Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Tanzania hakuna coronaaa narudia hakuna corona ndiyo maana naona hata apa kwenye hii thread hakuna aliyevaa barakoa,au nasema uongo ndugu zangu?.
 
Kwahiyo hiyo miongozo haifuatwi?
WHO walitangaza maongezeko ya maakambuzi ya korona, kesho yake magufuri akajitokeza hadharani na kumpongeza mgeni toka china kwa kutokuvaa barakoa na kudai korona haipo Tanzania.

Ushuzi ambao wamekuwa wakitoa mawaziri wa afya jaa korona toka mwezi wa kwanza aliukalia kimya, n.k

korona haipukwi kwa kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko ya watu ambayo mpaka sasa serikali haijaikemea kama mwaka jana, hatua ya kwanza ni kuepuka mikusanyiko, barakoa na kunawa kunafuatia.

mpaka sasa wagonjwa wa korona wanakwenda kwenye mahospitali,dispensali randomly, bila serikali kuingilia kati, matokeo yake wafanyakazi wa idara hizo ndio wanaongoza kwa vifo.

tuna ombwe la uongozi.
 
Binafsi huwa namshangaa sana mtu anayemsifia huyu baba, Kinamna fulani ameendelea kuziponda barakoa na ameendelea kushikilia msimamo wake wa yeye na wasaidizi wake kutokuvaa.

Lakini nimeamini serikali zetu za kiafrika hazithamini uhai wa watu wake, kumekuwa na kauli nyingi sana za kulinganisha vifo vilivyotokea kwa wenzetu na hapa kwetu, hii ni tabia ya ajabu kujifariji kwa matatizo ya wenzako kwa kudhani wewe una unafuu, kwanza population ya wenzetu ni kubwa, pia maambukizi yalianzia kule, pia maambukizi ya mwanzo kule yalikuwa makali hivyo ni obvious kule kungekuwa na vifo vingi kuliko huku, kudhani sisi tumependelewa huko ni kujitoa akili. Lakini pia uhai wa mtu hata mmoja unathamani sana, sio kusema sisi wamekufa watu wachache as if hao watu wachache sio kitu, tungechukua tahadhari zote zinazokubalika katika mazingira yetu, then vifo vilivyotokea ingekuwa sahihi kusema viko nje ya uwezo wetu. Hivi ndivyo serikali yoyote au mtu yeyote ambaye ni "responsible" angetakiwa kuwa.

Na hapo matamko yanakuja baada ya korona kupiga ikulu, kwa maana hiyo sisi the common mwananchi tungeendelea kufa hakuna kiongozi angejali na zaidi wangeendelea kuficha tatizo, huyu asingefiwa na swahiba wake wala asingejitokeza kukiri hata haya machache aliyoyapaka rangi. Yawezekana mabeberu hawatupendi kama asemavyo Rais, lakini napata wasiwasi kama yeye anatupenda!
 
Sijasikia je kazungumzia na Nyungu hapo kanisani ama. Nipo Kimamba nalima nyanya Chungu hapa Rudewa.
 
Hata Congo Kuna wakati wanafanikiwa na kuimaliza Ebola na kutangaza kuisha kwa Ebola,na huwa hivyo kweli kabisa.kuna wakati pia huwa inarudi na kuanza kuenea upya.Kwa Tanzania nn Cha ajabu ambacho huelewi!!?? Korona ilikuwepo siku za mwanzo ikadhibitiwa na amini hata ww unalijua,ikaisha..Sasa ukitaka tuendelee kuwaambia watu ipo wakati ilikwisha!!? imeingia kwa Mara nyingine mnaambiwa take self prequation then mnachallenge.shida ya wabongo mmezoea umaarufu wa njaa,magonjwa,ufisadi n.k haya yaki persist mnajisikia burudaaaaniiii na umaarufu kuongelewa katika haya. Mkiongeleshwa Mambo Kama uchumi wa Kati,pigeni kazi hamna kujifungia..mnapata shida kweli kwa brain zenu kuelewa vitu vya msingi.

NB.ni heri uibiwe Mali kuliko uibiwe ubongo.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Huhu baba angesali na kuondoka yaani viongozi wa Tanzania kama vile wameweuka wako kwa denial stage .Hawafahamu kinachorndelea chonde chonde tu wasiwanyime watu wanaoumwa wasilewe dawa hospital wakahamasisha za kienyeji tu tukarudi enzi za KINJEKITILE na vita ya MAJIMAJI
 
Unajua shida kisa alisema mwezi december kuwa hakuna Corona bado unataka kujiaminisha kuwa mpaka sasa ataamini hivo..!! Embu cheza na nyakati kipindi anasema hakuna Corona Tanzania kipondi waziri wa mambo ya nje uchina akiwa hapa..! Zimepita siku ngapi mpaka leo? Umeulizwa leo kwenu kuna msiba ukasema hapana baada ya siku mbili msiba unatokea utapaswa kusema hupo
 
Yaani umesema kweli.kabisa .Mara barakoa za kutoka nje kwani zinapitia wapi je mamlaka zetu kama TBS nk wanafanya nini mpaka hizo barakoa zinaletwa.Mwananchi hata mmoja uhai wake ni wadhamani sana ebu atuambie Taifa limejiandaaje na haya maambukizi ,hospital zina vifaa vya kutosha ,yeye anapataje mrejesho kitoka.ka wataalam.Barakoa ngapi zimezalishwa.Yaani utafikiria katumwa na waganga wa kienjeji sijui miti shamba
Sasa hiyo mitishamba sindio sasa haifanyi kazi watu wanakufa.Yaani naona aibu mimi Rais akiongea aisee
 
Tumeshindwa kumaliza kipindupindu halafu tuiweze Corona...!!

Kilichofanyika ni kuacha kutoa data na upimaji. Mpaka leo pamoja na kudai imerudi bado hauna data za kuonyesja athari zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…