Rais Magufuli upo sahihi kwa 100% unapothubutu kuhoji ubora wa Chanjo ya Corona

Rais Magufuli upo sahihi kwa 100% unapothubutu kuhoji ubora wa Chanjo ya Corona

Mkuu hapo kwenye Ebola naomba nikukumbushe kuwa wafanyakazi wa WHO walikuwa wanashukiwa na watu wa kongo kuwa wao ndio wanaeneza virusi vya ebola kwa makusudi kiasi kwamba wakawa wanauliwa na raia funzo langu hapo duniani sasa hivi kuna vita ya rasilimali na ndo mana magonjwa kama ebola hayaishi congo na pia ebola ni kirusi cha maabara( man made)...

Maendeleo ya teknolojia leo huyaoni kulinganishwa na siku hizo za polio.

Kwa hiyo mnataka kwanza watu wafe kama walivyokufa enzi hizo na zipite siku kama zile zile za nyakati hizo kabla ya kupata chanjo?

Eboo!

Kukariri kumbe kubaya ndiyo maana kutwa kucha mmekalia kukariri kilomita za urefu wa mabarabara na jumla ya madaraja.

Dunia haiko stagnant mtapwelewa!
 
Kwa chanjo hizo za covid, TFDA ni kama hawana kazi. Kazi yao inafanywa na Africa CDC. Unaletewa chanjo, unapewa makaratasi ya utafiti wao na kuambiwa wachache watu wenu haraka iwezekanavyo. Chanjo yenye haina muda mrefu kabla haijaharibiaka. (Short shelf life).
Acha uongo hawawezi ingilia sovereign ya nchi, mbona Tanzania ilizigomea na hawajaletewa chanjo na ni mwanachama wa WHO
 
Hapa umeandika kisiasa kuliko kiuhalisia, hakuna aliyekataa chanjo, kinachojataliwa ni kupokea chanjo na kuwapa wananchi bila ya sisi wenye kujiridhisha na ubora wa hiyo chanjo.

Hakuna chanjo inayotumika Tanzania ambayo haijapata mikononi mwa wataalamu wetu na kujiridhisha.
Jiwe amekataa chanjo several times unataka useme nin
 
Kwani waliowekeza unafikiri hawakujua watarudisha kwa njia hipi? Why Bill anatajwa sana kwenye issue ata huko kwao kiasi katoka kukanusha?
Chanjo/tiba za kisayansi ambayo watu wameumiza vichwa vyao, pesa nyingi, huwezi zingumzia kimipasho vile, kwani alishindwa nini kusema tu, zitatumika nchini baada ya wataalam wetu kuzizibitisha(kama huo uwezo wanao lakini)ilikuwa inatosha tu, na angeeleweka tu!

Kama ina tatizo mnakuja na findings zenu, za kisayansi!!sasa huwezi kuja tu na kusema eti mbona chanjo ya ukimwi haipo, malaria(cjui nayo ina chanjo)?, eti kwanini wapate ya covid19?!!kweli ina mantic hii??nasema hivi WHO, wameshasema ni chanjo ya lazima ni hutasafiri kwenda nchi nyingine bila kuwa na chanjo, haya TZ, ni kisiwa tuishi humu humu si tunajiweza!!waulize DRC, kilichowakuta kwenye ebola, baada ya kuleta ngojela kama hizi!!eti ni chanjo ya kupunguza population ya wafrika!!na wazungu wakatulia zao!!kuwaangalia!!kilichowakuta hadi chanjo hazikutosha, leo kuna ebola?
Wangekuwa wanatoa msaada bila malipo hapo sawa, lakini nchi iingie gharama kununua chanjo ambayo haijathibitishwa rasmi Kama ndo suluhisho la Covid-19 ni utahira.

Ukiangalia leo kuna makampuni mengi yanadhalisha hizo chanjo za covid lakini muda uliotumika kutengeneza chanjo hizo ni chini ya mwaka mmoja na utengenezaji wake haujapitia taratibu zote za kisayansi kuwa approved Kama chanjo rasmi ya covid-19, hakuna data za kutosha za majaribio yaliyofanyika kujiridhisha Kama hazina madhara kwa binadamu na effectiveness yake katika kuzuia maambikizi ya covid.

