#COVID19 Rais Magufuli yupo sahihi sana kuhusu COVID-19

#COVID19 Rais Magufuli yupo sahihi sana kuhusu COVID-19

Ndugu zangu

kwanza niwape pole waathirika wote na wafiwa wa ugonjwa wa corona ndo mapito tuwe na imani corona itaondoka, ila itaondoka pale tu sisi binadamu tutakapokuwa wanyenyekevu mbele ya Mungu

Hii corona ni pigo kutoka kwa Mungu kwa sababu sisi wanadamu ni washenzi tumezidi maasi na machafu tumeifanya dunia uwanja wa vita ushoga mauaji na ufedhuli mwingi, hili janga la corona ilibidi lazima lije tumemsahau sana Mungu katika matendo yetu na shetani amekuwa ni rafiki yetu na sasa shetani kama kawaida yake ametuacha na tunazidi kupotoka kwa kuendeleza mambo yasiompendeza Mungu

Baada ya Rais Magufuli kusema tumrudie Mungu atusaidie kwa hili janga la corona watu wengi walimkejeli sana, ila kiukweli alikuwa sahihi iwe kwa lock down isiwe kwa lock down corona itaendelea na ingeendelea kututesa sana, sababu corona haijaletwa na mchina wala mmarekani wala popo isipokuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa sababu ya matendo yetu, wanasayansi waendelee kukesha maabara kutafuta dawa ila wasisahau dawa ya corona ni sisi binadamu kumrudia Mungu

Tulipoombwa na Rais tufanye maombi watu walibeza ndo hao hao sasa corona imetamalaki wanapiga kelele wakati siku za maombi walikuwa juu ya vinena vya malaya!! mtu anafikia hadi kusema dini haina umuhimu kwa sababu haijatusaidia kuondoa corona, corona iondoke hali ya kuwa mmeasi??subirini ya Nabii Nuhu na Luti yatufike ndo mtajua hamjui

Na nyie mnaoenda mbali zaidi na kusema Mungu hakuna, mkishikwa na haja mbona mnaenda vyooni kuchutama, mnachutama for what?????gomeni basi na kuchutama kama nyie ni vidume kweli!!! ndo nyie mmesababisha kutuletea corona, kwani kawaida ya Mungu kosa la mtu mmoja anaweza akaleta janga katika jamii nzima Kiranga aretasludovick Retired Father of all Snipers The only nusuhela na wafuasi wenu wote mnaopotosha watu ni mda wenu wa kutubu ile saa imekaribia TUKIENDELEA KUMBEZA NA KUMDHIHAKI MUNGU CORONA ITAENDELEA KUTUTAFUNA

View attachment 1435930

Dawa ya corona ni kuendelea kuomba sana wote kwa umoja Mungu atatusamehe na kutuonyesha njia sahihi ya kukabiliana na haya maradhi na tena tuombe majumbani kwetu tuepuke mikusanyiko isiyo na lazima,
Italia makao makuu ya Roman Catholic,, Mama Reakatale wa mlima wa moto!...Nenda kaombe hujazuiwa ,,,
 
Kiranga ili tukuthibitishie uwepo wa Mungu hebu thibitisha wewe kwanini unaamini kuwa Mungu hayupo. Maana you are just one in a million.Isije ikawa elimu yako unayozani ni sahihi kumbe pengine ss tulishaisoma na kuipuuza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani ni contradiction.

Unaelewa hilo?
 
Nakukumbusha ndugu yangu kiranga sababu nakupenda sana

Mungu yupo Mkuu tubu

Sijatoa hili bandiko sababu ya kubishana na yeyote kuhusu uwepo wa Mungu, kwanza sasa naona ni kufuru sababu watu washabishana sana humu jukwaani, mie naamini hutakubali hoja yeyote ntakayokueleza hapa utakuja na blah blah zako hapa za ubishi,binadamu anakishinda kila kitu/kiumbe kwa ubishi kwa maneno yake Mungu.
HAKUNA KULAZIMISHANA KATIKA DINI KAMA UNAENDELEA NA UBISHI WAKO ENDELEA LAKINI JUA UMEPOTEA

Nimekukumbusha tu mkuu huko uliko siko jitafakari
Nimeomba uthibitisho.

Wewe unahubiiri.
 
Waafrika shida kama hizi zitatuzindua maana bado tumelala fofofo
Inawezekana uko sahihi.

