Rais Mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera amuondolea Kinga ya kutoshtakiwa Rais wa zamani, Peter Mutharika

Wewe unadhani tunalo Bunge la kupinga matakwa yake Rais anayotaka yapite?

Hebu kuwa mkweli, kwa Spika wa "design" ya Ndugai,ndiyo wa kupinga sheria atakayoileta Rais na atakayotaka ipite?
Kama watanzania Wanawachagua wabunge wa aina ya wale waliopo unategemea Rais afanyeje zaidi ya kuhakikisha anatekeleza matakwa ya wengi ambao walimpelekea wabunge wa aina hiyo na wakampata Spika wa aina hiyo.
Yeye ataanza kuvurugana na Bunge la wananchi?
Hebu tusiwe wanasiasa Uchwara na wasio na maarifa kama Mbowe anayeua upinzani kwa umaarufu na maslahi binafsi kwa kung'ang'ania Uenyekiti.
Tuwaambie ukweli watanzania kuwa Kosa ni la kwao sio Serikali. Serikali inatekeleza kile kilichopangwa Karne nyingi zilizopita.

Miaka mingi haya tunayoyaona yalishapangwa kinachofanyika ni utekelezaji tu. Serikali imejitahidi sana kutekeleza.
Bunge kazi yake ni kuhakikisha serikali inatekeleza majukumu yake ipasavyo. Sasa kama serikali inatekeleza majukumu yake basi Bunge sio lazima liiwajibishe kila Mara.
Hayo mengine ya kuwa na wabunge wa binafsi na wanaojipendekeza ni la kuwaachia wapiga kura.

Tunaona hata wapinzani hakuna wabunge Huru zaidi ya kujipendekeza tu kwa wenyeviti wao na wengine kujipendekeza kwa CCM ili wanunuliwe na kurudishwa Bungeni kwa msaada wa bunduki na mabomu ya dola. Sasa watu kama hao hatuwezi kuilaumu serikali peke yake mana hilo ni zao la Wapiga kura wengi ambao pia wana ubinafsi huo huo.
Akitokea mzalendo mmoja kama Magufuli ni kumshukuru tu Mungu mana atajenga Roho ya kizalendo kwa Taifa letu na mwisho atatumia uzalendo wake kutuachia Katiba na sheria nzuri.
Usifikiri Mh. Rais haoni madhaifu yaliyopo lakini hana uwezo wa kulipinga Bunge moja kwa moja kama anavyoweza kumpinga DAS mhuni na Malaya Malaya hadharani.
 
Wewe ndiyo unasema wananchi ndiyo wanachagua wabunge.......

Lakini katika hali halisi ya TZ ya Leo, ni Rais ndiye anayewachagulia wananchi hao wabunge wao majimboni kwao

Wewe hakuwahi kumsikia Rais Magufuli akisema waziwazi kuwa kura za maoni huko majimboni kwenu si lolote wala chochote, kwa kuwa itategemea yeye Mwenyekiti, kaamkaje siku hiyo ya kuendesha kikao cha Kamati Kuu, anaweza akawakata no 1 hadi no 3 ya walioongoza kwenye kura ya maoni ya majimboni kwenu na yeye akamchukua no 4 na asitoe sababu yoyote, ni kwa nini amewakata wale wote watatu walioongoza kwenye kura ya maoni jimboni kwenu!
 
Huu muswada uliopelekwa hivi karibuni bungeni kufanyiwa marekebisho unaondo kinga ya kuwashitaki viongozi? Au umeleta utaratibu mwingine wa kuwashitaki viongozi wakiwa katika utendaji wao, ambapo lazima uthibishe namna haki yako ilivyoathirika na mashitaka yanapitia kwa Ag. Au Chadema kushindwa uchaguzi 2020 ndio mnatafuta kisingizio kila kona.
 
Huu ndio ukosefu wa kufikiri kwa mapana. Rais alitolea mfano jinsi Cc ya chama chake inavyofanya mchujo kuangalia namna mgombea kura za maoni alivyoshinda na uadilifu wake. Wewe unapotosha na kusema uongo wako.
 
Kizungumkuti ni pale ambapo sipendi retroactive laws halafu pia sipendi presidential immunities.

Ndiyo maana nikauliza.
Hii taarifa inaweza kuwa ni misleading ama imeongezwa chumvi.

Maana waandishi wa habari huwa wana tabia ya kuvamia taarifa bila kuzihakiki usahihi wake neno kwa neno.

Si ajabu "presidential immunity" inayozungumzwa hapa inamaanisha kitu tofauti kabisa.

Otherwise, kama taarifa ni ya kweli, nadhani huyo Rais mpya amepotosha makusudi kwa manufaa ya kisiasa tu.

Nimeangalia Katiba ya Malawi inasema kwamba Rais anaweza kushitakiwa akiondoka madarakani. (the wording of that provision of the constitution is a bit complex, but i believe that to be the correct meaning from a number of case laws i have read which have interpreted the meaning of those types of immunities).

Sasa huyu Rais mpya naona ni msanii tu! Anajipa umaarufu kwa kitu ambacho kinawezekana hata kama asingesema.

Labda angesema atamchukulia hatua, na sio "atamuondolea kinga" kwasababu hiyo kinga haipo in the first place.
 
