Viongozi wa nchi hii, hasa Rais mwenyewe, wanaongoza kutuchanganya wananchi sana. Hatujui wanalipeleka wapi taifa. Hawa watu sijui vipi.
● Mwezi mzima wanaropoka "NCHI HII HAINA CORONA", na wana aminisha raia kwa kutokuvaa barakoa wala kuzingatia mita moja ya kujiepusha katika mikusanyiko yao, wengine walifikia hatua ya kuvua wenzao barakoa kwa nguvu kisa mamlaka.
● Viongozi wengine walienda mbele zaidi na kusema ni "SHULE YA ISM MOSHI KUTANGAZA INA WANAFUNZI WAWILI WAMEKUTWA NA CORONA NI YA UONGO, HIO NI VITA YA KIUCHUMI".
● Wengine kama Makamu Mkuu Wa Chuo Cha Open University baada ya kutoa wito kwa wanafunzi kujihadhari na kuchukua hatua stahiki kujilinda na Corona, aliamrishwa na Wizara Ya Elimu "AOMBE RADHI KWA KUTOA WITO ULE", zaidi ya yote Mkuu wa chuo nae akamruka hatua 100 na kusema sio wito wa chuo, ni wito wake yeye binafsi.
● Leo Wizara ya Afya inaomba wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona, kwa kunawa na maji tiririka na kuvaa barakoa. Wakati wao ndio walikua vinara kupinga kuwepo kwa Corona nchini, licha ya wananchi kupiga kelele kwa kupoteza wapendwa wao.
● Sasa tunasikia mkuu wa nchi akitoa wito wa "MAOMBI SIKU TATU YA KUMWOMBA MUNGU KWAAJILI YA KULIOMBEA TAIFA".
"MUNGU GANI ATAKAESIKIA MAOMBI YA TAIFA LENYE VIONGOZI WASIO WAKWELI NA WANAFIKI???? SI VIONGOZI WA DINI WALA WA NCHI" Kuomba huko ni sawa na maombi yaliofanywa na watu wa Sodoma Na Gomora baada ya ahadi ya adhabu ya mungu kuwafika, saa ilipofika ilifika, milango ya maombi na dua ilifungwa, na adhabu haikuchagua watoto wala wazee.