Ukiangalia maendeleo makubwa ya kisayansi Ulaya yalikuja baada ya watu kuzinduka kutokana na vifo vingi vya "The Black Death", watu wakapunguza imani za ajabu na kukimbilia kutafuta majibu ya kisayansi kutatua matatizo yao.

Kabla ya hapo hakukuwa na tofauti kubwa kimaendeleo kati ya Ulaya na Afrika.

Kuanzia hapo Ulaya ikaiacha sana Africa kimaendeleo.
 
And I believe we have many solutions around us as Africans. Shida yetu tuko kwenye dunia ya copy and paste. Hatutaki kujiongeza. Hatutaki kuhangaisha vichwa
 
Maisha yote yako hivyo.We are always supposed to be doing research and development.Unfortunately (or fortunately) we are all human, and we require resources and focus.

Corona ina intensify tu yote ya kawaida katika maisha.Kama Tanzania au Marekani tuna lack of leadership ambayo inafichika kirahisi under normal circumstances,Corona inakuja kufichua weaknesss zote. Kuanzia kuua wazee wenye kisukari, mpaka marais ambao hawana crisis management systems.

Swali kubwa zaidi ni hili.

Je, sisi huko Tanzania na Afrika tunaweza kuchambua, kugundua na kupambana na matatizo kivyetu ikibidi?

Mkuu,
Pole sana kwa kuondokewa na Mzee wako Mahiga
 
Hahaha eti 1 in a million. Hata statistics hujui. Watu tusioamini uwepo wa mungu tupo wengi mno. Nchi za kimasikini tu ndo mmejaa mnaoamini huu upuuzi. Nchi nyingi zilizoendelea ukifuatilia utakuta 50% hawaamini uwepo wa mungu. Ondoa za waarabu za kiislamu maana na zenyewe wamejaa ukilaza wao.

Alafu kuprove mlivyo vibaya kichwani, we ndiyo unasema mungu yupo wewe si ndiyo unayetakiwa kuprove kua yupo? Kwa nini asiyeimini aprove kua hayupo? Kwani umemuona? Hahaha akili ndogo mnashangaza toka lini mtu anaprove kitu kutokuwepo?

Nikija kwako umekaa sebuleni nikakwambia kuna simba sebuleni we ukasema hayupo kwa sababu hujamuona anayetakiwa aprove kua simba yupo si ni mimi? Umezaliwa na ubongo utumie.

Alafu nyie waamini mungu jifunzeni spelling mbona hua mnachanganya sana h, r,l, dh, z. Wengi akili ndogo naona. Hata mi nasubiri siku mtu aprove mungu yupo, kuanzia siku hiyo nitakua muumini namba moja.
Asante sana kwa kuona mwngi.

Mtu hata hana statistics anakuja na "alternate facts" zake hata kuanza kujadikiana naye tabu.

Maana haheshimu hata statistics, sasa unajadiliana naye vipi?

Anaweza kukulazimisha kwamba wewe unaamini Mungu, wakati huamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu

kwanza niwape pole waathirika wote na wafiwa wa ugonjwa wa corona ndo mapito tuwe na imani corona itaondoka, ila itaondoka pale tu sisi binadamu tutakapokuwa wanyenyekevu mbele ya Mungu

Hii corona ni pigo kutoka kwa Mungu kwa sababu sisi wanadamu ni washenzi tumezidi maasi na machafu tumeifanya dunia uwanja wa vita ushoga mauaji na ufedhuli mwingi, hili janga la corona ilibidi lazima lije tumemsahau sana Mungu katika matendo yetu na shetani amekuwa ni rafiki yetu na sasa shetani kama kawaida yake ametuacha na tunazidi kupotoka kwa kuendeleza mambo yasiompendeza Mungu

Baada ya Rais Magufuli kusema tumrudie Mungu atusaidie kwa hili janga la corona watu wengi walimkejeli sana, ila kiukweli alikuwa sahihi iwe kwa lock down isiwe kwa lock down corona itaendelea na ingeendelea kututesa sana, sababu corona haijaletwa na mchina wala mmarekani wala popo isipokuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa sababu ya matendo yetu, wanasayansi waendelee kukesha maabara kutafuta dawa ila wasisahau dawa ya corona ni sisi binadamu kumrudia Mungu