Huu ndio ukosefu wa kufikiri kwa mapana. Rais alitolea mfano jinsi Cc ya chama chake inavyofanya mchujo kuangalia namna mgombea kura za maoni alivyoshinda na uadilifu wake. Wewe unapotosha na kusema uongo wako.
Yeye Mwenyekiti kwa sasa ndiyo mwenye uwezo wa kumpa ubunge mbunge kwenye jimbo husika........

Wewe hukumsikia kule mikoa ya Kusini, akimwambia msanii mvaa "milegezo" Harmonize akachukue fomu ya ubunge kule Tandahimba?

Hivi wewe unadhani wananchi wa Tandahimba wako tayari kuwa na mbunge wa design ya msanii Harmonize?

Hilo ni chaguo lake Mwenyekiti mwenyewe kwa kuwa msanii huyo ametoa wimbo wa kumsifu na kumpongeza na wala siyo chaguo la wana Tandahimba
 
Wewe unajua vipi? Kama alikuwa anatania? Maana huwa anapenda utani.
 
Wewe unajua vipi? Kama alikuwa anatania? Maana huwa anapenda utani.
Nyinyi kwa kila kitu anachosema Mwenyekiti wenu hivi sasa mnaita eti alikuwa akifanya utani........

Wewe mwenyewe unajua kuwa taasisi ya Urais ni kubwa sana katika nchi, haiwezekani afanye mzaha mzaha wakati analihihutibia Taifa, utadhani mtu wa kijiweni anapiga stori!
 
Kwa hiyo unataka awe amenuna kama anagombana na wananchi wake? Lazima achomekee wacheke kidogom
 
Sipati picha mara Mh. Rais was JMT, Tundu Lissu anapokuwa amemaliza kutamka maneno haya katika kiapo chake ya "Mungu nisaidie" kwamba, baada ya nusu saa tu nini kitafuata....

I am sure haya yatafanyika immediately kabla mtu hata hajaingia ofisini;

1. Atatumia "Presidential decree" kufuta na kuondoa kinga za kutoshitakiwa kwa Marais wote waliopita, Maspika wa Bunge na Majaji baadhi ili waanze kulipia matendo yao...

2. Marais wote walio hai ( Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli) wataanza na kifungo cha kutotoka ndani (lockdown) wakati utaratibu wa kuwashitaki ukiandaliwa...!

3. Ku - seize bank accounts zao zote za ndani na nje ta nchi ikiwemo assets zao kama majumba, Magari nk nk...

Sipati picha, Magufuli ile 1.5trn sijui atakutwa ameiweka wapi tu....!!
 
Na yule jamaa yetu pale Bungeni kila akipelekewa muswada wa sheria tayari kashapitisha.. Angalieni yanayoendelea kwa majirani hapo endeleeni kujiwekea kinga halafu mfanye yasiyofaa mkamatwe kama ndege
 
16 July 2019
Mwanza, Tanzania

"Mimi mfungwa mtarajiwa..hapa ni mtakuja" - Rais Magufuli


Rais wa Tanzania, Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli ametoa zawadi ya ng’ombe watatu na magunia 15 ya mchele kwa wafungwa na mahabusu katika Gezeza Kuu la Butimba jijini Mwanza akisema na yeye ni kama mfungwa mtarajiwa ......
Source: ITV Tanzania
 
Ulishwahi tazama movie ya the last king of scotland, pale wakati Idd Amina anwahutubia waganda anasema Mimi na nyinyi ni dugu, wananchi wanashangilia. Yule dogo akawafurahi akasema jamaa inaelekea anapendwa na anajali wananchi sana, mke wa mchungaji akamjibu, hili siyo jipya kwa afrika kila inapotokea mapinduzi au uchaguzi wa raisi mpya mambo uwa hivi ahadi kede kede watu kufurahi kuwa ndiyomabadiriko lakini baada ya muda mambouwa yale yale.
Mpeni muda utasikia
 
You are a gentleman and a scholar.

This kind of analysis makes JF a priceless resource.
 
Wapi nilipoandika hivyo? Kama sheria zimekaa UOZO na MADUDU kwanini ZIKUMBATIWE badala ya KUFUTWA!?
Wapi nilipodai umeandika hivo?
Unadai sheria hubadilishwa na mtu kisa zina uozo, kwahiyo rais wao ndiye anayebadili sheria na kuweka anazotaka yeye?
Hata kama sheria zina uozo, hazibadilishwi na mtu kisa ni mchungaji sijui katoka kanisani. Bunge au mahakama ndo inabadili katiba/vifungu vya sheria. Sio kazi ya rais.
 
Huyo kachukua hayo kaamuzi kimhemuko! Yani ile mizuka na mihemko kama ya kina Lisu ndio iliyopelekea huyo jamaa kuchukua hayo maamuzi.

Lakini akikaa akatulia mizuka na mihemko ikitulia atajiona kumbe kachimba kaburi atalotumbukia hata yeye mwenyewe!
 
Bora awapige chini wezi wanaojifanya wema.

Hata awamu ya tatu na ya NNE watu walikatwa.
 
Mkuu,acha kufananisha mkuu wa meza na vitu vya hovyo hovyo,takataka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…