Mimi naweza kusema kwamba Covid-19, Coronavirus outbreak haijatokana na watu kukosa unyenyekevu kwa Mungu.
Kwa sababu Mungu hayupo. Kama unabusha, thibitisha factually, factually, the emphasis is on factyually, kwamba Mungu yupo in the first place.
Ila, nataka niseme, pamoja na kuwa mtu nisiyeamini habari za uwepo wa Mungu, nakubali kwamba habari ya Mungu kuwapo ina currency.
Si lazima kitu kiwepo, au kiwe kweli, ili kiwe na umuhimu. Mengine tunajiwekea tu watu.
Ile noti ya Sh 10,000 au USD 100 ina thamani swa na vitu inavyonunua?
Ikija kuwepo lockdown ya nguvu ya kuodnoa umuhimu wa central bank na national economies, kiasi kwamba hela inageuka karatasi tu, noti ya 10,000 Sh itakuwa na thamani tena?
Magufuli akisema leo tunawapa mwezi mmoja kubadili noti, baada ya mwezi mmoja, noti ya 10,000 itakuwa haitumiki, baada ya mwezi mmoja, hiyo noti ya 10,000 itakuwa na thamani tena?
Jibu ni wazi. Noti ya 10,000 sh ina thamani kwa sababu tumekubaliana iwe na thamani, tukikataa mkataba huu, thamani yake itashuka na kutoweka.
Can anyone prove that the 10,000 banknote actually has the value of the goods it buys?
Can anyone prove that an all knowing, all good and all capable God exists?
Inawezekana kwamba dhana ya kuamini Mungu ina maana kubwa tu.
Ukifuata kanuni za kula vyakula zilizopo katika Biblia, kwenye vitabu kama vya Mambo ya Walawi, inawezekana ukapata busara za miaka na miaka za watu kuhusu chakula gani kinafaa kuliwa na hakifai kuliwa.
Hilo tu linaweza kukufanya ujue kwamba popo, anayesababisha Coronavirus, inayoleta Covid-19, hafai kuliwa.
Pengine wenzetu walishawai kujaribu kula wanyama jamii ya popo, mamia na mamia, maelfu na maelfu ya miaka huko, wakaona watu wakila popo wanakufa sana. Wakaweka sheria za kukataza kula popo. Au wakaweka sheria za kukataza kula vitu vigeni ambavyo havijajulikana madhara yake.
Na kwa kuwa hawakuwa na namna ya kuwapa watu hofu ya kutokula vitu hivi, wakasema tu kwamba "hii ni sheria ya Mungu".
Hiyo ni shortcut. Ni uongo unaotaka kwenda kwenye ukweli.
Ni uongo kwa sababu hakuna Mungu. Ni ukweli kwa sababu unakufanya usitende mabaya yatakayokudhuru.
Kuna sheria za Mungu zinazokataza kuzini. Mtu akizifuata hizi, ataepuka matatizo mengi sana katika maisha, mengi sana.
Napenda kuziheshimu sheria hizi, si kwa sababu naamini Mungu kaziweka.
La hasha, mimi siamini uwepo wa Mungu.
Naziheshimu kwa sababu, ni sheria ambazo zinaweza kuniepusha na magonjwa ya zinaa, na mifarakano ya kijamii, na mengine mengi kama hayo.
Kuna mambo mengi kama hayo, ambayo, kwa watu wa kawaida, kufuata shortcut ya kuamini Mungu na kuishi kwa sheria zake kunaweza kuwa kunatosha.
Lakini kuna wengine wabishi tunataka tuziangalie hizo shortcuts kama bado zina maana au zimepitwa na wakati?