Kwa hiyo kinachofanyika leo ni kwamba chanjo inatolewa kwa watu ikiwa ni sehemu ya majaribio ya kuangalia ubora wake na madhara kwa binadamu. Usishangae baada ya muda kutakuwa na evidence nyingi za side effects kwa baadhi ya chanjo na nyingine zitaonekana hazina ubora wa kuzuia maambukizi. Hadi Sasa hakuna chanjo maalumu ambayo imekuwa approved kuzuia covid_19.
 
Aliyetuepushia athari mwaka jana anaweza hata mwaka huu
Sa chanjo ya nn
Me nadhani wao wangekuwa na akili na nia njema wangepeleza wajue siri ya nchi kama Tanzania kutopata athar za Corona sio kuleta chanjo
 
Wangekuwa wanatoa msaada bila malipo hapo sawa, lakini nchi iingie gharama kununua chanjo ambayo haijathibitishwa rasmi Kama ndo suluhisho la Covid-19 ni utahira....
Kwanini hatutengenezi chanjo hapa Tz na kuziuzia nchi zinazougua corona?

Uthubutu ni kutengeneza chanjo na dawa ya corona, siyo kupinga na kuzodoa jitihada za wengine.
 
Sasa kama hamtaki chanjo za Mabeberu, si mtengeneze za kwenu!! Au ndiyo ile ya KUJIFUKIZA ndiyo chanjo mliyo igundua?....
Korona ni spesho case,usibwabwaje tu, fungueni bongo zenu mfikiri nje ya boksi.
 
Acha uongo hawawezi ingilia sovereign ya nchi, mbona Tanzania ilizigomea na hawajaletewa chanjo na ni mwanachama wa WHO
Nadhani unasema kile kile nachosema mimi, Tanzania imegomea mfumo huo wa kulazimishwa chanjo tusio ijuwa madhara yake ya mbeleni. Kenya wameletewa chanjo juzi, leo wameshaanza kudunga watu wao. Hawana uhuru wa kuuliza nini implication ya hiyo chanjo au ni chanjo ngapi mtu anatakiwa kutumia mpaka mwisho wa maisha yake.
 
Nadhani unasema kile kile nachosema mimi, Tanzania imegomea mfumo huo wa kulazimishwa chanjo tusio ijuwa madhara yake ya mbeleni. Kenya wameletewa chanjo juzi, leo wameshaanza kudunga watu wao. Hawana uhuru wa kuuliza nini implication ya hiyo chanjo au ni chanjo ngapi mtu anatakiwa kutumia mpaka mwisho wa maisha yake.

..kwanini Tz hatutengenezi chanjo zetu na kuziuzia nchi zinazougua corona?

..Magufuli hapendi barakoa, unategemea kiongozi wa namna hiyo ataunga mkono chanjo?
 
..kwanini Tz hatutengenezi chanjo zetu na kuziuzia nchi zinazougua corona?

..Magufuli hapendi barakoa, unategemea kiongozi wa namna hiyo ataunga mkono chanjo?
HIvi kwa mtazamo wako chanjo ndio njia pekee ya kupambana na Corona? Mbona wenye chanjo bado Corona inawasubwa?
 
Mwongozo wa serikali ni lazima chanjo zikaguliwe ndani ya nchi kabla ya kuruhusiwa kutumika.
John Mnyika anawata mtoe majibu ya ile chanjo yenu mliyo ifuata kule Madagascar tena kwa ndege ya Serikali. Au ndiyo inawapa viburi baada ya kuinywa kimya kimya?
 
Chanjo/tiba za kisayansi ambayo watu wameumiza vichwa vyao, pesa nyingi, huwezi zingumzia kimipasho vile, kwani alishindwa nini kusema tu, zitatumika nchini baada ya wataalam wetu kuzizibitisha(kama huo uwezo wanao lakini)ilikuwa inatosha tu, na angeeleweka tu!..
Kwenda zako na mawazo mgando hayo..kuna siku watakubebea mke wakwambie wanakuletea wa kizunguzu nyambafu.

Huku mtaani Corona iko wapi? Mnaiona nyinyi tu? Mbona hamjawahi kuomba chanjo ya Malaria?

Hovyo kabisa
 
Salaam Wana JF.

