Mkuu, nimesikiliza clip alichosema tofauti na kilichoandikwa naomba nenda kasikilize. Amewasifu wale ambao hawajavaa barakoa na kuwasifu waziri mkuu na makamu wa rais kutovaa barakoa kwa kuwa wanamuamini Mungu.
Amesema barakoa sawa ila tununue za hapa na kushonesha lakini walizozileta hizo barakoa anazosema kila leo zina corona ziliingia vipi nchini na madukani?
Hotuba ukiisikia kwa kweli ni ya kebehi kwa ugonjwa na wavaa barakoa. Naomba kamsikilize mwenyewe m, iko YouTube ni hotuba fulani hujui anataka kusema nini anaacha watu grey zone, hakuna message moja anauma na kupuliza. Inasikitisha kiongozi kuongea vile.
Kuna sehemu kasema “Hawa wasaidizi wangu hawajavaa barakoa na mimi sijavaa, kwani siogopi kifo? Wala sijui wamekutana na nani lakini naamini Mungu. Nchi nyingi waliovaa barakoa ndio wamekufa maelfu.” Sasa ni ujumbe gani kapeleka?
Hiyo statement wame soft baadhi ya maneno, kamsilize mwenyewe halafu uta comment.