Rais Magufulli hawazii tena kuleta maendeleo ya Nchi ya Tanzania

Rais Magufulli hawazii tena kuleta maendeleo ya Nchi ya Tanzania

Mkuu Salary Slip kwa kufukunyua uzi huu utakuwa umewaka kilimi-limi walokunanga mwaka 2019. Hata wale praise team wanazisoma namba kama sie tu.
 
Kweli maendeleo ni yeye pengine ndiyo maana wanaonufaika ni yeye na wale walioko kwenye spheres zake. Sisi wale wa peripheral mmmh tunasubiri kuhadithiwa tu kwamba uchumi wetu unakuwa kwa kasi ya Dreamliner, labda ninyi huko akina MAYALA, lakini sie akina NYANZALA hali ni mbaya tumebaki tu kuganga njaa kama majina yetu.
 
Umeandika mengi sana... lakini ujue huu utawala umejaa kiburi na dharau... ma ukionekana mjuaji sana ndiyo hivyo tena...

Ngoja tuone...


Cc: mahondaw
 
kt the irreplaceable,
Hoja zangu hata moja hujajibu, tax base unaona kaimarisha? Politically au practically? Sikujui how analytical you are, ila ungekuwa 5% tuu usingeandika haya!

Hebu nielezee TRA wanakusanya vizuri na bandari iko full operational as per you choir singers? Hebu uniambie what are you doing for your earning? Unafanya biashara kama sie au unafanya kazi,(muajiliwa) au kula kulala?

Ungekuwa mfanyabiashara ungeelewa concept za kufungua hotel na kutegemea uteja mkubwa wa serikali and that is done throughout the entire world, wewe unaunga mkono. Kikwete alilitangaza hilo na kuliannzisha ili kuimarisha uwekezaji katika hospitality industry ili watuwengi wawekeze mahotel na wasipate hasara ila in a long run wawezeshe influx ya watalii, at least that is charisma! Wewe unaota na kuna vingine!

Kodi na hiyo tax base you and me we aren't sure of kwakuwa serikali hii imejaa propaganda, ukweli mwiko, mfano bwamkubwa alilitibua la sukari ikapanda kutoka 1500 mpaka 5000 two years baadae anasema alikuta sukari 5000 na nadhani wewe na wenzio uliliamini, nakushauri uwe na references za kutosha kabla ya kuongelea jambo, and that is what we Tanzanians are lacking!!!

Kuhusu utendaji serikalini my research tells me ni mwamko na fikra za wafanyakazi tuu, they thought wako kwenye rhythm nyingine tuu, that is why mawilayani walibomoa nyumba hivyo to fit in the rhythm na ninauhakika hakuamuru hilo, lakini ukweli ni kwamba he isn't at all kama hivyo! Don't expect something new kwa obvious certain characters like upendeleo, ubaguzi na kupenda sifa!

We need ones charisma, sio propaganda Mkuu!
 
Nimekuuliza wakati wa kikwete ni nini nchi ilinufaika? Narudia tena vitu anavyofanya rais havina impacts za haraka hivo, mpaka leo projects zote hazijakamilika anzia ndege, reli, umeme nk. Hivyo huwez ukamjaji mapema hivyo.....

Takwimu zinaonesha, ni katika awamu ya tano tu ndo tuliweza kukusanya mapato hadi ya trilioni moja per month, na hii ilitokana na kuzuia baadhi ya michezo michafu pale bandarini.

Toa majibu hata mistari miwili tu, ni wapi rais amekosea na awamu zilizopita zilifanya nini ambacho kinaweza kua ni "legacy" mpaka kesho. Suala la mimi kula kulala achana nalo....
 
britanicca,
Magufuli yule waziri wa ujenzi ni tofauti sana na magufuli huyu rais wetu.Yule wa ujenzi alikuwa magufuli hapa kazi tu,huyu wa leo ni magufuli hapa siasa tu tena siasa zenyewe siasa uchwara,Magufuli huyu wa leo anaonesha uwezo mdogo kwenye kila idara especially kwenye leadership and managment, .magufuli huyu wa leo anaamini sana katika matumizi ya nguvu kuliko akili,mbaya zaidi kaikumbatia ccm kuliko hata waasisi wa ccm wenyewe, may be kwa kuwa akina mwandosia walimwambia hajawahi kuwa hata balozi wa nyumba kumi wa ccm so anataka kuwaproove wrong kwa kuamua kuwa mfia ccm kuliko nchi yetu.

Finally baada ya kuona utamu wa kukaa ikulu akageuza,priority,sasa priority yake kubwa ni kulinda madaraka yake na genge lake aliloliteua katika nafasi mbali mbali,maendeleo si ajenda tena bali madaraka,ndo maana anapenda kusikia mzuri yanayomhusu yeye na mabaya yanayowahusu wapinzani wake,LISSU alipigwa risasi kwa kusema ukweli,ila uroho wa madaraka wa watawala wetu umempa kilema cha kudumu.Mungu ikimpendeza atatuondelea kikombe hiki
 
Unamtaka Makongoro?
Bongo za watu wa CCM zimechoka kuongoza hii nchi, wanachowaza ni kula tu. Na ndiyo maana kina Bashite wanaikimbiza nchi wanavyotaka.
Tunahitaji mapinduzi ya jumla akili za CCM zipumzike ziingie fikra mpya.
CHAMA CHAKO CHA CCM NI KANSA INAYOITAFUNA TANZANIA.
naunga mkono hoja,na ninapendekeza kuiondoa ccm kwa kutumia nguvu si kura
 
kt the irreplaceable,

Kwani serikali inajadili vipaombele vya wananchi au inatekeleza vipaumbele vya rais katika kusaka kiki za kisiasa? Mfano mrahisi tulisema nguvu iwekezwe kwenye kilimo kabla ya ndege, je hilo lilizingatiwa? Hizo ndege hivi leo anaweza kutokea mtu na kuonyesha kweli zipo kwa faida zaidi ya political millage?
 
Crimea,
Kama angekuwa anajenga hiyo msingi Point yako ingehold water sasa huyu hajengi bali anapomoa hata ile msingi legelege iliyokuwepo kutokana kuwa incompetent person huku akijifanya anajua wakati hajui,Nitawashangaa na dunia itatushangaa huyu akirudi madarakani 2020
 
kt the irreplaceable,
pole sana,ile bure umeiona wapi? na kuna nini huko wanachopata watoto wetu? walimu wenyewe pamoja na mishahara yao midogo watoto wao wapo private school
 
kt the irreplaceable,

Pointi yako namba nne, hizo ndege zake zimekuza utalii upi? Hizo ndege zinaenda nchi ipi ambayo imeleta watalii mpaka sasa? Acha siasa mfu boss.

Hiyo pointi yako namba 5, kinachowakuta hao kina Seth ni uonevu wa wazi kutokana na matumuzi mabaya ya madaraka na wala sio vita ya ufisadi. Hao wawili wako ndani sio kwa hukumu ya mahakama bali kwa amri ya rais, iweje hao wawili tu ndio wawe jela huku chain ya viongozi wa serikali walioshirikiana nao wakiwa nje? Kajipange tena.
 
Kukusanya mpaka trilioni imekuja baada ya vyanzo vya halmashauri kuhamishiwa serekali kuu. Kwenye utetezi wako uwe na kumbukumbu ya hilo. Halafu kwenye serekali inayopika data huwezi kuamini figures za makusanyo yake.
 
Back
Top Bottom