Nianze andiko hili kwa kurejea usemi huu usemao "Africa consumes what it does not produce and produces what it does not consume" Kuna mantiki pana juu ya usemi huu na kinachoendelea kwa sasa dhidi ya chanjo ya Covid 19, Rais wa Tanzania ameibua mjadala mpana ndani na nje ya Tanzania baada ya kuhoji ubora wa chanjo inayoendelea kutolewa kwa sasa kama sehemu ya mapambano dhidi ya Corona, Wapo wanaobeza na kukejeli juu ya kauli ya mkuu wa nchi, lakini ukweli ni kwamba Rais Magufuli yupo sahihi kabisa kuhoji na kutaka kujiridhisha dhidi ya ubora wa chanjo hiyo, kabla haijafanya kazi kwetu na huu ndio uongozi wa kujali na kulinda watu dhidi ya afya zao, Ni Rais Magufuli tu aliyethubutu kuhoji mpaka sasa kwa viongozi wa bara la Afrika, sijasikia mwingine mpaka muda huu.

Ukweli ni kwamba Tanzania sio kuwa tunaishi katika sayari tofauti na hii ya dunia la asha! wala Tanzania sio kisiwa tunahitaji kushirikiana na Wanadunia wenzetu pale inapohitajika kuungana na kupambana kwa pamoja, lakini sio kila kitu kinacholetwa kwetu tukubaliane nacho bila kuhoji na kudadisi faida, athari, ubora na umuhimu wake kwa afya ya binadamu, hata kama wenzetu wameamua kukubaliana na Jambo/kitu hicho. Bahati mbaya tumekuwa na watu wenye kariba tofauti katika jamii zetu wengi wao wakiwa ni wale "wa bora liende na kuthamini cha wazungu vs cha mwafrika" Huu ni utumwa kama ulivyo utumwa mwingine.

Mantiki ipo wazi ukiwauliza wale wote wanaombeza na kumshambulia Rais hasa Watanzania kuwa "Wanauelewa gani juu ya ubora wa hii chanjo wanayoishadadia?" hamna jibu la msingi zaidi ya Wazungu hawakosei na wanajua zaidi ya Mwafrika, Je Waafrika tutajipenda na kujithamini lini? Kwanini tunajibagua na kuona hatufai kwa lolote, nani aliye "tuchawia", Nilitegemea kauli ya Rais Magufuli itaonyesha njia na kumuunga mkono kwa kile alichokihoji badala yake imeonekana kama nongwa na dhambi fulani hivi, huu ni upuuzi kabisa kubeza maono ya viongozi wetu wanaothamini utu wa mwafrika na afya yake kwanza, ni Mara ngapi tunasikia athari ya chanjo tofauti tofauti zinazoletwa Afrika? au nalo hilo hatuna habari nalo, Je ni bora kwenda kuchanjwa tu bila kujua madhara ya hapo badae ya chanjo hiyo? ni bora kuhoji kuliko kutohoji kabisa.

Nilifikri hoja za Watanzania zitakuwa katika upande wa kuhamasisha wanasayansi wetu kutafiti na kutengeneza chanjo dhidi yetu lakini imekuwa tofauti kabisa badala yake tumekuwa vinara wa kushadadia chanjo tusiyoijua A to Z yake ni ipi katika afya zetu, Je liko wapi kosa la Rais Magufuli katika hoja yake dhidi chanjo ya Corona? Kwasababu tunapenda vya uzunguni miaka ya 1996 tuliwai kuingiziwa maziwa ya mbwa" fresh" sokoni na watu wakayatumia bila kuhoji japo badae ilikuja kubainika na kupigwa marufuku, tutangulize maslahi ya Uafrika wetu na tusikubali kupokea kila aina ya huduma bila kuhoji faida na hasara zake.

Deogratias Mutungi



Fanya maamuzi kuongea tu kila siku watu wamechoka na wanakufa. Chadema wakulaumu hayupo mwaka huu!. Kama kuna wanasayansi tuambiwe ni nani anafanya uchunguzi isije ikawa ni maneno tu kila siku. Je wameanza kuchunguza chanjo na wamefikia wapi!! sasa kuandika historia za ajabu ajabu hazisaidii watu wanataka maamuzi.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Chanjo hizi hazijapitia hatua zote!! Zimekuwa fast-tracked!! Zingepitia hatua zote zingetumia miaka 10 kukamilika. Lakini sasa zimetumia miezi 10 tu.
Kwa sababu hiyo maswali yafuatayo hayana majibu:.
Tutajie hatua ipi imerukwa.
 
Chanjo/tiba za kisayansi ambayo watu wameumiza vichwa vyao, pesa nyingi, huwezi zingumzia kimipasho vile, kwani alishindwa nini kusema tu, zitatumika nchini baada ya wataalam wetu kuzizibitisha(kama huo uwezo wanao lakini)ilikuwa inatosha tu, na angeeleweka tu!.
Another moron
 
Back
Top Bottom