Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Magufuli kupinga watu kuvaa barakoa labda iltaka kumuua.
Screenshot_20210221-101914.jpg
 
Watanzania walikuwa wanasubiri kwa hamu kauli ya Amiri Jeshi Mkuu kuhusu uwepo wa Covid -19.

Wale waliokuwa wanaona soni kuvaa barakoa na kuji sanitize kwa kumuogopa namba moja, waanze mara moja, bila kusahau kuweka sanitize kwenye milango ya ofisi zenu.

Tukifanya kwa pamoja, tutapunguza athari zitokenazo na Covid -19.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Maambukizi yanaanzia mbali sana..kuanzia kwa Dr,nesi,mochwari,waombolezaji

Sasa Kwa hali hii itakuaje?
Maana yake serekali ilipaswa iwe imetoa miongozo kadhaa kuhusiana na kadhia hii ya Corona pamoja na kuisimamia kwa nguvu zote ila wao wanachofanya sasa hivi ni kuziponda barakoa,kuiponda social distancing na kuweka msisitizo katika maombi(Soma paragraph ya 5 katika waraka wao hapo juu).Yaani Tanzania imekuwa ni Taifa la maruwani linaloongozwa na viongozi maruwani!
 
Maana yake serekali ilipaswa iwe imetoa miongozo kadhaa kuhusiana na kadhia hii ya Corona pamoja na kuisimamia kwa nguvu zote ila wao wanachofanya sasa hivi ni kuziponda barakoa,kuiponda social distancing na kuweka msisitizo katika maombi(Paragraph ya 5 katika waraka wao hapo juu).Yaani Tanzania imekuwa ni Taifa la maruwani linaloongozwa na viongozi maruwani!
Mungu mwenyewe kwenye maandiko anakanya upumbavu na kukosa akili.akisisitiza binadamu atumie maarifa na ufahamu.

Kama si maarifa na ufahamu tuliyopewa tuyatumie Leo ingekuwa hata mtu akiumwa kichwa badala ya kunywa maji mengi na panadol anakaa anamlilia Mungu kichwa kipone.
Kesho akigongwa na nyoka badala ya kutumia maarifa kutoa sumu na kuizuia anakaa anamlilia Mungu

Ni nani angebaki Leo kama ingekuwa hivi?

Bado binadamu anahitaji kutumia maarifa katika tatizo lolote huku akimuomba Mungu amsaidie
 
Hivi Mwalimu Nyerere alishapanda madhabahuni ST. Peters kutoa hotuba au popote kanisa Katoliki
Ngoja tuwaulize akina Mzee Warioba na Mzee Butiku manake huyu balaa kwa makamera
 
He is now coming to his sense.

Alikuwa anawasifia watu wasipovaa barakoa sasa akili inaanza kumrudia.

Alisema corona haipo sasa akili inamrudia kuwa huu msala upo na hauna utani.
Mkuu, nimesikiliza clip alichosema tofauti na kilichoandikwa naomba nenda kasikilize. Amewasifu wale ambao hawajavaa barakoa na kuwasifu waziri mkuu na makamu wa rais kutovaa barakoa kwa kuwa wanamuamini Mungu.

Amesema barakoa sawa ila tununue za hapa na kushonesha lakini walizozileta hizo barakoa anazosema kila leo zina corona ziliingia vipi nchini na madukani?

Hotuba ukiisikia kwa kweli ni ya kebehi kwa ugonjwa na wavaa barakoa. Naomba kamsikilize mwenyewe m, iko YouTube ni hotuba fulani hujui anataka kusema nini anaacha watu grey zone, hakuna message moja anauma na kupuliza. Inasikitisha kiongozi kuongea vile.

Kuna sehemu kasema “Hawa wasaidizi wangu hawajavaa barakoa na mimi sijavaa, kwani siogopi kifo? Wala sijui wamekutana na nani lakini naamini Mungu. Nchi nyingi waliovaa barakoa ndio wamekufa maelfu.” Sasa ni ujumbe gani kapeleka?

Hiyo statement wame soft baadhi ya maneno, kamsilize mwenyewe halafu uta comment.
 
Hivi Mwalimu Nyerere alishapanda madhabahuni ST. Peters kutoa hotuba au popote kanisa Katoliki

Mwalimu na Mkapa kusali kwao kote St. Peters na St. Imaculate Upanga, hata siku moja hawajawahi kupanda madhabahuni na kuhutubia. Hata kutoa Press baada ya misa hawajahi kufanya.

Hata siku moja huwezi kuona wanaenda kanisani na ma-camera.

Ni wasomi wanaoelewa kanisani ni jambo lao binafsi lisilohusiana na siasa/serikali.

Ushamba ni tatizo sana.
 
Yeye kama kiongozi anatakiwa awe mfano kwa anaowaongoza kwa kuvaa barakoa ili kuonesha msisitizo.
Namshauri na yeye avae......huwezi kuleta kiburi kwenye Corona otherwise itamng'oa.
Nimesikia alichoongea kwa kweli ni bora hata akalie kimya jambo hili watu wajiamulie wenyewe ila ni hotuba fulani imekosa uwajibikaji. unapo ongea jambo kubwa kama hili ni vizuri lika base katika facts sio personal opinion.
 
Back
Top Bottom