Tulipoombwa na Rais tufanye maombi watu walibeza ndo hao hao sasa corona imetamalaki wanapiga kelele wakati siku za maombi walikuwa juu ya vinena vya malaya!! mtu anafikia hadi kusema dini haina umuhimu kwa sababu haijatusaidia kuondoa corona, corona iondoke hali ya kuwa mmeasi??subirini ya Nabii Nuhu na Luti yatufike ndo mtajua hamjui

Na nyie mnaoenda mbali zaidi na kusema Mungu hakuna, mkishikwa na haja mbona mnaenda vyooni kuchutama, mnachutama for what?????gomeni basi na kuchutama kama nyie ni vidume kweli!!! ndo nyie mmesababisha kutuletea corona, kwani kawaida ya Mungu kosa la mtu mmoja anaweza akaleta janga katika jamii nzima Kiranga aretasludovick Retired Father of all Snipers The only nusuhela na wafuasi wenu wote mnaopotosha watu ni mda wenu wa kutubu ile saa imekaribia TUKIENDELEA KUMBEZA NA KUMDHIHAKI MUNGU CORONA ITAENDELEA KUTUTAFUNA

View attachment 1435930

Dawa ya corona ni kuendelea kuomba sana wote kwa umoja Mungu atatusamehe na kutuonyesha njia sahihi ya kukabiliana na haya maradhi na tena tuombe majumbani kwetu tuepuke mikusanyiko isiyo na lazima,
Ni kweli binadamu tumezidi maasi na machafu na miongoni mwa wanaoongoza kwa machafu ni yeye mwenyewe. Hivyo aanze yeye kutubu na kuomba msamaha kwa aliowasababishia mateso ndipo tutaamini kweli anmanisha anachoongea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naweza kusema kwamba Covid-19, Coronavirus outbreak haijatokana na watu kukosa unyenyekevu kwa Mungu.

Kwa sababu Mungu hayupo. Kama unabisha, thibitisha factually, factually, the emphasis is on factually, kwamba Mungu yupo in the first place.

Ila, nataka niseme, pamoja na kuwa mtu nisiyeamini habari za uwepo wa Mungu, nakubali kwamba habari ya Mungu kuwapo ina currency.

Si lazima kitu kiwepo, au kiwe kweli, ili kiwe na umuhimu. Mengine tunajiwekea tu watu.

Ile noti ya Sh 10,000 au USD 100 ina thamani sswa na vitu inavyonunua?

Ikija kuwepo lockdown ya nguvu ya kuondoa umuhimu wa central bank na national economies, kiasi kwamba hela inageuka karatasi tu, noti ya 10,000 Sh itakuwa na thamani tena?

Magufuli akisema leo tunawapa mwezi mmoja kubadili noti, baada ya mwezi mmoja, noti ya 10,000 itakuwa haitumiki, baada ya mwezi mmoja, hiyo noti ya 10,000 itakuwa na thamani tena?

Jibu ni wazi. Noti ya 10,000 ina thamani kwa sababu tumekubaliana iwe na thamani, tukikataa mkataba huu, thamani yake itashuka na kutoweka.

Can anyone prove that the 10,000 banknote actually has the value of the goods it buys?

Can anyone prove that an all knowing, all good and all capable God exists?

Inawezekana kwamba dhana ya kuamini Mungu ina maana kubwa tu.

Ukifuata kanuni za kula vyakula zilizopo katika Biblia, kwenye vitabu kama vya Mambo ya Walawi, inawezekana ukapata busara za miaka na miaka za watu kuhusu chakula gani kinafaa kuliwa na hakifai kuliwa.

Hilo tu linaweza kukufanya ujue kwamba popo, anayesababisha Coronavirus, inayoleta Covid-19, hafai kuliwa.

Pengine wenzetu walishawai kujaribu kula wanyama jamii ya popo, mamia na mamia, maelfu na maelfu ya miaka huko, wakaona watu wakila popo wanakufa sana. Wakaweka sheria za kukataza kula popo. Au wakaweka sheria za kukataza kula vitu vigeni ambavyo havijajulikana madhara yake.

Na kwa kuwa hawakuwa na namna ya kuwapa watu hofu ya kutokula vitu hivi, wakasema tu kwamba "hii ni sheria ya Mungu".

Hiyo ni shortcut. Ni uongo unaotaka kwenda kwenye ukweli.

Ni uongo kwa sababu hakuna Mungu. Ni ukweli kwa sababu unakufanya usitende mabaya yatakayokudhuru.

Kuna sheria za Mungu zinazokataza kuzini. Mtu akizifuata hizi, ataepuka matatizo mengi sana katika maisha, mengi sana.

