Rais mfute Abubakari Kunenge Ukuu wa Mkoa. Mrudishe Makonda Tafadhali

Rais mfute Abubakari Kunenge Ukuu wa Mkoa. Mrudishe Makonda Tafadhali

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
14,762
Reaction score
32,386
Karibia week ya pili au Tatu.hatujasikia TAMKO LOLOTE TOKA KWA MKUU WA MKOA. Hakuna watu waliobagazwa au garagazwa. Mkuu wa Mkoa gani Kapoa kama supu ya sangara isiyo na ndimu?

Sisi wakazi wa Dar tulishajizoelea kubagazwa, kudhihakiwa na kugaragazwa kimwili na kiakili. Sasa mji umepoa utadhani mate ya mgonjwa inaudhi sana.

Kama haumwondoi mkuu huyu wa mkoa basi angalau aje hata na tamko kuwa hivi sasa Wanaume wa Dar hakuna kula chips mayai. Mtu akikamatwa ashtakiwe. Hapo najua tena kutachangamka. Hasa wanaume wa Kinondoni watalalamika sana.

Chadema wameandama juzi juzi hapa... hawakupigwa hata mabomu wakati maandamo tunajua yanahatarisha usalama maana yake huyu mkuu wa mkoa mpya hana hata intelejensia ya kumwambia hilo kafeli sana aende zake.

Alishindwa hata kutengeneza chaos kwenye yale maandamano polisi wetu wapate nafasi ya kuonesha utaalamu wao wa kupiga hadi kuchakaza? Polisi wanaanza kupata baridi sasa maana ni muda hawajangamsha damu.

Kiukweli Dar haina tena mchaka mchaka. Wale wanaume ambao waliotoa tu mimba kwa wanawake na hawatoi pesa za matumizi sasa hivi wanatamba mitaani kuwa hawatatoa tena pesa kwa wazazi wenzao. Wanagawa mimba tu basi.

Mkuu wa Mkoa hatujamwona akisisitiza watu wasiende mjini bila kuoga. Hatumwoni akisimulia jinsi anavyopata raha dunia hii kuliko wengine wote. Huyu hafai ni bora tu awe mzee wa kanisa au msikiti. Mkoa umepoa sana kwenye social media hamna amsha amsha kabisa.

Hata mkewe mpaka sasa hatujamjua hatutajua ana elimu gani na alisoma wapi maana amepoa hata akina Mange na Kigogo hawatamgusa... Basi atangaze followers wa Mange na Kigogo wakamatwe angalau tuone amefanya jambo.

Ni bora umrudishe Makonda aje kuanza na wajumbe waliomnyima Kula. Hawa majina atakuwa nayo tu watafunguliwa kesi ya uhaini na uhujumu uchumi. Ndiyo. Wamehujumu uchumi pakubwa tu. Why wamwambie Makonda wapo naye bega kwa bega na kumbe wapo nyuma yake?

Hiki ni kipindi kizuri kumrudisha Makonda kwenye nafasi yake. Please arudishwe haraka.
 
Huku kwetu Malawi kunywa gongo ruhusa na kuvuta bangi si kosa la kufungwa

Sasa sijui huko Dar kama hivi vitu vinaruhusiwa

Umeandika kama mlevi anae vizia kuonja pombe ya jana atoe jibu kuwa bado haijaharibika
 
Kwani bado yupo mjini au keshatafutiwa kazi ya kufanya, maana alitutangazia hata akina Msigwa walipata tabu kweli kweli kwamba hutakiwi kukanyaga hapa town kama huna kazi na uwe umeoga.
 
Kabla hata sijasoma hoja zako naomba niwaambie tusipende kuishi kwa kukariri.

Mwacheni baba wa watu afanye kazi sio lazima apige kelele ndio mjue yeye ndio mkuu wa mkoa
mbaya zaidi hata ofisi bado hana.
 
Sarcasm at its best 😂😂😂😂😂
Kwa wale wasiojua maana ya sarcasm ndio hii. Safi kabisa. Yaani unaongea kitu kana kwamba unamaanisha kumbe humaanishi yaani.....inakujaaaaa, inakataa......au.....inakuja kwa mbaaaaaaaaliiiiiii ( in Bwege z voice)
 
Mwambie Bashite afungue bendi ya Singeli na atoe wimbo kila mwezi.
Itapendeza.
 
Akili nyingine kama sio matope ni takataka kabisa sio bora ungesema wamteuwe mjomba wako
 
Back
Top Bottom