongea na wananchi".
COVID-19 ilipewa nafasi vilivyo ili isambae hadi wananchi kuagizwa kutotumia Barakoa nyumba za ibada zikaendelea kama kawa.
Baada ya Ugonjwa kufeli kuua wengi na kutamalaki, mission impossible ikageuzwa kinyume chake kwamba juhudi za malaika mkuu ndo zimeviondoa virus kumbe ni uwezo wa MWENYEZI MUNGU ili mtu fulani asipate sababu ya kufuta ama kusimamisha uchaguzi
Najua malaika mkuu amenusa hasira za wananchi kuanzia wakulima wa koroshow, kahawa, Pamba, tumbaku etc.
Bila kusahau vijana maelfu kwa maelf waliomaliza level mbalimbali za elimu na kubaki mtaani bila ajira kuanzia serikalini hadi sekta binafsi anatamani awaambie kuwa niliajiri wengi sana ila mliobaki ni wachache hii nayo imebuma baada ya rais kusema alitengeneza ajira Mil. 6 waziri mkuu nae akasema wametengeneza ajira laki 6.
Nikajiuliza hawa watu waliwasiliana au kuna jambo halijakaa sawa? Alifunga watu midomo wasizungumze akawa yeye na kundi lake ndiyo wanatamba kila kona, sasa hivi ndo wamegundua kuwa walikosea kwani hawakupata challenge yoyote wakahisi wapo huru kufanya chochote.
Matokeo yake anaanza kutisha watu "ooh hatutaki matusi tu tumtangulize Mungu mbele" utadhani anania njema kume Chui kavaa ngozi ya kuku. Ngoja tuingie uwanjani na new styles of Pushups.