Napenda kuziheshimu sheria hizi, si kwa sababu naamini Mungu kaziweka.

La hasha, mimi siamini uwepo wa Mungu.

Naziheshimu kwa sababu, ni sheria ambazo zinaweza kuniepusha na magonjwa ya zinaa, na mifarakano ya kijamii, na mengine mengi kama hayo.

Kuna mambo mengi kama hayo, ambayo, kwa watu wa kawaida, kufuata shortcut ya kuamini Mungu na kuishi kwa sheria zake kunaweza kuwa kunatosha.

Lakini kuna wengine wabishi tunataka tuziangalie hizo shortcuts kama bado zina maana au zimepitwa na wakati?
Yaani popo amekuwa akisingiziwa sana na binadamu hapa duniani. Ebola walisema alisababisha Popo sasa Corona naye wanasema Popo kwetu kijijini Popo wanasema ni mchawi. Jamani acheni kumsingizia Popo mrudieni Mungu mwache madhambi yaliyokithiri duniani kama vile kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo ni kosa kubwa sana ndiyo maana hata SODONA NA GOMOLA zilifutwa! Huu ugonjwa wa corona utaisha kama binadamu tutamrudia Mungu tu Wanasayansi wameshindwa!
 
Ni kweli binadamu tumezidi maasi na machafu na miongoni mwa wanaoongoza kwa machafu ni yeye mwenyewe. Hivyo aanze yeye kutubu na kuomba msamaha kwa aliowasababishia mateso ndipo tutaamini kweli anmanisha anachoongea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acheni ufirauni ndiyo kosa kubwa sana ambalo limekuwa linawaangamiza binadamu duniani tangu zamani
 
Waziri mmoja ameshapukutika huko. Mapambio yaendelee. Ila kuna siku mtajua kuwa mlikuwa mnaandika ujinga.
wewe ulinadhani kuna mtu ataishi milele

sie tu tunaobaki tunakua na huzuni ila hatujui tu wakati mwingine kifo kwa marehemu ni bora kuliko karaha za ulimwengu

mahiga katangulia mimi ntafuata wewe utafuata hakuna kitakachobaki chini ya jua
 
Acheni ufirauni ndiyo kosa kubwa sana ambalo limekuwa linawaangamiza binadamu duniani tangu zamani
Magufuli lilikuwa chaguo la Mungu, ni imani ya hali ya juu Rais kuwataka watu wamrudie Mungu kwenye majanga

wapagani hawawezi kuelewa hili
 
Yaani popo amekuwa akisingiziwa sana na binadamu hapa duniani. Ebola walisema alisababisha Popo sasa Corona naye wanasema Popo kwetu kijijini Popo wanasema ni mchawi. Jamani acheni kumsingizia Popo mrudieni Mungu mwache madhambi yaliyokithiri duniani kama vile kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo ni kosa kubwa sana ndiyo maana hata SODONA NA GOMOLA zilifutwa! Huu ugonjwa wa corona utaisha kama binadamu tutamrudia Mungu tu Wanasayansi wameshindwa!
Thibitisha Mungu yupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndipo ninapowaona buku 7 mapunguani. Yes hatuishi milele. Ila hilo halitufanyi tushindwe kujilinda.

Hao wabunge wameona posho ni tamu kuliko afya zao. Eti wanamuogopa jiwe.

Waendelee tu na vikao watapukutika wengi tu halafu watakuwa wanasema ni mipango ya mungu wakati ni ujinga wao.
wewe ulinadhani kuna mtu ataishi milele

sie tu tunaobaki tunakua na huzuni ila hatujui tu wakati mwingine kifo kwa marehemu ni bora kuliko karaha za ulimwengu

mahiga katangulia mimi ntafuata wewe utafuata hakuna kitakachobaki chini ya jua
 
Hapa ndipo ninapowaona buku 7 mapunguani. Yes hatuishi milele. Ila hilo halitufanyi tushindwe kujilinda.

Hao wabunge wameona posho ni tamu kuliko afya zao. Eti wanamuogopa jiwe.

Waendelee tu na vikao watapukutika wengi tu halafu watakuwa wanasema ni mipango ya mungu wakati ni ujinga wao.
hakuna mtu anakufa kwa ujinga wake wala hakuna anaebaki kwa werevu wake

mie imani yangu iko hivyo ila sikulazimish kuamin mkuu
 
Back
Top Bottom